Jeshi la Polisi lianze uchunguzi kwa kuwahoji waliokuwemo kwenye basi moja na Ali Kibao, walioona tukio la kutekwa

Hahahahahaha wanajua yoote .....wewe ndio hujui.....jibu moja tu Kifo ni kifo tu
 
Hilo Jeshi la Polisi, ndiyo "main suspects" wa unyama huu wa kutekana na kuuwana.
Full Stop
Sheria ilipopitishwa tulikaa kimya sasa jamaa wana power na hawagusiki wana kinga....sijui kama tunaelewanaa
 
Sheria ilipopitishwa tulikaa kimya sasa jamaa wana power na hawagusiki wana kinga....sijui kama tunaelewanaa
Bunge lenyewe linalopitisha sheria ni la chama kimoja, sisi wengine hatupaswi kulaumiwa😳
 
Mimi naviamini kwaaslimia mia mbili vyombo vyetu vya usalama, mnadhani hawajui kazi yao. Hapa Afrika hakuna vyombo makini vya ulinzi na usalama kama vyombo vya Tanzania, vina watu wenye ujuzi wa hali ya juu kupita kiasi.Kwahiyo viachwe wala visifanyiwe shikizo wakaamua wenyewe ni dakika sifuri tu.
 
Mwenye picha ya eneo la Kibo-Tegeta aipandishe hapa jukwaani tuone ambapo basi la Tashrif lilisimamishwa na abiria mmoja akashushwa kwa mtutu wa bunduki mchana kweupe wakatokemea naye kusikojulikana.

Kwa namna ya eneo la Kibo-Tegeta lilivyo haiwezekani kuna wakati huwa hakuna watu waliosimama au wanatembea mpaka usiku wa manane.

Pili eneo la sehemu alipotupwa abiria yule pale Ununio pako peupe hakutupwa upande wa pili ambao una miti ya miiba , bonde la msitu wa mikoko mkabala na majengo ya NSSF yaliyotelekezwa miaka kadhaa iliyopita. Sehemu aliyotupwa kuna ukuta na ndani ya ukuta kuna kibanda cha mlinzi wa eneo ambaye anajishughulisha na kilimo cha nyanya na anapanga nyanya kwa mauzo kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa moja jioni.

Endapo kungekuwa na kutiliwa maanani malalamiko ya CDM mamlaka wangekuwa wameshapata ukweli kwamba abiria alipelekwa saa ngapi pale kando kando ya barabara ya Ununio (usiku wa manane).
Utu wa binadamu ni sharti uheshimiwe hata kama kuna tofauti za namna yoyote ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…