Jeshi la Polisi limekamilisha Uchunguzi dhidi ya Fatma Kigondo, jalada liko kwa DPP

Jeshi la Polisi limekamilisha Uchunguzi dhidi ya Fatma Kigondo, jalada liko kwa DPP

Jeshi la Polisi limesema limeshafanya Uchunguz wa kina dhidi ya Afisa wa Polisi anayetajwa kwa jina la 'Fatma Kigondo' ikiwa ni pamoja na kupata maelezo ya watu mbalimbali

Kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, imeeleza kuwa Jeshi limeshachukua maelezo ya Afisa huyo na tayari jalada lake limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)

Afisa huyo wa Polisi amekuwa akitajwa kuhusika katika kuratibu na kuwezesha tukio la Ubakaji na Ulawiti lililofanywa na Watuhumiwa 5 dhidi ya 'Binti wa Yombo' ambapo tayari kesi yake ipo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma.

Soma Pia:' Afande' Fatma Kigondo anayedaiwa kusaidia Binti wa Yombo afanyiwe Ukatili wa Kingono afunguliwa Kesi ya Jinai

View attachment 3077939
Yaani wabakane wao halafu yeye awe mratibu. Ushahidi hapa ni mgumu sana labda kuwe na mawasiliano ya maandishi na sauti yaliyorekodiwa. Vinginevyo hii kesi haina mashiko kwa huyu mtuhumiwa.

Wabakane wao na vifaa vyao halafu afande ahusike. Hata kama ni kweli aliratibu, wajipange sana kwa ushahidi
 
kigogo._.2014_8c4fa6c5017741f9bd7c16e4cc336924.jpg
 
Wabakane wao na vifaa vyao halafu afande ahusike.
Dk za mwisho,ile clip inaonesha analazimishwa amwombe msamaha afande.
Kabla hawajaliamsha Kule twita,Kila kitu walishakijua,swala lingine linaloleta sintofahamu,mume WA huyo mtuhumiwa alishafariki 2021.
 
Yaani wabakane wao halafu yeye awe mratibu. Ushahidi hapa ni mgumu sana labda kuwe na mawasiliano ya maandishi na sauti yaliyorekodiwa. Vinginevyo hii kesi haina mashiko kwa huyu mtuhumiwa.

Wabakane wao na vifaa vyao halafu afande ahusike. Hata kama ni kweli aliratibu, wajipange sana kwa ushahidi
Wanaweza kumpeleka mahakamani. Ila kumfunga hawawezi.

Labda, Jamhuri iombe mitandao ya simu ipekue mawasiliano yake kama walitumana kwa njia ya simu.

Japo kua bado ni ngumu, since shahidi wa kwanza anakua ni yule nyundo ambao hata madai yao kubaka washaanza kuyakataa.

Hivyo, Jamhuri itakua na kibarua kizito sana kudeal na huyu mama
 
Tutaishia kuandika kulaumu bila kuchukua hatua. Wakimsafisha pelekeni kesi kwenye mahakama za kutetea haki za binadamu internationally. Msisumbuke na ku appeal.
 
Dk za mwisho,ile clip inaonesha analazimishwa amwombe msamaha afande.
Kabla hawajaliamsha Kule twita,Kila kitu walishakijua,swala lingine linaloleta sintofahamu,mume WA huyo mtuhumiwa alishafariki 2021.
Hapo sasa. Inawezekana adui zake wanataka kumharibia tu. Kulazimishwa kumtaja sio ushahidi usiotia shaka.

Na hilo sasa la mume kuwa hayupo duniani kama ni kweli.
 
Wanaweza kumpeleka mahakamani. Ila kumfunga hawawezi.

Labda, Jamhuri iombe mitandao ya simu ipekue mawasiliano yake kama walitumana kwa njia ya simu.

Japo kua bado ni ngumu, since shahidi wa kwanza anakua ni yule nyundo ambao hata madai yao kubaka washaanza kuyakataa.

Hivyo, Jamhuri itakua na kibarua kizito sana kudeal na huyu mama
Ni ngumu kwakweli. Ngoja tuone
 
Back
Top Bottom