Jeshi la Polisi limemkamata James Damson Ngole (34) kwa kujifanya Afisa Usalama na kutapeli watu kupitia Whatsap

Jeshi la Polisi limemkamata James Damson Ngole (34) kwa kujifanya Afisa Usalama na kutapeli watu kupitia Whatsap

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Jeshi la Polisi limemkamata na linamshikilia mtuhumiwa mmoja aliyetambulika kwa jina la James DamsonNgole (34) kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya utapeli huku akijifanya ni Afisa Usalama.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia kivuli cha idara ya usalama kufanya matukio mbalimbali ya kuwalaghai wananchi.

Katika upekuzi uliofanywa na Jeshi hilo, ilibainika kupitia simu yake ya mkononi katika mtandao wa WhatsApp, mtuhumiwa alikuwa akitumiwa na kuhifadhi nakala za vyeti mbalimbali vya taaluma vya watu waliohitimu katika vyuo na shule mbalimbali.

"Jeshi La Polisi limemkamata mtumiwa mwingine ambaye amefahamika kwa jina la James Damson Ngole, miaka 34. Huyu yeye ni, anajihusisha na makosa ya utapeli kwa kujifanya ni afisa usalama. Na kujifanya kwake afisa usalama, anatumia kivuli hicho kufanya matukio mbalimbali ya kitapeli.

Lakini kwenye upekuzi wakati akiwa anafanya utapeli wake, tumebaini kwamba alikuwa na simu yake upande wa mtandao wa WhatsApp imebainika kwamba amekuwa akitumiwa na nakala mbalimbali za vyeti, vya taaluma, walio maliza katika vyuo mbalimbali pamoja na shule, na alikuwa akiwa anawaahidi kuwatafutia kazi sehemu mbalimbali serikalini.

Yeye amekuwa akifanya mawasiliano aidha kwa njia ya WhatsApp lakini na kwa njia ya kawaida. Na mara nyingi amekuwa akiwashawishi watu mbalimbali kuhusiana na utoaji wa ajira. Na amekuwa akidimandi mara kadhaa kwamba awatumie hivyo vyeti ili aweze kuwapatia ajira katika maeneo tofauti tofauti"



 
Nyumbu kama kawaida wanalizwa tu
Mwanaume kujilegeza namna hii haipendezi
Screenshot_20260611-101536.png
 
Wakina Mwamposa wanauza mpaka udongo, mbona hawakamatwi?
 
Back
Top Bottom