Jeshi la Polisi limewakamata na kuwahoji waliovunja vioo Treni ya SGR, ni watoto wa miaka 12 na 16

Walitumia manati kurusha hayo mawe?
 
Juzi mama alipanda hiyo treni, kinachofanyika sasa ni kutaka rais aongelee hujuma hewa zinazofanyika, hata hivyo mbona mabasi nayo hutokea yakarushiwa mawe lakini hatujasikia polisi wakiingilia kama hili?
 
Jambo lililofanywa na hawa watoto ni baba na nilakukemewa vikali ili lisiwahi rudia tena kutetea uovu ni mbaya sana na uharibifu wa Mali ya uma. Hatua zilizochukuliwa ni sahihi na elimu itolewe kwa wakazi wote wanaoishi maeneo jirani na train inapopita. Na sio kurusha mawe tu hata kupita ama kulisha maeneo ya kupitia train ni hatia inaweza hababisha madhara makubwa. Kuchukua tahadhali ni bora kuliko kusubiria majanga..
 
Tanganyika Kuna vituko!
Polisi tuwekeeni picha na video nasi tuone!
Inawezekana hao watoto baba zao ni wamiliki wa mabasi ya abiria.
Mwisho wa kunukuu.
 
Chanzo cha kufanya uharibifu huo ni baada ya kuona treni ikipita wakarusha mawe kwa pamoja ili kuona kama mawe waliyoyarusha yataweza kushindana na mwendo wa treni.
  1. Je ilikuwa ni usiku? Walitumia mbinu gani kuwatambua kuwa kweli ni wao beyond reasonable dought
  2. Je ilikuwa ni mchana? Hakuna abiria walioshuhudia tukio hilo? Je ni kweli waliowaona ha watoto wakirusha mawe?
  3. Hiyo reli ina fence na iko takribani mita 15 kutoka reli, hao watoto walikuwa na nguvu kiasi gani na mawe ya uzito gani mpaka yaende umbali huo na kuvunya vioo ambavyo I believe ni toughened glasses?
Tuanzie hapo
 
Hili nalo ni la kujiuliza, na kwa umri huo nadhani vitakuwa vile vimawe kama wanapiga ndege tu,
Huenda ni hujuma zinafanywa na watu wenye nguvu kifedha ila tunazugwa
 
Mm nashauri hao ma-junior waachiwe tuu mana wakikasirika watakataa kula 😎

Alisikika mwanaharakati wa watoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…