Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Taarifa kwa vyombo vya Habari.
Dar es salaam, 16/11/2021
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linafanya uchunguzi wa tukio la kijana anayefahamika kwa jina la Issa Kassim (20) mkazi wa Goba Wilaya Kinondoni kudaiwa kupigwa na askari wa Jeshi la Polisi na kusababishiwa maumivu makali.
Kijana huyo inadaiwa alikamatwa tarehe 10 Novemba 2021 kwa tuhuma za wizi wa TV na baadae kupigwa huku ikidaiwa ndugu zake walikuwa wakiombwa rushwa ili aachiwe. Malalamiko hayo ni mazito hivyo Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limeshafungua jalada la uchunguzi na mifumo ya kisheria itatumika ili kupata ukweli wa jambo hilo na ikibainika ni kweli hatua za kisheria na kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wahusika, Uchunguzi huo tayari ulikwisha anza.
MULIRO J. MULIRO– ACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.
Kuona malalamiko soma hapa>> Goba, Dar es Salaam: Polisi watuhumiwa kumpiga mtu mmoja na kumjeruhi