Jeshi la Polisi Mbeya: Tunachunguza kutoweka kwa Shadrack Chaula, aliye na taarifa za mahali alipo atutaarifu

Jeshi la Polisi Mbeya: Tunachunguza kutoweka kwa Shadrack Chaula, aliye na taarifa za mahali alipo atutaarifu

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana Agosti 8,2024, Kamanda Kugaza amekiri kuwepo kwa tukio la kutoweka kwa kijana Shadrack huku akiomba wananchi kutoa ushiriano.

Jeshi la Polisi limesema kuwa lilipokea taarifa na kwa sasa wako katika uchunguzi kujua watu waliomchukua na kuomba wananchi kutoa ushirikiano ili aweze kupatikana.

Shadrack hapo awali alihukumiwa kulipa faini ya Sh5 milioni au kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukiri kosa la kuchoma picha ya Rais ila kifungo hicho baada ya wananchi kuchanga na kulipa faini hiyo kisha kufanikiwa kumtoa katika Gereza la Ruanda Mkoa lililoko mkoani Mbeya.

View attachment 3065253

- Baba Chaula: Polisi niambieni mwanangu kama yu hai tu basi inatosha, nahisi roho yangu inashindwa kuvumilia haya maumivu
- Aliyehukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa kuchoma picha ya Rais amechukuliwa na watu wasiyojulika, mpaka sasa hajulikani alipo
Polisi mkiwa na mtuhumiwa mnagoma kukiri mnaye mtuhumiwa, mnapotaka msaada kutoka kwa wananchi hao wananchi wanao uhakika gani kwamba mtuhumiwa hayuko mikononi mwenu! Polisi mkifanya mambo yenu kwa uwazi wa kutowaficha watu mnaowateka wananchi nao watakuwa mbele kuwasaidia, ni swala la nipe nikupe au nikune mgongi wangu nami nikukune wako.
 
HUYU kijana ANAE semekana ametekwa na wasio JULIKANA aliichora picha yeye mwenyewe kwa pencil yake , na kwa kutenga muda wake.

Alivyoichora halikuwa kosa na aliichora akiwa na matumaini yakuwa iko siku picha ile itamfikia Mh Rais ili walau impatie kipato picha limekaa weeee hakuna lolote na maisha yakazidi kumtandika na huku kwenye mitandao anaona Rais anatetea ununuzi wa gari za kifahari kwa ajili ya watumishi AMBAO wengi wao ni wabadhilifu wa fedha za Umma
Pasipo kujali muda alio upoteza kalamu,na akili kubwa anaamua kuichoma moto kazi ya mikono yake mwenyewe je kosa lake ni lipi?

Je kosa kuchoma picha ya Rais TU au hata akichoma yangu LINAKUWA ni kosa?
 
INAUMA SANA.

CHA AJABU SASA:

HUTASIKIA VIONGOZI WA DINI KAMA KINA SHEIKH ZUBERI, MWAMPOSA, MALASUSA, KILAINI AU RUWAICHI WAKIKEMEA MATESO KAMA HAYA KWA WATANGANYIKA. WANAANGALIA MATUMBO YAO TU.
 
Tatizo linakuja kuwa kila mtu anataka aonekane kuwa anafanya kazi ili asogezewe mirija na mama.

Nina hakika asilimia 100 Chura Kiziwi na mapungufu yake yote hawezi kuidhinisha mtu atekwe sababu tu kachoma picha yake. Tatizo ni vijakazi wake ndio wenye kimbembele.

Mtu anataka kuhalalisha matumizi ya pesa kama kwa ajili ya ulinzi, ukiuliza ulinzi gani utaambiwa kudhibiti wanaoleta uchochezi mitandaoni, ndio hao wanaotekwa. Kumbe pesa yote inaliwa na watoto wa watu wanaumizwa.
 
Katika Quran, siku hii imeelezwa kwa undani kama siku ya mwisho na ya kuhesabu, ambapo kila mtu atajibu kwa matendo yake. Baadhi ya aya zinazohusiana na siku hii ni:

  1. Surah Al-Zalzalah (99:1-8): "Siku hiyo ardhi itatoa taarifa zake, na binadamu atajua matendo yake; kwa sababu Mwenyezi Mungu atamfunulia. Siku hiyo watu wataonekana wakigawanyika kwa makundi ili kuona matendo yao. Kwa hivyo, atakaye fanya wema wa chembe moja atauona, na atakaye fanya uovu wa chembe moja atauona."
  2. Surah Al-Qariah (101:1-11): "Siku ya Kiyama! Siku hiyo itakuwa ya kuvuruga na kutikisa. Watu wataonekana wakigawanyika kama makundi, na kazi zao zitathaminiwa kwa uzito."
  3. Surah Al-Haaqqa (69:13-18): "Siku ya Kiyama! Siku hiyo kila mmoja atapata malipo kwa kile alichofanya, na kila jambo litahesabiwa."
 
Afya ya akili ni jambo muhimu sanaa

Je uwapo na hasira / furaha ilopitiliza kiasi huwa unafanya Nini kurudi kawaida?
 
Daaaa wanakuua kisa kuchoma picha ya Rais tu na sio ile official wanaweka maofisiniii.....
 
Tatizo linakuja kuwa kila mtu anataka aonekane kuwa anafanya kazi ili asogezewe mirija na mama.

Nina hakika asilimia 100 Chura Kiziwi na mapungufu yake yote hawezi kuidhinisha mtu atekwe sababu tu kachoma picha yake. Tatizo ni vijakazi wake ndio wenye kimbembele.

Mtu anataka kuhalalisha matumizi ya pesa kama kwa ajili ya ulinzi, ukiuliza ulinzi gani utaambiwa kudhibiti wanaoleta uchochezi mitandaoni, ndio hao wanaotekwa. Kumbe pesa yote inaliwa na watoto wa watu wanaumizwa.
Upo sahihi... "Fungu maalum kwa vyombo vya ulinzi na usalama kudhibiti wachochezi"...kumbe wizi mtupu. Huyu mama amekosa washauri watamdanganya KILA kukicha.
 
Tatizo linakuja kuwa kila mtu anataka aonekane kuwa anafanya kazi ili asogezewe mirija na mama.

Nina hakika asilimia 100 Chura Kiziwi na mapungufu yake yote hawezi kuidhinisha mtu atekwe sababu tu kachoma picha yake. Tatizo ni vijakazi wake ndio wenye kimbembele.

Mtu anataka kuhalalisha matumizi ya pesa kama kwa ajili ya ulinzi, ukiuliza ulinzi gani utaambiwa kudhibiti wanaoleta uchochezi mitandaoni, ndio hao wanaotekwa. Kumbe pesa yote inaliwa na watoto wa watu wanaumizwa.
Kwanini asikemee matukio hayo? Kukaa kwake kimya kunamaanisha kuwa matukio yana baraka zake. Anastahili kuwa mlaumiwa namba moja na haikwepeki, hakuna cha vijakazi wala wasaidizi.

Kipindi cha nyuma nilikuwa na imani sana na wema wake na niliona katika suala la usalama wanachi (bila kujali tofauti zetu kimitazamo nk) sasa tupo mikono salama, lakini sasa naona u-jiwe unamuingia kwa kasi naye. Naona maisha ya jengo jeupe yamemnogea sana naye kaanza kuwa Belishaza kama mtangulizi wake.

Mwanadamu akijipata ana tabia ya kujisahau na kujawa na kiburi cha uzima na ukwasi wakati mwisho wake ukifika anazima tu kama mshumaa hata ukwasi wake usiweze kumsaidia chochote. Mama asijisahau bhana maisha ni ubatili mtupu, akumbuke mwisho wa anayefuata nyendo zake ulivyokuwa.
 
Afya ya akili ni jambo muhimu sanaa

Je uwapo na hasira / furaha ilopitiliza kiasi huwa unafanya Nini kurudi kawaida?
Mi nikikasirika naondoka pale mahali nilipokasirishwa! Hapo kurudi ni kesho au next week au sirudi kabisa kama ni kwa mtu! Wala siongei kitu!! Maana nakuwa nimejaa hasira za kuua mtu, huyooo nasepa zangu!! Ujinga huwa sipendi kabisa!!
 
HUYU kijana ANAE semekana ametekwa na wasio JULIKANA aliichora picha yeye mwenyewe kwa pencil yake , na kwa kutenga muda wake.

Alivyoichora halikuwa kosa na aliichora akiwa na matumaini yakuwa iko siku picha ile itamfikia Mh Rais ili walau impatie kipato picha limekaa weeee hakuna lolote na maisha yakazidi kumtandika na huku kwenye mitandao anaona Rais anatetea ununuzi wa gari za kifahari kwa ajili ya watumishi AMBAO wengi wao ni wabadhilifu wa fedha za Umma
Pasipo kujali muda alio upoteza kalamu,na akili kubwa anaamua kuichoma moto kazi ya mikono yake mwenyewe je kosa lake ni lipi?

Je kosa kuchoma picha ya Rais TU au hata akichoma yangu LINAKUWA ni kosa?
Liajabu lakweli.
 
Hii Serikali yaani inafanya mambo ya ajabu ambayo hayana tija matokeo yake Kodi zetu zinatumika kwa vitu ambavyo wala vilikuwa havina msingi..., Kwanini walimshika in the first place ?
 
Back
Top Bottom