GE2025 Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe imetoa elimu kwa bodaboda kuepeuka kutumika vibaya kipindi cha uchaguzi

GE2025 Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe imetoa elimu kwa bodaboda kuepeuka kutumika vibaya kipindi cha uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Katika kuhakikisha Uchaguzi Mkuu 2025 unafanyika kwa usalama na amani Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kupitia watendaji wake wa kata limeendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali katika jamii, wakiwemo wasafirishaji wa abiria kwa kutumia Pikipiki maarufu kama bodaboda, kuhusu umuhimu wa kujiepusha kutumika vibaya kisiasa kabla, wakati na baada ya uchaguzi

Akizungumza Julai 13, 2025 na wasafirishaji hao wa kijiwe cha Transfoma, katika ukumbi wa Karibu Tena uliyopo Kata ya Mwakakati Mji wa Tunduma Wilaya ya Momba, Polisi kata wa kata hiyo, Mkaguzi wa Polisi Robert Kasunga aliwahimiza wasafirishaji hao kujiepusha na vitendo vya fujo, ushawishi wa kisiasa wenye nia ovu, pamoja na usafirishaji wa watu wasiofuata sheria za kuingia nchini

Soma pia: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Waendesha bodaboda mna nafasi kubwa sana katika jamii, lakini pia ni rahisi kutumika vibaya na watu wenye nia mbaya kisiasa. Nawaomba muwe makini, mchague usalama na amani kuliko tamaa ya fedha,” alisema Mkaguzi Kasunga

Mkaguzi Kasunga, alisema kuwa kupitia vikundi vya Ulinzi Shirikishi na Viongozi wa Vijiwe vyote vya Bodaboda ndani ya kata hiyo kwa usimamizi wake ataendelea na mipango mikakati wa
kuwachukulia hatua za kisheria dhidi ya yeyote atakayebainika kuhatarisha amani au kushawishi wengine kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani katika kata hiyo

songwe.png



Chanzo: Zanzibar_mpya
 
Bodaboda wanatumikaje vibaya wakati wa uchaguzi??
 
Na sisi boda boda tunaandaa semina ya kuwapa Polisi wasitumike na wana siasa vibaya
 
Back
Top Bottom