Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limesema linamshikilia kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani humo Swahibu Juma Mwanyoka kutokana na tuhuma zilizoripotiwa.
Katika taarifa iliyotolewa na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi leo Jumatano Machi 12,2025 imeeleza kuwa uchunguzi unaendelea ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.
"Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linathibitisha kukamatwa kwa Swahibu Juma Mwanyoka kwa tuhuma zilizoripotiwa, uchunguzi unaendelea ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria,"imeeleza taarifa hiyo ya Kamanda Mchunguzi.