Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kurusha fedha ovyo sakafuni

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kurusha fedha ovyo sakafuni

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
My Take: Hili la Mwanza liwe fundisho kwa wengine kuheshimu pesa.

Ikumbukwe BoT walipiga marufuku huu upuuzi.👇👇

==========

JESHI la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kurusha fedha ovyo sakafuni wakati wakimtunza bwana harusi na bibi harusi katika sherehe iliyokuwa ikifanyika katika moja ya kumbi za starehe jijini hapa.

Akithibitisha kukamatwa kwa watu hao, Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Wilbroad Mutafungwa, alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Julai 7, mwaka huu, katika moja ya ukumbi wilayani Ilemela wakati wa sherehe ya Robert Shija.

Alitaja watuhumiwa hao kuwa ni Majani Mabele (47), mfanyabiashara na mkazi wa Nyansaka, Kiruma Lucas (31), mfanyabiashara na mkazi wa Ibanda, Sharifu Dotto (29), mfanyabiashara na mkazi wa Kiseke na Seleman Mbuga (39), mfanyabiashara na mkazi wa Nyamanoro wilayani Ilemela.

“Wote hao walionekana katika kipande cha video kilichokuwa kimerushwa mitandaoni wakitupa chini noti za fedha ya Kitanzania za Sh.10,000 na Dola za Kimarekani, huku wengine wakizizoa kutoka sakafuni kama uchafu," alibainisha DCP Mutafungwa.

IPP
 
Hatutoki kwenye mjadala wa Chadema na kile kilichotokea Mbeya.
 
Back
Top Bottom