Johnson Yesaya
Member
- Jan 1, 2013
- 21
- 31
1.0 Utangulizi.
Jeshi la polisi la Tanzania, ni kati ya majeshi mengi Afrika ambayo yanalaumiwa sana na wananchi kwa ukiukaji mkubwa wa sheria na haki za binadamu ikiwemo kuua raia katika mazingira ya kutatanisha, kupora mali na fedha za wananchi wanapokuwa mikononi mwa polisi, kuwatolea wananchi lugha chafu za matusi wanapoenda katika vituo vya polisi, rushwa, kuweka watu kizuizini kinyume cha sheria na mengineyo mengi. Sasa uvunjifu huu wa sheria unachochewa na mambo mengi kama ifuatavyo;
i. Vigezo duni vinavyotumika kuajiri polisi wakati wa ajira.
Elimu za askari polisi, wengi ni kidato cha nne na hawana elimu yoyote ya sheria. Ni askari wachache tu ambao wamefika kidato cha sita, vyuo, na ambao wamesoma sheria. Hili ni jambo baya sana kuwa na askari ambao hawajasoma hasa sheria. Unawezaje kusimamia sheria ikiwa wewe mwenyewe huzijui sheria?
ii. Nguvu au ushawishi wa kisiasa katika utendaji kazi wa jeshi la polisi.
Mara nyingi jeshi la polisi hutumiwa kama chombo cha kisiasa na viongozi wa serikali kwa manufaa ya kisiasa. Hii huathiri uhuru na uadilifu wa jeshi la polisi katika kutekeleza majukumu yake kwa haki na bila upendeleo.
iii. Mafunzo duni.
Mafunzo yasiyo ya kiwango cha juu na yasiyozingatia haki za binadamu na utawala wa sheria yanachangia polisi kutekeleza majukumu yao vibaya. Mafunzo bora na endelevu ni muhimu kwa maafisa wa polisi ili waweze kushughulikia changamoto za kiusalama kwa njia za kitaalamu zaidi kulingana na mabadiliko ya teknolojia.
iv. Ukosefu wa vitendea kazi.
Jeshi la polisi linakabiliwa na uhaba wa rasilimali muhimu kama vile vifaa vya kisasa, magari, na teknolojia, ambayo inasababisha ugumu katika utekelezaji wa majukumu yake kwa ufanisi. Hivyo wanajikuta wakifanya kazi zao kwa kiwango cha chini kabisa na kuathiri wananchi.
v. Mishahara midogo na mazingira mabaya ya kazi.
Mishahara duni na mazingira magumu ya kazi yanachangia kupungua kwa motisha miongoni mwa maafisa wa polisi. Hali hii inawasukuma baadhi yao kutafuta njia za haraka za kujiongezea kipato kama vile kuomba rushwa.
vi. Kurithi jeshi la kikoloni na kuendelea kufuata utaratibu wa kikoloni katika kuhudumia wananchi.
Jeshi letu la polisi ni jeshi tulilolirithi kwa wakoloni, sheria tunazozitumia leo nyingi zilirithiwa kutoka kwa wakoloni wa waingereza. Na ikumbukwe kuwa, wakoloni walitengeneza jeshi onevu, kandamizi, lisilozingatia haki za binadamu kwaajili ya kumkandamizi mtu mweusi. Kwahiyo uovu huo ulirithiwa na jeshi la polisi la leo na unaendelea kutumika kukandamiza wananchi mpaka sasa.

2.0 Nini Kifanyike Kuboresha Jeshi la Polisi.
i. Vigezo au sifa za kupata ajira ya polisi vipandishwe zaidi.
Chanzo ; Jeshi la polisi Tanzania I kutoka mtandao wa X.Kwa kuangalia vigezo au sifa hizo za kujiunga katika jeshi la polisi basi utagundua sifa hizi ni ndogo sana ukilinganisha na kazi zingine katika utumishi wa umma ambazo huanza kuajiri watu wenye stashahada na shahada tu.
Mapendekezo.
Sifa za kuajiri askari polisi ziwe kuanzia elimu ya kidato cha sita na kuendelea na kigezo cha stashahada ya sheria. Mwajiriwa lazima awe amehitimu na kufaulu kidato cha sita na mwenye stashahada ya sheria. kwa waajiriwa wa kuanzia shahada, ziwe ni shahada za sheria au zinazoendana na sheria kama (law enforcement). Stashahada na shahada zingine pia wanaweza kuajiriwa kuzingatia mahitaji ya jeshi. Huwezi kuwa polisi hujui sheria ni ajabu.
ii. Uanzishwaji wa tume huru ya polisi
Ianzishwe tume huru ya polisi itakayokuwa na mamlaka ya kusimamia na kuongoza jeshi la polisi bila kuingiliwa na wanasiasa. Tume hii inapaswa kuwa na wajumbe wanaochaguliwa kwa kuzingatia weledi, uadilifu, na uzoefu wao, na si kwa misingi ya kisiasa. Tume hii itafanya kazi bila kusukumwa na wanasiasa na kwa kufuata sheria pekee. Watu katika serikali wenye mamlaka juu ya polisi kama waziri wa mambo ya ndani na waziri wa ulinzi na usalama walazimishwe na sheria kupitisha amri zao katika tume hiyo kabla ya kutekelezwa na jeshi la polisi na hii itasaidia sana kuliondoa jeshi la polisi katika mikono ya wanasiasa.
Mfano mzuri wa tume huru ya polisi ni Tume ya Polisi ya Uingereza, inayojulikana kama "Independent Office for Police Conduct (IOPC)." Tume hii ilianzishwa ili kuchunguza malalamiko dhidi ya polisi na kuhakikisha uwajibikaji na uadilifu ndani ya jeshi la polisi. IOPC inafanya uchunguzi huru, bila kuingiliwa na maafisa wa polisi au wanasiasa, na inatoa ripoti kwa umma juu ya matokeo ya uchunguzi wake. Faida za tume hii ni pamoja na kuimarisha imani ya umma kwa polisi, kuboresha uwazi na uwajibikaji, na kuhakikisha kuwa vitendo vya ukiukwaji wa sheria vinashughulikiwa ipasavyo.
iii. Kuboresha mafunzo zaidi kwa polisi na mafunzo yawe endelevu.
Mafunzo ya polisi yanaweza kuboreshwa kwa kuzingatia mbinu za kisasa na kuimarisha mitaala inayolenga maadili, haki za binadamu, na matumizi sahihi ya nguvu. Hii inajumuisha kuingiza masomo ya sheria, mawasiliano bora, na mbinu za utatuzi wa migogoro kwa njia za amani. Mafunzo ya mara kwa mara ya kujenga uwezo katika teknolojia mpya za kiusalama na upelelezi pia ni muhimu. Aidha, ushirikiano na taasisi za kimataifa na za ndani kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na mbinu bora za polisi unaweza kusaidia sana. Pia, kujenga utamaduni wa uwajibikaji na uwazi ndani ya jeshi la polisi kwa kutoa mafunzo juu ya madhara ya rushwa na umuhimu wa uadilifu kutalifanya jeshi la polisi kuwa bora zaidi na lenye kuaminika na jamii.
iv. Kuongeza vifaa vya kazi vya kisasa.
Polisi wanahitaji magari, radio za mawasiliano, silaha na vifaa vya kujilinda, vifaa vya kufanyia upelelezi, vifaa vya uokozi, drones na boti za kufanyia doria baharini, vifaa vya kutambua vilipuzi, lakini kubwa zaidi ni sare ziliambatanishwa na kamera (police body camera) kwaajili ya kunasa kila tukio ambalo polisi analifanya wakati wa utendaji wa kazi zao.
v. Kuwaongezea mishahara
Askari pia ni binadamu, waongezewe mishahara wafanye kazi zao bila tamaa ya kuomba rushwa.
vi. Maboresho katika sheria
Ili marekebisho mengine yafanywe ni lazima kwanza yatambuliwe katika sheria, pili ule ukoloni tunaousema katika jeshi la polisi utapungua au kuondoka kabisa endapo tutaanza kubadili kanuni ngumu za kikoloni zilizowekwa kwa lengo la kumuumiza mtu mweusi na kutunga kanuni zingine nafuu kwa wananchi.
Maneno 1000 ni machache ningependa kuandika zaidi lakini kwa haya machache inatosha.
Upvote
1