Jeshi la Polisi: Ndoo sio choo, tusubirie utekelezaji wake

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Jeshi la Magereza kuchukua hatua zinazowezekana kwa kutumia rasiliamli zilizopo, kuondoa dhana ya kudhalilisha utu na kukiuka haki za binadamu kwa wafungwa.

View: https://youtu.be/u-0S0jmUsuQ?si=lWVDbgKVZmI5KlP6

Amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza unaofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo, Msalato mkoani Dodoma ambapo amesema ni muhimu kupunguza na hata kuondokana kabisa na matumizi ya ndoo magerezani kama choo.

Labda kwa kuwa umezungumza wewe Mheshimiwa Mpango, Makamu wa Rais, basi Wizara husika na Jeshi la Polisi watakusikiliza. Tusubirie utekelezaji wake.
 
Ukiwaona na suti zao hauwezi kuamini kama wanakatazwa matumizi ya ndoo huko magerezani..
 
Bado kuna ujinga wa kunya kwenye choo?
 
Kwamba hawajawahi kufikiri jinsi ya kuziondoa kwenye magereza yao ,nchi hii ngumu sana
Ukiona hivyo ujue wamepigiwa sana simu mpaka jamaa kaona awaambie tu hadharani maana wao wanaona ni kitu cha kawaida ukiwaambia wasitumie wanakushangaa ni hatari pia kwa afya zao kuwasimamia watu wanatumia ndoo..
 
Ni hatari hata kwa afya zao hao walinzi, ila wao wanahisi wafungwa/mahabusu ndo wanakiona cha moto kumbe hata wao hawako salama.
 
Ukiwa lokap ya polisi choo ndio hapo hapo dining room.
IGP yupo, waziri yupo na wakuu wa wilaya wapo.
 
tz ni taifa la kihuni lenye tabia za ukima
Ukiona hivyo ujue wamepigiwa sana simu mpaka jamaa kaona awaambie tu hadharani maana wao wanaona ni kitu cha kawaida ukiwaambia wasitumie wanakushangaa ni hatari pia kwa afya zao kuwasimamia watu wanatumia ndoo..
z b
 
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Jeshi la Magereza kuchukua hatua zinazowezekana kwa kutumia rasiliamli zilizopo, kuondoa dhana ya kudhalilisha utu na kukiuka haki za binadamu kwa wafungwa.

View: https://youtu.be/u-0S0jmUsuQ?si=lWVDbgKVZmI5KlP6

Amesema hayo wakati akifungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza unaofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo, Msalato mkoani Dodoma ambapo amesema ni muhimu kupunguza na hata kuondokana kabisa na matumizi ya ndoo magerezani kama choo.

Labda kwa kuwa umezungumza wewe Mheshimiwa Mpango, Makamu wa Rais, basi Wizara husika na Jeshi la Polisi watakusikiliza. Tusubirie utekelezaji wake.

Yaani hawajawahi kujiongeza tangu enzi wameendelea na utaratibu huo. Hata vituo vipya navyo kwenye sero hakuna vyoo. Kwanini sero isiwe self kama zilivyo sero za mahakamani?
 
Back
Top Bottom