Jeshi la Polisi Pwani kuanzia Septemba hadi Novemba limekamata watuhumiwa 203 wa makosa mbalimbali

Jeshi la Polisi Pwani kuanzia Septemba hadi Novemba limekamata watuhumiwa 203 wa makosa mbalimbali

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Septemba hadi Novemba limeendelea na operesheni na Misako ya kuzuia na kutanzua uhalifu katika Wilaya zote. Katika Operesheni hizo limefanikiwa kukamatwa jumla ya watuhumiwa 203 wa makosa mbalimbali.

Katika operesheni na misako hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani lilikamata Magobole 13 yaliyokuwa yanamilikiwa kinyume cha sheria, Bastola 1 aina ya Luger M90 ikiwa na risasi 09, Bunduki aina ya Shortgun 1, Mitambo 3 ya kupikia pombe ya moshi, na Pombe ya Moshi lita 375.

Aidha, Lilikamata Madawa ya kulevya aina ya bhangi Viroba 21, debe 5 , Puli 557, kete 3998, Misokoto 193, Pakiti 43 za bhangi aina ya skanka vyote vikiwa na jumla ya kilogramu 328.5 na kuteketeza mashamba ya bhangi yenye ukubwa wa hekari 4, Mirungi bunda 187 zenye jumla ya kilogramu 187. Pia lilikamatwa gari aina ya Scania lenye namba za usajili T. 625 CBD na trela lenye namba T.467 lililobeba shehena ya nondo mali idhaniwayo kuwa ni ya wizi.

Katika operesheni hizo Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuokoa mali mbalimbali
kama ifuatavyo:-
1. Pikipiki 37 za aina tofauti
2. Simu za mkononi 93 za aina mbalimbali
3. Laptop 1 na CPU 1
4. Bomba 28 za umeme
photo_2025-12-06_21-25-20.jpg
photo_2025-12-06_21-26-00.jpg
 
Kuna picha lengine polisi wa mwanza wanakuja na magodoro wakisema October 29 walikama watu
 
Nchi yetu sijui tumerogwa tunaona sifa kukamatana na kusumbuana kwa vitu ambavyo havipo..
 
Back
Top Bottom