Jeshi la Polisi rudisheni heshima yenu, msitumike kisiasa

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
18,653
Reaction score
31,010
1782971212632.png

Hivi majuzi tumemsikia IGP Mstaafu Omari Mahita akitamka waziwazi , tena bila kumung'unya maneno , akisema katika nafasi yake ya Mkuu wa Polisi, yeye alikataa kutumika kwa mambo dhahiri ya kisiasa.

Huo ni msimamo unaoeleweka, msimamo wa kufuata sheria zinazoongoza jeshi la polisi katika kutekeleza majukumu yake.

Msimamo huo umedorora kwa viongozi wa polisi katika miaka ya karibuni.

Kutumika polisi kudhibiti siasa za nchini sasa hivi kumeliweka jeshi la polisi kuwa mmoja wa wadau wa chama tawala, picha ambayo inalichafua jeshi.

Najua kuna mada humu JF inayoelezea vizuri swala hili, lakini tena Msemaji wa Polisi, hapo majuzi ameongea kuwa mambo ya kisiasa yatatuliwe kwa maongezi, na si kwa mawe na virungu na risasi.

Wanasiasa mlio madarakani mkumbuke kuwa hawa vijana na hata maofisa wa polisi wanaishi na jamii, na kazi ikiisha watarudi kwa jamii.
Mnawawekea mazingira magumu kimaisha.
Liwekeni hilo katika malengo yenu kisiasa.
 
Ni hadi pale ccm itakapotoka madarakani. Kinyume na hapo, sahau.
 
Ipo siku kamanda murilo atakuja kuwashangaa police kwani wanatumikishwa na wanasiasa au ccm ila adi atakapokua kikongwe
 
Leo Mahita anasema alichosema maana yupo pamoja na wananchi maskani kwake, na analiona jeshi lake la polisi kwa jicho tofauti.
 
View attachment 3620320
Hivi majuzi tumemsikia IGP Mstaafu Omari Mahita akitamka waziwazi , tena bila kumung'unya maneno , akisema katika nafasi yake ya Mkuu wa Polisi, yeye alikataa kutumika kwa mambo dhahiri ya kisiasa.

Huo ni msimamo unaoeleweka, msimamo wa kufuata sheria zinazoongoza jeshi la polisi katika kutekeleza majukumu yake.

Msimamo huo umedorora kwa viongozi wa polisi katika miaka ya karibuni.

Kutumika polisi kudhibiti siasa za nchini sasa hivi kumeliweka jeshi la polisi kuwa mmoja wa wadau wa chama tawala, picha ambayo inalichafua jeshi.

Najua kuna mada humu JF inayoelezea vizuri swala hili, lakini tena Msemaji wa Polisi, hapo majuzi ameongea kuwa mambo ya kisiasa yatatuliwe kwa maongezi, na si kwa mawe na virung,

Wanasiasa mlio madarakani mkumbuke kuwa hawa vijana na hata maofisa wa polisi wanaishi na jamii, na kazi ikiisha watarudi kwa jamii.
Mnawawekea mazingira magumu kimaisha.
Liwekeni hilo katika malengo yenu kisiasa.
Polisi ni miungoni mwa jumuiya za CCM
 
Back
Top Bottom