Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kupitia kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Camillus Wambura, limemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia magari mapya manne aina ya Toyota Hilux Double Cabin yatakayotumika kuimarisha ulinzi na usalama mkoani humo.
Magari hayo yamepokelewa Septemba 12, 2025 na Kamanda wa Polisi Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Amon D. Kakwale ambaye ameyakabidhi kwa Wakuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya ya Ikungi, Manyoni, Iramba na Mkalama ili kuboresha utendaji kazi wao kwa kuwahudumia wananchi kwa haraka.
Aidha, Kamanda Kakwale amewahimiza madereva wa magari hayo kuyatunza na kuyatumia ipasavyo kama ilivyoelekezwa kwenye taratibu za usimamizi wa magari ya Serikali.