Jeshi la Polisi (Trafiki) lianze na vitu hivi ili kudhibiti ajali

Jeshi la Polisi (Trafiki) lianze na vitu hivi ili kudhibiti ajali

HUNA HOJA Sababu kubwa ya Ajali ni Mwendo kasi
Ubovu wa Magari
Barabara mbaya
Kutokujua Sheria
Kutokuwa na Leseni na ADHABU kuwa Ndogo
Adhabu haijawahi kufuta uhalifu duniani, wewe ni mkosoaji mzuri ila ni mzito wa kuelewa kinachoongelewa.
 
Chanzo Cha Ajali ni kauli iliyotolewa Tunduma na Mzee Kinana ya Jeshi la polisi kupunguza Vituo vya ukaguzi barabarani. Ni matokeo ya ku politicize professions za watu.
Soma vizuri nilichokiongelea kisha urudi hapa.
 
Kimsingi barabara zote zinapaswa kuwa na taa mara Giza linapoingia.

Kutembea barabarani nyakati za usiku kwa kutegemea taa za gari pekee ni mambo ya kienyeji sana.

Ni Sawa mtu kuwa na macho lakini ikifika usiku anahitaji mwanga wa taa ili aone vizuri
Wewe nawe! Mmuliko wa taa za mitaani ni tofauti na wa za gari, umenikumbusha miaka ya sabini mwanzoni kuna mheshimiwa mmoja alimgonga mtu na gari lake wakati wa usiku na kusababisha kifo, kwenye utetezi wake alisingizia taa za barabani kutokuwa na mwanga wa kutosha, alileta kicheko mahakamani kama cha Kingai, kwahiyo Korogwe na Pandambili kulikuwa na giza ndiyo sababu!
 
Magari ya kisasa yana taa zinaumiza macho kama ujakalili mistari inakula kwako
Taa zinaumiza macho kwa sababu madereza wanapenda kumulikana na hii inatokea kwa sababu vyuo havifundishi matumizi mazuri ya taa, wao hufundisha jinsi ya kuwasha indiketa tu. Wakati wa usiku hapa mjini utaona madereva wanawasha mwanga mkubwa(fulllight) na mwanga mkubwa haukuwezeshi kuona mashimo yaliyo mbele yako.
 
Haya ndiyo mambo muhimu sana kwenye kudhibiti ajali za barabarani;

~ Iwekwe sheria ambayo itahakikisha kabla ya anayetaka leseni ya udereva pamoja na mafunzo anapimwa macho na dakitari wa polisi au wa hosipitali ya serikali, madereva wengi wana tatizo la mtoto wa jicho ambalo husababisha uono hafifu wakati wa usiku hasa macho yanapoangalia mwanga wa taa, tatizo hili ndilo chanzo cha magari kugongana yanapopishana.

~ Trafiki wapige marufuku matumizi ya diski za breki zinazochongwa mitaani na kubandikwa kwa gundi za viatu, hawa ajali ikitokea husingizia breki ilifeli kumbe gundi iliyeyuka na kusababisha breki isifanye kazi.

~ Mwisho matairi ya kuchongwa, matairi haya kwa hapo Dar yanachongwa karibu na kituo cha polisi Chang'ombe Temeke. Matairi haya huchongwa kurudishia mifereji (kashata) iliyokwisha, uchongaji huu husababisha tairi kulainika na gari kuyumba litembeapo pia kushindwa kusimama haraka breki ifungwapo.

Ninaamini endapo mambo haya niliyoyataja yatatekelezwa yataweza kusaidia sana kupunguza ajali kwani madereva wengi wanaona vizuri nyakati za mchana lakini wanauono hafifu sana usiku.

Sijui uhakiki wa leseni ni nini, leseni husika hupitia mikononi mwa trafiki na mtoaji ni TRA, sasa wanahakiki nini! Labda watueleze kama zipo leseni zinazotengenezwa mitaani.

Kuhusu vyuo, vingi havina walimu, mabasi na malori ya kufundishia madereva, wengi wao huanzia udeiwaka kwenye daladala kisha kwenye mabasi na utawakuta kwenye malori.
Uzi mzuri sana.Hayo hasa ya macho ni madereva wengi wana matatizo ya uoni hafifu,wapo wanaojitambua,ikiingia giza la jioni,wanakataa kuendesha gari.
 
Mbona kama mnaamisha goli kwa makusudi kila ajali inapotokea mnarudia maneno yaleyale na soln zenu zile zile, kwa nini hamtaki kwanza kujua nini hasa chanzo cha ajari. Sababu kubwa ya ajari nchini ni miundo mbinu ya barabara, barabara bado ni nyembamba na si salama tena kutokana na matumizi kuongezeka kila kukicha. Tatizo mnakwepesha kwenye chanzo kwa makusudi ili kutaka kuonyesha serikali haikosei na haijakosea.

Madereva wa nchi tena wanastahili pongezi kwa kusafirisha mamilioni ya watu na mizigo kwenye barabara za hatari namna hii, hiyo panda mbili kwa mfano ndio mahali ambapo marehemu Chacha wangwe ndio alipata ajari lakini hatua bado hazijachukuliwa na bado mnasingizia madereva. Hapa kabla ya kuongeza sheria barabara itanuliwe hasa yale maeneo hatarishi. Watunga sera na wafanya maamuzi wajifunze kutoka nchi nyingine kuliko kuachia kila alieshiba kande aje na suluhu kwa vitu vinavyoonekana dhahiri shairi.
haya magari nchi nyingine huko yanajiendesha, waotengeneza barabara wakati mwingine waone umuhimu wa kupunguza kona kona.
Mawasiliano kwa maana ya alama za barabarani hasa usiku ndio za kuongeza zaidi, kama serikali kweli mnayo akili anzeni kupunguza rushwa kwa askari wenu manake mpaka akili, utu na weledi hawana tena.

Kauli za mafunzo kwa madereva hatutaki tena kusikia mtu anaendesha basi miaka na miaka mnataka aje na cheti gani.
Nilichokiandika mimi hakijawahi kuzungumziwa na polisi, wao hujikita kwenye leseni wazitoazo wao na TRA uwezo wao wa kufikiri umeishia hapo.
 
Uzi mzuri sana.Hayo hasa ya macho ni madereva wengi wana matatizo ya uoni hafifu,wapo wanaojitambua,ikiingia giza la jioni,wanakataa kuendesha gari.
Uko sahihi, dereva anayejitambua huendesha gari kwa kujihami sana, huwezi ona anafuata nyuma ya gari futi mbili mlimani kama Kitonga, lakini kaangalie madereva wetu wanachofanya milimani, moja akifeli ni balaa. Dereva hajalala muda wa kutosha na anajua ana safari ndefu, bado kakomaa na gari. Mtu anatumia busta(red bull) na anajua kuna saa mwili utakataa tu. Njaa nayo ni hatari, mtu analazimisha awe na trip nyingi za safari kana kwamba mwili wake hauhitaji mapumziko.
Kuna watu wanajidunga, utaona maji ya Kilimanjaro pale kwenye dash bodi ya gari kumbe ndani kuna pombe kali na lile joto la pale kwenye kiti ni balaa lingine.Umalaya pia ni chanzo kilicho jificha kwa madereva wetu. Mungu anatupenda sana, basi upuuzi wetu.
 
Huwa wanasingizia kufeli, gari zinazotumia vipuri halisi huwa hazina hadithi za kufeli, ukitumia spea iliyochongwa gerezani lazima gari italeta hadithi ya kufeli.
 
Haya ndiyo mambo muhimu sana kwenye kudhibiti ajali za barabarani;

~ Iwekwe sheria ambayo itahakikisha kabla ya anayetaka leseni ya udereva pamoja na mafunzo anapimwa macho na dakitari wa polisi au wa hosipitali ya serikali, madereva wengi wana tatizo la mtoto wa jicho ambalo husababisha uono hafifu wakati wa usiku hasa macho yanapoangalia mwanga wa taa, tatizo hili ndilo chanzo cha magari kugongana yanapopishana.

~ Trafiki wapige marufuku matumizi ya diski za breki zinazochongwa mitaani na kubandikwa kwa gundi za viatu, hawa ajali ikitokea husingizia breki ilifeli kumbe gundi iliyeyuka na kusababisha breki isifanye kazi.

~ Mwisho matairi ya kuchongwa, matairi haya kwa hapo Dar yanachongwa karibu na kituo cha polisi Chang'ombe Temeke. Matairi haya huchongwa kurudishia mifereji (kashata) iliyokwisha, uchongaji huu husababisha tairi kulainika na gari kuyumba litembeapo pia kushindwa kusimama haraka breki ifungwapo.

Ninaamini endapo mambo haya niliyoyataja yatatekelezwa yataweza kusaidia sana kupunguza ajali kwani madereva wengi wanaona vizuri nyakati za mchana lakini wanauono hafifu sana usiku.

Sijui uhakiki wa leseni ni nini, leseni husika hupitia mikononi mwa trafiki na mtoaji ni TRA, sasa wanahakiki nini! Labda watueleze kama zipo leseni zinazotengenezwa mitaani.

Kuhusu vyuo, vingi havina walimu, mabasi na malori ya kufundishia madereva, wengi wao huanzia udeiwaka kwenye daladala kisha kwenye mabasi na utawakuta kwenye malori.
1681152248741.png
 
Back
Top Bottom