Jeshi la Polisi (Trafiki) lianze na vitu hivi ili kudhibiti ajali

HUNA HOJA Sababu kubwa ya Ajali ni Mwendo kasi
Ubovu wa Magari
Barabara mbaya
Kutokujua Sheria
Kutokuwa na Leseni na ADHABU kuwa Ndogo
Adhabu haijawahi kufuta uhalifu duniani, wewe ni mkosoaji mzuri ila ni mzito wa kuelewa kinachoongelewa.
 
Chanzo Cha Ajali ni kauli iliyotolewa Tunduma na Mzee Kinana ya Jeshi la polisi kupunguza Vituo vya ukaguzi barabarani. Ni matokeo ya ku politicize professions za watu.
Soma vizuri nilichokiongelea kisha urudi hapa.
 
Wewe nawe! Mmuliko wa taa za mitaani ni tofauti na wa za gari, umenikumbusha miaka ya sabini mwanzoni kuna mheshimiwa mmoja alimgonga mtu na gari lake wakati wa usiku na kusababisha kifo, kwenye utetezi wake alisingizia taa za barabani kutokuwa na mwanga wa kutosha, alileta kicheko mahakamani kama cha Kingai, kwahiyo Korogwe na Pandambili kulikuwa na giza ndiyo sababu!
 
Magari ya kisasa yana taa zinaumiza macho kama ujakalili mistari inakula kwako
Taa zinaumiza macho kwa sababu madereza wanapenda kumulikana na hii inatokea kwa sababu vyuo havifundishi matumizi mazuri ya taa, wao hufundisha jinsi ya kuwasha indiketa tu. Wakati wa usiku hapa mjini utaona madereva wanawasha mwanga mkubwa(fulllight) na mwanga mkubwa haukuwezeshi kuona mashimo yaliyo mbele yako.
 
Uzi mzuri sana.Hayo hasa ya macho ni madereva wengi wana matatizo ya uoni hafifu,wapo wanaojitambua,ikiingia giza la jioni,wanakataa kuendesha gari.
 
Nilichokiandika mimi hakijawahi kuzungumziwa na polisi, wao hujikita kwenye leseni wazitoazo wao na TRA uwezo wao wa kufikiri umeishia hapo.
 
Uzi mzuri sana.Hayo hasa ya macho ni madereva wengi wana matatizo ya uoni hafifu,wapo wanaojitambua,ikiingia giza la jioni,wanakataa kuendesha gari.
Uko sahihi, dereva anayejitambua huendesha gari kwa kujihami sana, huwezi ona anafuata nyuma ya gari futi mbili mlimani kama Kitonga, lakini kaangalie madereva wetu wanachofanya milimani, moja akifeli ni balaa. Dereva hajalala muda wa kutosha na anajua ana safari ndefu, bado kakomaa na gari. Mtu anatumia busta(red bull) na anajua kuna saa mwili utakataa tu. Njaa nayo ni hatari, mtu analazimisha awe na trip nyingi za safari kana kwamba mwili wake hauhitaji mapumziko.
Kuna watu wanajidunga, utaona maji ya Kilimanjaro pale kwenye dash bodi ya gari kumbe ndani kuna pombe kali na lile joto la pale kwenye kiti ni balaa lingine.Umalaya pia ni chanzo kilicho jificha kwa madereva wetu. Mungu anatupenda sana, basi upuuzi wetu.
 
Huwa wanasingizia kufeli, gari zinazotumia vipuri halisi huwa hazina hadithi za kufeli, ukitumia spea iliyochongwa gerezani lazima gari italeta hadithi ya kufeli.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…