Pre GE2025 Jeshi la Polisi: Tumemkamata Dkt. Slaa, tunamhoji na kuangalia mifumo ya Sheria inatuelekeza nini cha kufanya

Pre GE2025 Jeshi la Polisi: Tumemkamata Dkt. Slaa, tunamhoji na kuangalia mifumo ya Sheria inatuelekeza nini cha kufanya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Saa chache baada ya kutolewa taarifa ya kukamatwa kwa mwanasiasa mkongwe, Dk Willibrod Slaa, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia kwa mahojiano.

Taarifa ya kukamatwa kwa Dk Slaa imesambaa kupitia mitandao ya kijamii, ikisikika sauti ya mwanasiasa huyo akizungumza kuhusu kukamatwa na Jeshi la Polisi akieleza anapelekwa kituo cha Mbweni, Dar es Salaam.

“Nawajulisha tu kwamba kuna polisi wamenifuata, nitawajulisha kitakachotokea. Napelekwa Mbweni kituoni,” alisikika Dk Slaa katika sauti inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Zaidi soma Dkt. Slaa akamatwa usiku huu nyumbani kwake Mbweni

Alipozungumza na Kituo cha Redio cha Wasafi FM leo Januari 10, 2025 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amethibitisha kukamatwa na kushikiliwa Dk Slaa kwa mahojiano.

“Ni sahihi daktari yupo, tuko naye na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na mahojiano yetu yanakwenda vizuri kwa hiyo tunaangalia mifumo ya kisheria inatuelekeza nini cha kufanya naamini taarifa zaidi zitatolewa baadaye,” amesema.

Pia soma - Balozi Dkt. Wilbroad Slaa afichua siri mpya ya mikakati ya Mbowe kushinda uenyekiti. Apewa mapesa zaidi na Rais Samia na M/kiti CCM kummaliza Lissu..
 
Nchi ina sanaa nyingi sana kwa mazingira haya hata mkiweka dira ya maendeleo ya miaka 1000 mbele mtaendelea kuwa hivi hivi hakuna kitu cha maendeleo mnakipa kipaumbele kwenu zaidi ya mambo ya kijinga jinga tu yaliyowadumaza Ubongo..
Mzee Slaa ni mnafiki sana. Huu ni umri wa yeye kucheza na wajukuu. Siasa za Tanzania siyo SIZE yake
 
Nchi ina sanaa nyingi sana kwa mazingira haya hata mkiweka dira ya maendeleo ya miaka 1000 mbele mtaendelea kuwa hivi hivi hakuna kitu cha maendeleo mnakipa kipaumbele kwenu zaidi ya mambo ya kijinga jinga tu yaliyowadumaza Ubongo..
Ndio maana wananchi wanapigwa za uso na kina mwamposa wakisubia miujiza huku wao wakipalilia vitambi tu
 
Kumbe mmemkamata kabla ya kujua Sheria inawelekezaje? Hapo bila shaka mnamtafutia jinai kwa nguvu ili kosa lionekane. Kweli hakuna aliyesalama. Jiwe alianza hivyo hivyo. (Mkamate mtafutie jinai) Matokeo yake halkutoboa. Na nyie mjue uchaguzi hauko mbali. Mnaweza kutoboa na siku chache baadae yakatokea ya kutokea. (Hatuombi hivyo)
 
Kiusalama ni lazima ahojiwe. Mbaya zaidi alisemea Clubhouse ambamo watu wa usalama wa taifa lazima wamo. Na wanaweza kukurekodi kirahisi tu. Amejitakia mwenyewe
 
Nje ya mada...
Hivi kwanini utawala wa awamu hii hawamuiti Dr Slaa kwa kuanza na neno Balozi??
 
Back
Top Bottom