Pre GE2025 Jeshi la Polisi: Tumemkamata Dkt. Slaa, tunamhoji na kuangalia mifumo ya Sheria inatuelekeza nini cha kufanya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Inawesekana wakati Tanganyika inapata Uhuru ilikuwa na maendeleo kuliko sasa!
Miaka nasoma ya 90 viwanda vya nguo vilikuwepo na bus zao wafanyakazi walikua wanapanda bure watu walikua walikua wanaoneka wana nuru na akili zipo kichwani sio sasa hivi ni ujinga ujinga tu ndio umewajaa yaani tuanze kusikiriza sijui mfanyakazi wao wamemkata usiku na kutoa maelekezo asubuhi..
 
Bwa shee tuonyeshe mshikamano wetu timu Lissu kukamwekee dhamana mwenzetu. Tupo katikati ya mpambano.
Dr Slaa ni Boss wa Freeman kama ulikuwa haujui 😂😂

20% vs 80%

Sidhani kama utaelewa hapo Machame 🐼
 
Aisee! amelamba Billion 12?
Tetesi toka Twitter zinasema mwamba kalambishwa asali ya 12B+ na Dr Slaa alilisemea hilo suala kwe Clubhouse ya Twitter anasema kapewa Taarifa na watu wa system.

Ila 12B sio pesa ya kitoto 🤣
 
Saa chache baada ya kutolewa taarifa ya kukamatwa kwa mwanasiasa mkongwe, Dk Willibrod Slaa, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia kwa mahojiano.

Taarifa ya kukamatwa kwa Dk Slaa imesambaa kupitia mitandao ya kijamii, ikisikika sauti ya mwanasiasa huyo akizungumza kuhusu kukamatwa na Jeshi la Polisi akieleza anapelekwa kituo cha Mbweni, Dar es Salaam.

“Nawajulisha tu kwamba kuna polisi wamenifuata, nitawajulisha kitakachotokea. Napelekwa Mbweni kituoni,” alisikika Dk Slaa katika sauti inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Zaidi soma Dkt. Slaa akamatwa usiku huu nyumbani kwake Mbweni

Alipozungumza na Kituo cha Redio cha Wasafi FM leo Januari 10, 2025 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amethibitisha kukamatwa na kushikiliwa Dk Slaa kwa mahojiano.

“Ni sahihi daktari yupo, tuko naye na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na mahojiano yetu yanakwenda vizuri kwa hiyo tunaangalia mifumo ya kisheria inatuelekeza nini cha kufanya naamini taarifa zaidi zitatolewa baadaye,” amesema.

Pia soma - Balozi Dkt. Wilbroad Slaa afichua siri mpya ya mikakati ya Mbowe kushinda uenyekiti. Apewa mapesa zaidi na Rais Samia na M/kiti CCM kummaliza Lissu..
Unamkamata ndio unaangalia vifungu vya sheria? Si ilitakiwa aambiwe kosa lake wakati ana kamatwa?

Amandla...
 
Hii heading inatia kinyaa..!! Kwamba mpaka anakamatwa hawajajua cha kufanya?
 
Kibabu roporopo hicho kifungeni tuu hata kwakosa lakuiba mke wamtu...
 
Nchi ina sanaa nyingi sana kwa mazingira haya hata mkiweka dira ya maendeleo ya miaka 1000 mbele mtaendelea kuwa hivi hivi hakuna kitu cha maendeleo mnakipa kipaumbele kwenu zaidi ya mambo ya kijinga jinga tu yaliyowadumaza Ubongo..
Nimeipenda hii expert
 
Back
Top Bottom