Jeshi la Uhamiaji wamenirudisha Nyumbani wakidai sipo Fiti. Nimepoteza dira ya maisha

Asante nashukuru sana kwa ushauri na faraja mkuu, hicho kitu ni kweli kipo unakuta mtu anaondoka asubuhi jion anaingia mwingine hadi tukawa tunajiuliza hizi replacement mbona zinafanyika fasta sana ni kama wakureplace wameshaandaliwa na wanakuwepo around kusubiri gap....
Na kusema kutafuta mwanasheria hapana ningekuwa na hiyo pesa ningeifanya tuu mtaji maisha mengine yaendelee, maana naamin Mungu hajanipangia huko kama angekuwa amenipangia niajiriwe huko asingeruhusu nikutane na hiyo changamoto hivyo sitakiwi kulazimisha.
Pole sna nimeumia mno kwa jinsi walivyo kufanyia umenikumbusha jinsi nilivyokata naangaika katk ofc zao posta kudhibitisha majibu ya dogo kuwa hajawai kutumia makitu yao ya uongo

Ila ungeenda kwa waziri masauni aisee
 
Nawasalim kwa jina la JMT, Naamin kila mmoja wetu ni mzima wa afya na kwa wenzetu ambao hawako sawa kiafya basi mwenyezi Mungu awafanyie wepesi. Amin

Wakuu maisha yana mitihani mingi sana wakati mwingine inakatisha tamaa na moyo unashindwa kuendelea, mimi ni mwanachama wa muda mrefu wa huu mtandao wetu pendwa wa JF ila kwa jina tofauti na hili nimeona nitumie hii akaunti mpya ili niwe huru kuomba ushauri na msaada wowote ule utakaoweza kunisaidia ili kutoka kwenye hii hali ninayoipitia.

Mimi mhitimu wa shahada ya kwanza fani ya maabara za kisayansi miaka 7 iliyopita, umri wangu ni miaka 30 sasa na pia ni mama wa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 6 ambaye namlea mwenyewe kwa kila kitu.

Baada ya kuhitimu masomo nilifanikiwa kupata kazi ya mkataba katika shirika mojawapo la kimataifa na kupangiwa mkoa mmojawapo uliopo nyanda za juu kusini kwa miaka 3.

Baada ya mkataba kuisha nilirejea nyumbani jijin Dar na kufanya kazi kwa kujitolea katika taasis ya utafiti yenye tawi lake hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa mwaka mmoja na baadae nikaitwa tena kwenye mradi mwingine wa utafiti mkoa ule ule niliokuwepo kikazi mara ya kwanza kwa mkataba wa miaka 2, bahati mbaya sana baada ya miezi 3 tangu nianze kazi kukatokea changamoto ule mradi ukasitishwa na serikali na wale wafadhili wakaamishia mradi nchi jirani ya Zambia hivyo nikawa sina kazi.

Wakati hayo yanatokea mtoto wangu nilikuwa nimeshamuanzisha shule, kwa sababu ule mkoa tayari nilishauzoea nikaona nijiajiri kwenye biashara ya nafaka na mafuta ya kupikia japo kwa shida shida kwa sababu sikua nimejipanga kimtaji wakati nikiendelea kutafuta kazi, namshukuru Mungu biashara ikawa inaenda vizuri inanisaidia kukidhi mahitaji ya msingi ya kila siku.

Sasa mwaka jana 2022 nikawa nimepata changamoto kidogo nilinunua magunia ya alizeti mwezi wa 6 na kuyatunza nikitegemea nikamue mwezi wa 11/12 na kuuza mafuta wakati bei zinakuwa zimechangamka kidogo lakin badala yake ikawa kinyume bei ya mafuta iliporomoka zaidi nikalazimika kuuza kwa hasara kwa sababu ya uhitaji wa fedha niliokuwa nao.

Hivyo kiasi kidogo cha pesa kilichopatikana nilikitumia kuongeza nguvu dukani, kulipa bili nyinginezo kama kodi ya nyumba ninapoishi, kodi ya fremu na ada ya mtoto shuleni.

Wakati nikiwa kwenye mawazo ya hasara na kuporomoka kwa mtaji kinyume na matarajio, zikatoka nafasi za kazi za jeshi la polisi na Uhamiaji,nikaenda kufanya vipimo hospitali ya serikali ya mkoa kama ilivyotakiwa kwenye vigezo vya muombaji nashukuru nikakuta nipo sawa nikaomba zote na bahati nzuri nikaitwa kwenye saili zote, hivyo ikanibidi nichote tena kiasi cha pesa dukani ili niweze kufika kwenye usaili.

Nashukuru baada ya mchakato mrefu nikafanikiwa kuitwa kwenye kozi chuo cha Uhamiaji Tanga, kwa kweli nilifurahi sana. Hivyo ndani ya muda mchache wa maandalizi tuliokuwa tumepewa nililazimika kuuza duka na vyombo vyote vya ndani nilivyokuwa navyo japo kwa hasara, nikamuhamishia mtoto nyumban kwa wazazi wangu.

Pesa iliyopatikana kiasi nikamtumia mtu aliyenisaidia kupata nafasi kama shukrani, nyingine nikamlipia mtoto wangu ada ya shule ya mwaka mzima, nikanunua chakula cha kutosha angalau miezi miwili nyumbani na kiasi kilichobaki nikakitumia kwa ajili ya manunuzi ya mahitaji ya kule chuoni, nauli na akiba.

Basi siku ikafika nikaripoti chuoni, wiki ya kwanza ukaguzi wa vyeti na manunuzi ya vifaa vya kozi kama godoro, neti, tranka n.k ukafanyika, tukaendelea na mazoezi ya kawaida kuweka mwili sawa, mwanzoni mwa wiki ya pili zoezi la vipimo likafanyika na baada ya wiki moja majibu yakatoka bahati mbaya sana jina langu likawa moja kati ya majina ya watu walioonekana hawapo fiti kuendelea na kozi kwa mujibu wa vipimo vyao japo hatukupewa nafasi kujua tatizo ni nini kwa yeyote baina yetu.

Hivyo tukatakiwa kuchukua mizigo yetu na kuondoka eneo la chuo.
Katika siku nilizohisi kukata tamaa ya maisha na kutamani kufa ni ile siku natoka nje ya geti la chuo, kwa sababu kitu kikubwa kilichonijia kichwani kwa wakati ule ni kuwa naanzaje maisha upya tayari nilishauvuruga mtaji wangu nikitegemea tayari naenda kupata kazi ya kudumu, umri wangu umeenda, nina wadogo zangu watatu ambao bado wanasoma wazazi wanapambana ambao ninapokuwa vizuri nilikuwa nasapoti hapa na pale, nina mtoto wangu anayenitegemea kwa asilimia 100% baba yake tulishapotezana tangu nikiwa mjamzito.

Sasa na mimi naenda kuwa mzigo kwa wazazi nyumbani. Wakati ilibidi niwe msaada kwao, naumia sana.
Ndugu zangu ni wiki tatu sasa tangu hayo yatokee lakin bado moyo wangu una uchungu mno, wanasema muda unaponya mbona mimi hauniponyi?

Nahisi kukata tamaa nikiwaangalia marafiki zangu niliosoma nao wengi tayari wana maisha yao mazuri, natamani kuendeleza biashara zangu za nafaka, lakin sina pa kuanzia nilishavuruga mtaji, nikiangalia hali ya maisha hapa nyumbani ni ngumu basi nazidi kuchanganyikiwa nashinda tuu ndani sitamani kuonana na mtu yeyote.

Ndugu zangu wa JF naamin huku kuna watu wenye busara, uzoefu na nafasi mbalimbali za kunisaidia kwa namna yoyote ile, nahitaji ushauri wenu, msaada wa namna gani naweza kupata mtaji au hata connection ya kupata kazi itakayonisaidia kupata mtaji na kusimama tena akili yangu imeganda.

Nitashukuru sana na Mungu awabariki.
Penye ugumu ndo kwa kukomaa baraka ipo hapo
 
Uhamiaji Chini ya wizara ya mambo ya ndani mlichomfanyia huyu member wetu Aidama siyo Cha kiungwana kbsa.

iweje mtu haruusiwe kuanza kozi kbla hamjajiridhisha kuwa Yuko fit kiafya na utimamu kwa jumla kuliko Kuja kufanya test katikati ya mazoez ya kiendelea na kisha kuanza kuwa zingizia watu magonjwa ili wafukuzwe jeshini Kisha ninyi muweke watot wenu wasio kuwa na sifa Wala vigezo ??

Sakata lake limenikumbusha way back kipindi Cha nyuma jinsi mlivyo mzingizia ndugu yangu kuwa anatumia madawa ya kulevya Kisha mkamtoa ktktk ya mazoezi wakt dogo hajawai kutumia madawa ya kulevya wala kujuwa yako vip kimuonekano wake ila nyinyi mliweza kumsingizia dogo yule kuwa aliwai kutumia madawa na kupeleka kufukuzwa ktkt ya mazoezi ..hata sampuli zake tulipeleke south Africa kujiridhisha Kama dogo aliwai kutumia hayo makitu lkn majibu kote yalitoka kuwa hajawai Leo Tena mmerudia mambo Yale Yale binti wa watu anaenda kujinyonga kwa upuuz wenu

....

Leo Tena mmeibuka na hbr hzo hzo za kuwazingizia watu magonjwa ili muweke ndugu zenu ktk nafsi hzo Hilo Jambo ni baya ikiwa huyu dada /mwanamke huyu amesha uza biashara zake na kuwa tayari kufanya Kaz yenu na Kisha kutumikia JMT kwa mujibu wa Sheria leo hi ktk ya mozoezi mnamtimua bila kumpa kinacho msibu wakt mtu aliingia jeshi lenu akiwa na afya kamili na vipimo vilifanyika ktk hospital za serekali

Am [emoji817] Nina uhakika mnanzingizia huyu bint magonjwa tu Ile mishe yenu itimie kuweka watu wenu ninyi mliowapanga

Mam Samia naomba uliingilie Jambo hili alilofanyiwa mwanamke mwezako huyu nimechukizwa Sana kwa utapeli huu wa kiwango Cha lami
vitu ambavyo vinaweza fanya ukafukuzwa mafunzoni ni pamoja na

criminal records, unfit na utovu wa nidhamu nk hapa kwenye criminal records uhamiaaji hushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi kupata information za recruits na huchukua muda sana kupata reports ya mwisho ya uyo recruits .

NB: usahili wao hawa jamaa ni noma pdf karibia nzima walijaza watu wa imani moja na ukanda fulani, nafasi hii nikaikosa. kama wameanza kufukuzana wao kwa wao ni jambo jema.
 
1. Tafuta vibarua tu sehemu yoyote ile hata vya matofali au zege.

2. Sali sana lakini

Ilaa ulikosea sana kuwa singo maza kwa miaka 6 huyo mtoto kakupukunyua sana anyway huwezi kurudi nyuma

N. B USIJIUZE NASIKIA BIASHARA YA MALAYA IMEKUWA NGUMU, WALA USIJIUE MAANA HUJUI UENDAKO BAADA YA HAPO

MTUMAINIE MUNGU 😢😢
Acha kejeli kwani pana mtu anapenda kuwa single mother.
Zipo sababu zingine ni nje ya uwezo wa Mwanadamu
 
Nahisi kukata tamaa nikiwaangalia marafiki zangu niliosoma nao wengi tayari wana maisha yao mazuri, natamani kuendeleza biashara zangu za nafaka, lakin sina pa kuanzia nilishavuruga mtaji, nikiangalia hali ya maisha hapa nyumbani ni ngumu basi nazidi kuchanganyikiwa nashinda tuu ndani sitamani kuonana na mtu yeyote
Pole sana mdogo wangu! Hapo kwenye kukata tamaa sasa na kushinda ndani tu! Hutaki kuonana na watu! Hii hali itakuongezea msongo wa mawazo jitahidi kuwa unabadilishana mawazo na watu, fanya chochote cha halali cha kukuingizia hata pesa kidogo tu wala uwe busy. Kama kwa wazazi ni kijijini na kuna mashamba nenda ukae huko kwa muda wakati unajipanga, fursa itakukuta ukiwa njiani! Jijini bila shughuli ya kufanya mwisho wa siku utachukua maamuzi ya hovyo bora uko kwa wazazi ambako huduma zingine ni bure!
 
Huu ndio ujinga wa majeshi yetu hii ipo Sana, mtu anaingia gharama anaambiwa anunue KILA kitu mtu anakopa apate nauli na pesa ya kununua mahitaji akifika chuo anaambiwa utumbo anarudi tena mtaani SAsa hivyo vitu atamuuzia nani, hizo gharama alizokopa atarejesha vipi. Kwann msiwapime watu waliofiti ndio muwaambie wanunue vitu. Tunapenda Sana kuumizana watanzania
 
Nawasalim kwa jina la JMT, Naamin kila mmoja wetu ni mzima wa afya na kwa wenzetu ambao hawako sawa kiafya basi mwenyezi Mungu awafanyie wepesi. Amin

Wakuu maisha yana mitihani mingi sana wakati mwingine inakatisha tamaa na moyo unashindwa kuendelea, mimi ni mwanachama wa muda mrefu wa huu mtandao wetu pendwa wa JF ila kwa jina tofauti na hili nimeona nitumie hii akaunti mpya ili niwe huru kuomba ushauri na msaada wowote ule utakaoweza kunisaidia ili kutoka kwenye hii hali ninayoipitia.

Mimi mhitimu wa shahada ya kwanza fani ya maabara za kisayansi miaka 7 iliyopita, umri wangu ni miaka 30 sasa na pia ni mama wa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 6 ambaye namlea mwenyewe kwa kila kitu.

Baada ya kuhitimu masomo nilifanikiwa kupata kazi ya mkataba katika shirika mojawapo la kimataifa na kupangiwa mkoa mmojawapo uliopo nyanda za juu kusini kwa miaka 3.

Baada ya mkataba kuisha nilirejea nyumbani jijin Dar na kufanya kazi kwa kujitolea katika taasis ya utafiti yenye tawi lake hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa mwaka mmoja na baadae nikaitwa tena kwenye mradi mwingine wa utafiti mkoa ule ule niliokuwepo kikazi mara ya kwanza kwa mkataba wa miaka 2, bahati mbaya sana baada ya miezi 3 tangu nianze kazi kukatokea changamoto ule mradi ukasitishwa na serikali na wale wafadhili wakaamishia mradi nchi jirani ya Zambia hivyo nikawa sina kazi.

Wakati hayo yanatokea mtoto wangu nilikuwa nimeshamuanzisha shule, kwa sababu ule mkoa tayari nilishauzoea nikaona nijiajiri kwenye biashara ya nafaka na mafuta ya kupikia japo kwa shida shida kwa sababu sikua nimejipanga kimtaji wakati nikiendelea kutafuta kazi, namshukuru Mungu biashara ikawa inaenda vizuri inanisaidia kukidhi mahitaji ya msingi ya kila siku.

Sasa mwaka jana 2022 nikawa nimepata changamoto kidogo nilinunua magunia ya alizeti mwezi wa 6 na kuyatunza nikitegemea nikamue mwezi wa 11/12 na kuuza mafuta wakati bei zinakuwa zimechangamka kidogo lakin badala yake ikawa kinyume bei ya mafuta iliporomoka zaidi nikalazimika kuuza kwa hasara kwa sababu ya uhitaji wa fedha niliokuwa nao.

Hivyo kiasi kidogo cha pesa kilichopatikana nilikitumia kuongeza nguvu dukani, kulipa bili nyinginezo kama kodi ya nyumba ninapoishi, kodi ya fremu na ada ya mtoto shuleni.

Wakati nikiwa kwenye mawazo ya hasara na kuporomoka kwa mtaji kinyume na matarajio, zikatoka nafasi za kazi za jeshi la polisi na Uhamiaji,nikaenda kufanya vipimo hospitali ya serikali ya mkoa kama ilivyotakiwa kwenye vigezo vya muombaji nashukuru nikakuta nipo sawa nikaomba zote na bahati nzuri nikaitwa kwenye saili zote, hivyo ikanibidi nichote tena kiasi cha pesa dukani ili niweze kufika kwenye usaili.

Nashukuru baada ya mchakato mrefu nikafanikiwa kuitwa kwenye kozi chuo cha Uhamiaji Tanga, kwa kweli nilifurahi sana. Hivyo ndani ya muda mchache wa maandalizi tuliokuwa tumepewa nililazimika kuuza duka na vyombo vyote vya ndani nilivyokuwa navyo japo kwa hasara, nikamuhamishia mtoto nyumban kwa wazazi wangu.

Pesa iliyopatikana kiasi nikamtumia mtu aliyenisaidia kupata nafasi kama shukrani, nyingine nikamlipia mtoto wangu ada ya shule ya mwaka mzima, nikanunua chakula cha kutosha angalau miezi miwili nyumbani na kiasi kilichobaki nikakitumia kwa ajili ya manunuzi ya mahitaji ya kule chuoni, nauli na akiba.

Basi siku ikafika nikaripoti chuoni, wiki ya kwanza ukaguzi wa vyeti na manunuzi ya vifaa vya kozi kama godoro, neti, tranka n.k ukafanyika, tukaendelea na mazoezi ya kawaida kuweka mwili sawa, mwanzoni mwa wiki ya pili zoezi la vipimo likafanyika na baada ya wiki moja majibu yakatoka bahati mbaya sana jina langu likawa moja kati ya majina ya watu walioonekana hawapo fiti kuendelea na kozi kwa mujibu wa vipimo vyao japo hatukupewa nafasi kujua tatizo ni nini kwa yeyote baina yetu.

Hivyo tukatakiwa kuchukua mizigo yetu na kuondoka eneo la chuo.
Katika siku nilizohisi kukata tamaa ya maisha na kutamani kufa ni ile siku natoka nje ya geti la chuo, kwa sababu kitu kikubwa kilichonijia kichwani kwa wakati ule ni kuwa naanzaje maisha upya tayari nilishauvuruga mtaji wangu nikitegemea tayari naenda kupata kazi ya kudumu, umri wangu umeenda, nina wadogo zangu watatu ambao bado wanasoma wazazi wanapambana ambao ninapokuwa vizuri nilikuwa nasapoti hapa na pale, nina mtoto wangu anayenitegemea kwa asilimia 100% baba yake tulishapotezana tangu nikiwa mjamzito.

Sasa na mimi naenda kuwa mzigo kwa wazazi nyumbani. Wakati ilibidi niwe msaada kwao, naumia sana.
Ndugu zangu ni wiki tatu sasa tangu hayo yatokee lakin bado moyo wangu una uchungu mno, wanasema muda unaponya mbona mimi hauniponyi?

Nahisi kukata tamaa nikiwaangalia marafiki zangu niliosoma nao wengi tayari wana maisha yao mazuri, natamani kuendeleza biashara zangu za nafaka, lakin sina pa kuanzia nilishavuruga mtaji, nikiangalia hali ya maisha hapa nyumbani ni ngumu basi nazidi kuchanganyikiwa nashinda tuu ndani sitamani kuonana na mtu yeyote.

Ndugu zangu wa JF naamin huku kuna watu wenye busara, uzoefu na nafasi mbalimbali za kunisaidia kwa namna yoyote ile, nahitaji ushauri wenu, msaada wa namna gani naweza kupata mtaji au hata connection ya kupata kazi itakayonisaidia kupata mtaji na kusimama tena akili yangu imeganda.

Nitashukuru sana na Mungu awabariki.
pole sana mkuu , kwa uharaka ungemcheki aliekusaidia kupata nafasi ange sovu hii ishu yako .mm pia ninezitegea sana hizo post lkn mambo yaka yumbishwa.

pili watafute watu uliofanya nao kazi kwenye kazi za awali watakupa abc ikiwezekana pia na connection ya kurudi mzigoni
 
Wamezingua sana. Nina ndugu yangu alishawahi kutolewa jeshini wakampa sababu mguu mmoja ni mfupi kuliko mwingine. Mwaka uliofata wakakataa na kumpa sababu kuwa miguu yake haina uvungu, hivyo hatoweza kupiga kwata au kusimama kwa muda mrefu.

Mwaka uliofatia tena, baada ya kuhonga alikubaliwa kujiunga na jeshi. Now anadunda tu. 😅😅😅😅
 
Uhamiaji Chini ya wizara ya mambo ya ndani mlichomfanyia huyu member wetu Aidama siyo Cha kiungwana kbsa.

iweje mtu haruusiwe kuanza kozi kbla hamjajiridhisha kuwa Yuko fit kiafya na utimamu kwa jumla kuliko Kuja kufanya test katikati ya mazoez ya kiendelea na kisha kuanza kuwa zingizia watu magonjwa ili wafukuzwe jeshini Kisha ninyi muweke watot wenu wasio kuwa na sifa Wala vigezo ??

Sakata lake limenikumbusha way back kipindi Cha nyuma jinsi mlivyo mzingizia ndugu yangu kuwa anatumia madawa ya kulevya Kisha mkamtoa ktktk ya mazoezi wakt dogo hajawai kutumia madawa ya kulevya wala kujuwa yako vip kimuonekano wake ila nyinyi mliweza kumsingizia dogo yule kuwa aliwai kutumia madawa na kupeleka kufukuzwa ktkt ya mazoezi ..hata sampuli zake tulipeleke south Africa kujiridhisha Kama dogo aliwai kutumia hayo makitu lkn majibu kote yalitoka kuwa hajawai Leo Tena mmerudia mambo Yale Yale binti wa watu anaenda kujinyonga kwa upuuz wenu

....

Leo Tena mmeibuka na hbr hzo hzo za kuwazingizia watu magonjwa ili muweke ndugu zenu ktk nafsi hzo Hilo Jambo ni baya ikiwa huyu dada /mwanamke huyu amesha uza biashara zake na kuwa tayari kufanya Kaz yenu na Kisha kutumikia JMT kwa mujibu wa Sheria leo hi ktk ya mozoezi mnamtimua bila kumpa kinacho msibu wakt mtu aliingia jeshi lenu akiwa na afya kamili na vipimo vilifanyika ktk hospital za serekali

Am [emoji817] Nina uhakika mnanzingizia huyu bint magonjwa tu Ile mishe yenu itimie kuweka watu wenu ninyi mliowapanga

Mam Samia naomba uliingilie Jambo hili alilofanyiwa mwanamke mwezako huyu nimechukizwa Sana kwa utapeli huu wa kiwango Cha lami
Inauma Sana kwa kweli umeanza coz katikati unaludishwa bila Sababu Ya Msingi, kwani Vipimo hamuwafanyii Kabla ya kuanza kozi Ujinga Tu.. [emoji706]
 
Pole Sana kwa yaliokutokea dada huu ujinga wa uhamiaji aliwai kufanyiwa rfk wangu wa karibu Sana sakata lako limefanana kila kitu

Kwanza jamaa aliishaanza koz kbsa kipindi hcho ccp Moshi Hadi kupiga mazoez ya kutumia silaha ,

Ktkt ya zoezi wakaja kuchukuwa Tena sample za wanafunzi ikaja ikabainika kuwa dogo yule alikuwa anatumia madaya ya kulevya hvyo yeye na wenzio watano hawatakiwi kuwepo ktk eneo Hilo ,

Katik hayo yote dogo hakuwai hata kuguza Wala kutumia dawa zozote iwe bangi hajawai na hata kuzitambua dawa za kulevya hajui maskini ila madakta wa vipimo wakasema kuwa Ni mtumuaji wa madawa ya kulevya

Bas dogo pmj na kak ake na Bab ake wakachukua sample Hadi hospital ya regency na sample zingine kutumwa South Africa na majibu yote yalitoka kuwa hajawai kutumia dawa hzo ,

Kurudi uhamijaji kurudisha majibu akambiwa koz inakaribia kuisha na hvyo aombe kipind kingine duh ...

Kuchunguza hiyo kitu kumbe Kuna mtu aliwekwa faster kwenye hyo nafsi yake kimafya Zaid without being noticed

Kufatilia Zaid Alichogundua kuwa yule mtu waliompa pesa kumsadia azame uhamiaji zile pesa hajazifikisha kwa wakubwa jamaa alizila zote bila kushare na wakubw wa juu Zaid na Kisha kutumia njia anaxojuwa yey kumpenyeza jamaa katk jeshi Hilo kwa taratibu anazo zijuwa yeye

NNI KIFANYIKE
Nenda kuomba kuonana na wazir wa mambo ya ndani bwana masauni au katibu mkuu wa wizara hyo Ni mwalimu wangu wa chuo nilichosoma mm Ila sijui Kama kabadilishwa ,fanya hvyo walilie wale watu wakupe msaada na waangalie namna ya kupata haki zako mnk hapo umefanyiwa uhuni wa kipuuz Sana ,ile nafsi yako wamepenyezwa watot wa wakubwa

Au Kama upo vzr mtafute mwanasheria makini kawashataki kwa kukuzingiza magonjwa na kukuaribia maisha yako

Note yule rfk angu mpk leo mwaka wa Saba unaenda hajawai pata Kaz yoyote ile ya maana yupo tu Ni mzazi wake ana mpa backup
doh
 
Back
Top Bottom