Jeshi la Uhamiaji wamenirudisha Nyumbani wakidai sipo Fiti. Nimepoteza dira ya maisha

Pole sna nimeumia mno kwa jinsi walivyo kufanyia umenikumbusha jinsi nilivyokata naangaika katk ofc zao posta kudhibitisha majibu ya dogo kuwa hajawai kutumia makitu yao ya uongo


Ila ungeenda kwa waziri masauni aisee
 
Penye ugumu ndo kwa kukomaa baraka ipo hapo
 
vitu ambavyo vinaweza fanya ukafukuzwa mafunzoni ni pamoja na

criminal records, unfit na utovu wa nidhamu nk hapa kwenye criminal records uhamiaaji hushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi kupata information za recruits na huchukua muda sana kupata reports ya mwisho ya uyo recruits .

NB: usahili wao hawa jamaa ni noma pdf karibia nzima walijaza watu wa imani moja na ukanda fulani, nafasi hii nikaikosa. kama wameanza kufukuzana wao kwa wao ni jambo jema.
 
Acha kejeli kwani pana mtu anapenda kuwa single mother.
Zipo sababu zingine ni nje ya uwezo wa Mwanadamu
 
Pole sana mdogo wangu! Hapo kwenye kukata tamaa sasa na kushinda ndani tu! Hutaki kuonana na watu! Hii hali itakuongezea msongo wa mawazo jitahidi kuwa unabadilishana mawazo na watu, fanya chochote cha halali cha kukuingizia hata pesa kidogo tu wala uwe busy. Kama kwa wazazi ni kijijini na kuna mashamba nenda ukae huko kwa muda wakati unajipanga, fursa itakukuta ukiwa njiani! Jijini bila shughuli ya kufanya mwisho wa siku utachukua maamuzi ya hovyo bora uko kwa wazazi ambako huduma zingine ni bure!
 
Huu ndio ujinga wa majeshi yetu hii ipo Sana, mtu anaingia gharama anaambiwa anunue KILA kitu mtu anakopa apate nauli na pesa ya kununua mahitaji akifika chuo anaambiwa utumbo anarudi tena mtaani SAsa hivyo vitu atamuuzia nani, hizo gharama alizokopa atarejesha vipi. Kwann msiwapime watu waliofiti ndio muwaambie wanunue vitu. Tunapenda Sana kuumizana watanzania
 
pole sana mkuu , kwa uharaka ungemcheki aliekusaidia kupata nafasi ange sovu hii ishu yako .mm pia ninezitegea sana hizo post lkn mambo yaka yumbishwa.

pili watafute watu uliofanya nao kazi kwenye kazi za awali watakupa abc ikiwezekana pia na connection ya kurudi mzigoni
 
Wamezingua sana. Nina ndugu yangu alishawahi kutolewa jeshini wakampa sababu mguu mmoja ni mfupi kuliko mwingine. Mwaka uliofata wakakataa na kumpa sababu kuwa miguu yake haina uvungu, hivyo hatoweza kupiga kwata au kusimama kwa muda mrefu.

Mwaka uliofatia tena, baada ya kuhonga alikubaliwa kujiunga na jeshi. Now anadunda tu. πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Inauma Sana kwa kweli umeanza coz katikati unaludishwa bila Sababu Ya Msingi, kwani Vipimo hamuwafanyii Kabla ya kuanza kozi Ujinga Tu.. [emoji706]
 
doh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…