Jeshi la Uhamiaji wamenirudisha Nyumbani wakidai sipo Fiti. Nimepoteza dira ya maisha

vitu ambavyo vinaweza fanya ukafukuzwa mafunzoni ni pamoja na

criminal records, unfit na utovu wa nidhamu nk hapa kwenye criminal records uhamiaaji hushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi kupata information za recruits na huchukua muda sana kupata reports ya mwisho ya uyo recruits .

NB: usahili wao hawa jamaa ni noma pdf karibia nzima walijaza watu wa imani moja na ukanda fulani, nafasi hii nikaikosa. kama wameanza kufukuzana wao kwa wao ni jambo jema.
Acheni kujitetea mnafanyaga punguzeni laanabasi
 
Utakiwi kufikiria yaliyopita yatakuumiza zaidi wala usiwaze kwenda KWA waganga utapotea zaidi Acha nature ifanye maamuzi. Ukiweza badili mazingira KWA mda pia ukajichanganye na chochote mtaani, huku ukiendelea kutuma cv sehemu na sehemu, pia ukiomba hata za kujitolea.
 
Nawasalim kwa jina la JMT, Naamin kila mmoja wetu ni mzima wa afya na kwa wenzetu ambao hawako sawa kiafya basi mwenyezi Mungu awafanyie wepesi. Amin

Wakuu maisha yana mitihani mingi sana wakati mwingine inakatisha tamaa na moyo unashindwa kuendelea, mimi ni mwanachama wa muda mrefu wa huu mtandao wetu pendwa wa JF ila kwa jina tofauti na hili nimeona nitumie hii akaunti mpya ili niwe huru kuomba ushauri na msaada wowote ule utakaoweza kunisaidia ili kutoka kwenye hii hali ninayoipitia.

Mimi mhitimu wa shahada ya kwanza fani ya maabara za kisayansi miaka 7 iliyopita, umri wangu ni miaka 30 sasa na pia ni mama wa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 6 ambaye namlea mwenyewe kwa kila kitu.

Baada ya kuhitimu masomo nilifanikiwa kupata kazi ya mkataba katika shirika mojawapo la kimataifa na kupangiwa mkoa mmojawapo uliopo nyanda za juu kusini kwa miaka 3.

Baada ya mkataba kuisha nilirejea nyumbani jijin Dar na kufanya kazi kwa kujitolea katika taasis ya utafiti yenye tawi lake hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa mwaka mmoja na baadae nikaitwa tena kwenye mradi mwingine wa utafiti mkoa ule ule niliokuwepo kikazi mara ya kwanza kwa mkataba wa miaka 2, bahati mbaya sana baada ya miezi 3 tangu nianze kazi kukatokea changamoto ule mradi ukasitishwa na serikali na wale wafadhili wakaamishia mradi nchi jirani ya Zambia hivyo nikawa sina kazi.

Wakati hayo yanatokea mtoto wangu nilikuwa nimeshamuanzisha shule, kwa sababu ule mkoa tayari nilishauzoea nikaona nijiajiri kwenye biashara ya nafaka na mafuta ya kupikia japo kwa shida shida kwa sababu sikua nimejipanga kimtaji wakati nikiendelea kutafuta kazi, namshukuru Mungu biashara ikawa inaenda vizuri inanisaidia kukidhi mahitaji ya msingi ya kila siku.

Sasa mwaka jana 2022 nikawa nimepata changamoto kidogo nilinunua magunia ya alizeti mwezi wa 6 na kuyatunza nikitegemea nikamue mwezi wa 11/12 na kuuza mafuta wakati bei zinakuwa zimechangamka kidogo lakin badala yake ikawa kinyume bei ya mafuta iliporomoka zaidi nikalazimika kuuza kwa hasara kwa sababu ya uhitaji wa fedha niliokuwa nao.

Hivyo kiasi kidogo cha pesa kilichopatikana nilikitumia kuongeza nguvu dukani, kulipa bili nyinginezo kama kodi ya nyumba ninapoishi, kodi ya fremu na ada ya mtoto shuleni.

Wakati nikiwa kwenye mawazo ya hasara na kuporomoka kwa mtaji kinyume na matarajio, zikatoka nafasi za kazi za jeshi la polisi na Uhamiaji,nikaenda kufanya vipimo hospitali ya serikali ya mkoa kama ilivyotakiwa kwenye vigezo vya muombaji nashukuru nikakuta nipo sawa nikaomba zote na bahati nzuri nikaitwa kwenye saili zote, hivyo ikanibidi nichote tena kiasi cha pesa dukani ili niweze kufika kwenye usaili.

Nashukuru baada ya mchakato mrefu nikafanikiwa kuitwa kwenye kozi chuo cha Uhamiaji Tanga, kwa kweli nilifurahi sana. Hivyo ndani ya muda mchache wa maandalizi tuliokuwa tumepewa nililazimika kuuza duka na vyombo vyote vya ndani nilivyokuwa navyo japo kwa hasara, nikamuhamishia mtoto nyumban kwa wazazi wangu.

Pesa iliyopatikana kiasi nikamtumia mtu aliyenisaidia kupata nafasi kama shukrani, nyingine nikamlipia mtoto wangu ada ya shule ya mwaka mzima, nikanunua chakula cha kutosha angalau miezi miwili nyumbani na kiasi kilichobaki nikakitumia kwa ajili ya manunuzi ya mahitaji ya kule chuoni, nauli na akiba.

Basi siku ikafika nikaripoti chuoni, wiki ya kwanza ukaguzi wa vyeti na manunuzi ya vifaa vya kozi kama godoro, neti, tranka n.k ukafanyika, tukaendelea na mazoezi ya kawaida kuweka mwili sawa, mwanzoni mwa wiki ya pili zoezi la vipimo likafanyika na baada ya wiki moja majibu yakatoka bahati mbaya sana jina langu likawa moja kati ya majina ya watu walioonekana hawapo fiti kuendelea na kozi kwa mujibu wa vipimo vyao japo hatukupewa nafasi kujua tatizo ni nini kwa yeyote baina yetu.

Hivyo tukatakiwa kuchukua mizigo yetu na kuondoka eneo la chuo.
Katika siku nilizohisi kukata tamaa ya maisha na kutamani kufa ni ile siku natoka nje ya geti la chuo, kwa sababu kitu kikubwa kilichonijia kichwani kwa wakati ule ni kuwa naanzaje maisha upya tayari nilishauvuruga mtaji wangu nikitegemea tayari naenda kupata kazi ya kudumu, umri wangu umeenda, nina wadogo zangu watatu ambao bado wanasoma wazazi wanapambana ambao ninapokuwa vizuri nilikuwa nasapoti hapa na pale, nina mtoto wangu anayenitegemea kwa asilimia 100% baba yake tulishapotezana tangu nikiwa mjamzito.

Sasa na mimi naenda kuwa mzigo kwa wazazi nyumbani. Wakati ilibidi niwe msaada kwao, naumia sana.
Ndugu zangu ni wiki tatu sasa tangu hayo yatokee lakin bado moyo wangu una uchungu mno, wanasema muda unaponya mbona mimi hauniponyi?

Nahisi kukata tamaa nikiwaangalia marafiki zangu niliosoma nao wengi tayari wana maisha yao mazuri, natamani kuendeleza biashara zangu za nafaka, lakin sina pa kuanzia nilishavuruga mtaji, nikiangalia hali ya maisha hapa nyumbani ni ngumu basi nazidi kuchanganyikiwa nashinda tuu ndani sitamani kuonana na mtu yeyote.

Ndugu zangu wa JF naamin huku kuna watu wenye busara, uzoefu na nafasi mbalimbali za kunisaidia kwa namna yoyote ile, nahitaji ushauri wenu, msaada wa namna gani naweza kupata mtaji au hata connection ya kupata kazi itakayonisaidia kupata mtaji na kusimama tena akili yangu imeganda.

Nitashukuru sana na Mungu awabariki.
Relax best kwanza
 
Pole sana,
Itakuwa umefanyiwa figisu na nafasi yako kupewa mtu mwenye pesa yake.
Any way Usikate tamaa inaonekana unajua kupambana na maisha hasa biashara.
Nakushauri anza tena kidogo kidogo.
Nyota yako iko kwenye biashara huko kwenye ajira sio kwako.
Be strong.
 
Pole Sana kwa yaliokutokea dada huu ujinga wa uhamiaji aliwai kufanyiwa rfk wangu wa karibu Sana sakata lako limefanana kila kitu

Kwanza jamaa aliishaanza koz kbsa kipindi hcho ccp Moshi Hadi kupiga mazoez ya kutumia silaha ,

Ktkt ya zoezi wakaja kuchukuwa Tena sample za wanafunzi ikaja ikabainika kuwa dogo yule alikuwa anatumia madaya ya kulevya hvyo yeye na wenzio watano hawatakiwi kuwepo ktk eneo Hilo ,

Katik hayo yote dogo hakuwai hata kuguza Wala kutumia dawa zozote iwe bangi hajawai na hata kuzitambua dawa za kulevya hajui maskini ila madakta wa vipimo wakasema kuwa Ni mtumuaji wa madawa ya kulevya

Bas dogo pmj na kak ake na Bab ake wakachukua sample Hadi hospital ya regency na sample zingine kutumwa South Africa na majibu yote yalitoka kuwa hajawai kutumia dawa hzo ,

Kurudi uhamijaji kurudisha majibu akambiwa koz inakaribia kuisha na hvyo aombe kipind kingine duh ...

Kuchunguza hiyo kitu kumbe Kuna mtu aliwekwa faster kwenye hyo nafsi yake kimafya Zaid without being noticed

Kufatilia Zaid Alichogundua kuwa yule mtu waliompa pesa kumsadia azame uhamiaji zile pesa hajazifikisha kwa wakubwa jamaa alizila zote bila kushare na wakubw wa juu Zaid na Kisha kutumia njia anaxojuwa yey kumpenyeza jamaa katk jeshi Hilo kwa taratibu anazo zijuwa yeye

NNI KIFANYIKE
Nenda kuomba kuonana na wazir wa mambo ya ndani bwana masauni au katibu mkuu wa wizara hyo Ni mwalimu wangu wa chuo nilichosoma mm Ila sijui Kama kabadilishwa ,fanya hvyo walilie wale watu wakupe msaada na waangalie namna ya kupata haki zako mnk hapo umefanyiwa uhuni wa kipuuz Sana ,ile nafsi yako wamepenyezwa watot wa wakubwa

Au Kama upo vzr mtafute mwanasheria makini kawashataki kwa kukuzingiza magonjwa na kukuaribia maisha yako

Note yule rfk angu mpk leo mwaka wa Saba unaenda hajawai pata Kaz yoyote ile ya maana yupo tu Ni mzazi wake ana mpa backup
Hivi hizi nafasi bila kuwa mtoto wa kigogo au bila kutoa kitu kidogo inaonekana ni ngumu sana kuzipata
 
Kila nikifikiria kwenye huu mkasa wa dada yetu Ñaumia sana.Samahani lakini maaana Mimi sipo Jeshini,je ulijifungua Kwa kawaida au Operation??...Ili tujue pengine ulikuwa na mshono..Maana Afya inaweza kuwa uko vizuri ila mara nyingi Mshono huwa hawataki...
 
Nawasalim kwa jina la JMT, Naamin kila mmoja wetu ni mzima wa afya na kwa wenzetu ambao hawako sawa kiafya basi mwenyezi Mungu awafanyie wepesi. Amin

Wakuu maisha yana mitihani mingi sana wakati mwingine inakatisha tamaa na moyo unashindwa kuendelea, mimi ni mwanachama wa muda mrefu wa huu mtandao wetu pendwa wa JF ila kwa jina tofauti na hili nimeona nitumie hii akaunti mpya ili niwe huru kuomba ushauri na msaada wowote ule utakaoweza kunisaidia ili kutoka kwenye hii hali ninayoipitia.

Mimi mhitimu wa shahada ya kwanza fani ya maabara za kisayansi miaka 7 iliyopita, umri wangu ni miaka 30 sasa na pia ni mama wa mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 6 ambaye namlea mwenyewe kwa kila kitu.

Baada ya kuhitimu masomo nilifanikiwa kupata kazi ya mkataba katika shirika mojawapo la kimataifa na kupangiwa mkoa mmojawapo uliopo nyanda za juu kusini kwa miaka 3.

Baada ya mkataba kuisha nilirejea nyumbani jijin Dar na kufanya kazi kwa kujitolea katika taasis ya utafiti yenye tawi lake hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa mwaka mmoja na baadae nikaitwa tena kwenye mradi mwingine wa utafiti mkoa ule ule niliokuwepo kikazi mara ya kwanza kwa mkataba wa miaka 2, bahati mbaya sana baada ya miezi 3 tangu nianze kazi kukatokea changamoto ule mradi ukasitishwa na serikali na wale wafadhili wakaamishia mradi nchi jirani ya Zambia hivyo nikawa sina kazi.

Wakati hayo yanatokea mtoto wangu nilikuwa nimeshamuanzisha shule, kwa sababu ule mkoa tayari nilishauzoea nikaona nijiajiri kwenye biashara ya nafaka na mafuta ya kupikia japo kwa shida shida kwa sababu sikua nimejipanga kimtaji wakati nikiendelea kutafuta kazi, namshukuru Mungu biashara ikawa inaenda vizuri inanisaidia kukidhi mahitaji ya msingi ya kila siku.

Sasa mwaka jana 2022 nikawa nimepata changamoto kidogo nilinunua magunia ya alizeti mwezi wa 6 na kuyatunza nikitegemea nikamue mwezi wa 11/12 na kuuza mafuta wakati bei zinakuwa zimechangamka kidogo lakin badala yake ikawa kinyume bei ya mafuta iliporomoka zaidi nikalazimika kuuza kwa hasara kwa sababu ya uhitaji wa fedha niliokuwa nao.

Hivyo kiasi kidogo cha pesa kilichopatikana nilikitumia kuongeza nguvu dukani, kulipa bili nyinginezo kama kodi ya nyumba ninapoishi, kodi ya fremu na ada ya mtoto shuleni.

Wakati nikiwa kwenye mawazo ya hasara na kuporomoka kwa mtaji kinyume na matarajio, zikatoka nafasi za kazi za jeshi la polisi na Uhamiaji,nikaenda kufanya vipimo hospitali ya serikali ya mkoa kama ilivyotakiwa kwenye vigezo vya muombaji nashukuru nikakuta nipo sawa nikaomba zote na bahati nzuri nikaitwa kwenye saili zote, hivyo ikanibidi nichote tena kiasi cha pesa dukani ili niweze kufika kwenye usaili.

Nashukuru baada ya mchakato mrefu nikafanikiwa kuitwa kwenye kozi chuo cha Uhamiaji Tanga, kwa kweli nilifurahi sana. Hivyo ndani ya muda mchache wa maandalizi tuliokuwa tumepewa nililazimika kuuza duka na vyombo vyote vya ndani nilivyokuwa navyo japo kwa hasara, nikamuhamishia mtoto nyumban kwa wazazi wangu.

Pesa iliyopatikana kiasi nikamtumia mtu aliyenisaidia kupata nafasi kama shukrani, nyingine nikamlipia mtoto wangu ada ya shule ya mwaka mzima, nikanunua chakula cha kutosha angalau miezi miwili nyumbani na kiasi kilichobaki nikakitumia kwa ajili ya manunuzi ya mahitaji ya kule chuoni, nauli na akiba.

Basi siku ikafika nikaripoti chuoni, wiki ya kwanza ukaguzi wa vyeti na manunuzi ya vifaa vya kozi kama godoro, neti, tranka n.k ukafanyika, tukaendelea na mazoezi ya kawaida kuweka mwili sawa, mwanzoni mwa wiki ya pili zoezi la vipimo likafanyika na baada ya wiki moja majibu yakatoka bahati mbaya sana jina langu likawa moja kati ya majina ya watu walioonekana hawapo fiti kuendelea na kozi kwa mujibu wa vipimo vyao japo hatukupewa nafasi kujua tatizo ni nini kwa yeyote baina yetu.

Hivyo tukatakiwa kuchukua mizigo yetu na kuondoka eneo la chuo.
Katika siku nilizohisi kukata tamaa ya maisha na kutamani kufa ni ile siku natoka nje ya geti la chuo, kwa sababu kitu kikubwa kilichonijia kichwani kwa wakati ule ni kuwa naanzaje maisha upya tayari nilishauvuruga mtaji wangu nikitegemea tayari naenda kupata kazi ya kudumu, umri wangu umeenda, nina wadogo zangu watatu ambao bado wanasoma wazazi wanapambana ambao ninapokuwa vizuri nilikuwa nasapoti hapa na pale, nina mtoto wangu anayenitegemea kwa asilimia 100% baba yake tulishapotezana tangu nikiwa mjamzito.

Sasa na mimi naenda kuwa mzigo kwa wazazi nyumbani. Wakati ilibidi niwe msaada kwao, naumia sana.
Ndugu zangu ni wiki tatu sasa tangu hayo yatokee lakin bado moyo wangu una uchungu mno, wanasema muda unaponya mbona mimi hauniponyi?

Nahisi kukata tamaa nikiwaangalia marafiki zangu niliosoma nao wengi tayari wana maisha yao mazuri, natamani kuendeleza biashara zangu za nafaka, lakin sina pa kuanzia nilishavuruga mtaji, nikiangalia hali ya maisha hapa nyumbani ni ngumu basi nazidi kuchanganyikiwa nashinda tuu ndani sitamani kuonana na mtu yeyote.

Ndugu zangu wa JF naamin huku kuna watu wenye busara, uzoefu na nafasi mbalimbali za kunisaidia kwa namna yoyote ile, nahitaji ushauri wenu, msaada wa namna gani naweza kupata mtaji au hata connection ya kupata kazi itakayonisaidia kupata mtaji na kusimama tena akili yangu imeganda.

Nitashukuru sana na Mungu awabariki.
huko nyanda za juu kusini ngo nyingi zilifutwa na bado zitaendelea kufutwa kwa sababu zina tuhuma za kuendeleza na kufundisha masuala ya ushoga. Kama NGO uliyofanyia kazi mlikuwa mnahamasisha mambo hayo, kuajiriwa katika mifumo ya serikali tena wizara ya mambo ya ndani....sahau.
 
Kila nikifikiria kwenye huu mkasa wa dada yetu Ñaumia sana.Samahani lakini maaana Mimi sipo Jeshini,je ulijifungua Kwa kawaida au Operation??...Ili tujue pengine ulikuwa na mshono..Maana Afya inaweza kuwa uko vizuri ila mara nyingi Mshono huwa hawataki...
Hapana nilijifungua kwa kawaida na sina alama yoyote kuhusiana na hilo.
 
Pole sana ila Commandant wa chuo Cha kijeshi anapokufukuza imeisha hiyo hasa kozi za awali (Ukuruta)

Kumbuka kwa Swala lako limebase kwenye afya si wamesema unfit maana hufai au hutoweza kazi za kijeshi.

Kuna mwenzio mmoja enzi wanapiga CCP alikwenda kulalamika mpaka Bungeni ila hakuweza kurudishwa na akawashuhudia wenzie wakiapishwa kupitia Runinga.

N.B Dr Nabugari yule kijana aliye fukuzwa ni kweli alikuwa anatumia mihadarati acha kuchafua taswira ya majeshi vibaya.
Nashukuru sana mkuu,
 
Nilikua na wazo la kwenda uhamiaji jpo kwa njia za panya lilivotoka lile tangazo

Ila Mzee akanambia wakija kufanya ukaguzi na ukikutwa na hatia yni unafukuzwa chuo dah nikasema bora nusu shari kuliko shari kamili

Mtoa mada pole sanaa tafuta hospitali hizi ukapige day worker
Pole imeshatok ibad uwaz yajaYo
 
huko nyanda za juu kusini ngo nyingi zilifutwa na bado zitaendelea kufutwa kwa sababu zina tuhuma za kuendeleza na kufundisha masuala ya ushoga. Kama NGO uliyofanyia kazi mlikuwa mnahamasisha mambo hayo, kuajiriwa katika mifumo ya serikali tena wizara ya mambo ya ndani....sahau.
Hapana ngo niliyokuwa nafanyia ilikuwa inahusiana na maswala ya kilimo na lishe
 
Back
Top Bottom