Fani niliyosoma inaitwa "Biotechnology and Laboratory Science' kupitia fani hii naweza kufanya kazi Hospitali kwenye upande wa Molecular diagnostic, naweza kufanya kazi kwenye Taasisi yoyote inayojihusisha na utafiti iwe upande wa magonjwa ya binadamu, tafiti za kilimo na mifugo, kwenye maabara za viwandani kama Laboratory Analyst, maabara za migodini pia kama Laboratory Techologist, kufundisha baadhi ya masomo katika vyuo vya kati vya kilimo na mifugo, pia ningekuwa na mtaji ningeweza kujiajiri kwa kufungua ofisi inayojishughulisha na utoaji wa ushauri wa jinsi ya kudesign maabara za kisasa, uuzaji wa kemikali za maabara, vifaa vya maabara, vifaa tiba na vya kujifunzia.