Jeshi la Urusi kuwapokea Wanafunzi Watanzania waliopo Ukraine, wapewa maelekezo maalum ili warudishwe Tanzania

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Ubalozi wa Tanzania uliopo Urusi umetoa taarifa juu ya njia ambazo wanafunzi Watanzania walipo katika Chuo cha Taifa cha Sumy Nchini Ukraine wanazotakiwa kutumia pamoja na namba za simu kwa ajili ya mawasiliano wakati watakapokuwa wanaelekea sehemu salama kupokelewa.

Wanafunzi wanatakiwa kuelekea eneo la Sudja, watapokelewa na Jeshi la Urusi kisha kusafirishwa hadi Belgorod, hapo watakabidhiwa kwa maofisa wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Urusi kwa taratibu za kurejeshwa Tanzania.

Wanafunzi wameshauriwa kutoka kwa makundi wakiwa na bendera ya Tanzania ili kuwatambulisha kwenye safe corridor, pia wanaweza kuwasiliana na timu ya mapokezi kwa namba za simu walizowapatia.

 
Tungefanya kimyakimya kisha tutangaze baadaye. Au hatuna mawasiliano ya moja kwa moja na hao wanafunzi?
 
Ndio wabebe tu bendera ya Tanzania then watapokelewa
 
Ukiwa mbabe kwa watu wengi mwishowe unajikuta kila mtu anataka upigwe! Naona dalili USA inapoteza ushawishi wake dunian. Ni kama ina marafik wanafik tu ili wapate riziki kwake, waishi.
Watz wengi kwa level ya tunaopita vijiwen wako na Putin haijarishi kwanini. Kisa russia iko kinyume na USA!
 
Busara na hekma ya kutoegemea upande wowote zimeanza kulipa.
vijana wetu wanarudi salama n
Washauri wa Putin,imekuwa rahisi kumshawishi,ameanza kulegeza msimamo kidogo.
 
Wakiwatwanga ao ukraine tunatuma makomandoo wetu na mafuta ya nazi katoni mbili 😁😁
 
Hao wote wanaomshabikia mrusi ndio timu kidugu!!wengi wao ni wale ambao ukiwasikiliza hata hawaelewi mambo, ila ni ushabiki tu kama wa yanga na simba!!
 
Ivi Urusi wametupa sh, ngapi na EU "NATO"
Wametupa sh ngapi, mbona tunajichanganya, πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† wakizuiya mpunga wao huyu putin atamalizia miradi yetu kweli?.
 
Tanzania ilitumia akili kubwa sana juzi kwenye baraza la usalama UN kwa kujizuia kupiga kura. Kenya, Uganda, na Rwanda waliamua kupiga kura dhidi ya Urusi kama vile hakuna wanafunzi wao huko Ukraine.

Naamini uamuzi wa kutounga mkono upande wowote kwenye hiyo vita umesaidia wanafunzi wa Kitanzania kuwa salama kwa Warusi.

Vv
 
Naona taifa dg la Tanzania....tunapewa heshima kubwa ....

Asante nyerere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…