Jeshi La Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lakanusha Wanajeshi wa Ngazi ya Juu Kuongezewa Mshahara

Jeshi La Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lakanusha Wanajeshi wa Ngazi ya Juu Kuongezewa Mshahara

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa kuwa kuna habari ya uzushi iliyosambazwa na mtandao wa kiiamii wa Tanzania Abroad TV (TAT) kwamba Wanajeshi wa ngazi za juu wa JWTZ wameongezewa mshahara. Taarifa hiyo imeeleza kuwa ongezeko hilo limelipwa tarehe 18 Agosti 2023.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linaujulisha Umma kuwa taarifa hiyo ni ya uzushi na upotoshaji kwa jamii. Watanzania waelewe kuwa taarifa hiyo ina nia ovu, hivyo ipuuzwe.

Ukweli ni kwamba had leo tarehe 19 Agosti 2023 kwa JWTZ haijafika tarehe ya kulipwa mshahara. Aidha, hakuna ongezeko lolote la mshahara au malipo yoyote kwa Wanajeshi wa ngazi yoyote wa JWTZ yaliyofanyika tarehe 18 Agosti 2023 kama ilivyotajwa na mtandao huo wa kijamii.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linaendelea kufuatilia na kuchunguza kwa kina aliyehusika na upotoshaji huo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.​

View attachment 2721694
Bora mngeuchuna, kama mkiongezewa mwezi ujao so ndio watu watafualia? Vitu vingine ni vya kunyamaza tu.
 
Hapa pa kusoma tuu.Unaweza quote ukaonekana una taarifa za kuwasaidia
 
Back
Top Bottom