Jeshi la Zimamoto na Vibali vya Ujenzi

Jeshi la Zimamoto na Vibali vya Ujenzi

Obimbo

Member
Joined
Nov 17, 2020
Posts
35
Reaction score
36
Asalam Alekum ndugu zangu,

Naombeni ufafanuzi juu ya uhisika wa mamlaka ya Jeshi la Zimamoto katika taratibu za uombaji wa kibali cha ujenzi.

Nimekuwa nikisimamia ujenzi katika nyumba ya ibada mahala flani lakini watu hawa wamekuwa hawakauki katika eneo hili huku tukipigwa faini juu ya kutofuata utaratibu wao katika ujenzi.

Kupitia Mwongozo wa TAMISEMI juu ya vibali vya ujenzi ya mwaka 2018, katika sura ya 4, umetoa mtiririko wa wataalamu ambao watapitia mchoro huo kwa waombaji vibali lakini hao zimamoto hawamo.

Maswali yangu juu yao ni haya

1. Kama mwongozo huo haujawataja ni kwann waje kutusumbua wananchi tusio na hatia??

2. Kama ni matakwa ya Halmashauri kwann wasiwepo kwenyi list ya wakaguaji michoro kabla ya mhusika kupewa kibali cha ujenzi?

Nitafurahia nikipata mwongozo
 
Attachments

Kibali cha Ujenzi (Building Permit) ni nyaraka ya ki-Sheria inayotolewa na Mamlaka za Upangaji (Planning Authorities) ambazo ni Mamlaka za Serikali za Mitaa (The Local Government Authorities) ili kuruhusu Ujenzi mpya, kubomoa, kuondosha, kuongeza, au kufanya marekebisho makubwa. Kufanya hivyo kutasaidia kurekebisha kasoro zinazoweza kuathiri uimara wa jengo na mifumo mingine ya maji safi na taka, tahadhari za moto, umeme, usalama wa jamii na uharibifu au uchafuzi wa mazingira.
 
Kibali cha Ujenzi (Building Permit) ni nyaraka ya ki-Sheria inayotolewa na Mamlaka za Upangaji (Planning Authorities) ambazo ni Mamlaka za Serikali za Mitaa (The Local Government Authorities) ili kuruhusu Ujenzi mpya, kubomoa, kuondosha, kuongeza, au kufanya marekebisho makubwa. Kufanya hivyo kutasaidia kurekebisha kasoro zinazoweza kuathiri uimara wa jengo na mifumo mingine ya maji safi na taka, tahadhari za moto, umeme, usalama wa jamii na uharibifu au uchafuzi wa mazing

Kibali cha Ujenzi (Building Permit) ni nyaraka ya ki-Sheria inayotolewa na Mamlaka za Upangaji (Planning Authorities) ambazo ni Mamlaka za Serikali za Mitaa (The Local Government Authorities) ili kuruhusu Ujenzi mpya, kubomoa, kuondosha, kuongeza, au kufanya marekebisho makubwa. Kufanya hivyo kutasaidia kurekebisha kasoro zinazoweza kuathiri uimara wa jengo na mifumo mingine ya maji safi na taka, tahadhari za moto, umeme, usalama wa jamii na uharibifu au uchafuzi wa mazingira.

Kibali cha Ujenzi (Building Permit) ni nyaraka ya ki-Sheria inayotolewa na Mamlaka za Upangaji (Planning Authorities) ambazo ni Mamlaka za Serikali za Mitaa (The Local Government Authorities) ili kuruhusu Ujenzi mpya, kubomoa, kuondosha, kuongeza, au kufanya marekebisho makubwa. Kufanya hivyo kutasaidia kurekebisha kasoro zinazoweza kuathiri uimara wa jengo na mifumo mingine ya maji safi na taka, tahadhari za moto, umeme, usalama wa jamii na uharibifu au uchafuzi wa mazingira.
Shukran mkuu, Hiyo nyaraka ninayo, na ilipatikana baada ya kufuata taratibu zoote na hatimae kukabidhiwa. Licha ya kuwa na nyaraka hizo Zimamoto bado wananilipisha faini. Je! Ninalisolve vip bila ya kulipa faini wakati kibali ninacho??
 
Fire and OSHA compliance ni takwa la sheria kwa miradi yote ya Ujenzi (Hapa huwa wanatarget miradi mikubwa mikubwa) . Hapo unapotakiwa nenda kasajili mradi Fire gharama ni tsh 200,000/=, OSHA kusajili mradi ni bure kabisa.

Unachotakiwa kufanya waite haohao fire wakague site yako, watakupa report ambayo inaelekeza mapungufu, Utayafanyia kazi baada ya hapo utawaita tena wajiridhishe then utapewa control number utalipia hiyo tsh 200,000. Utasubiria cheti chao mchezo unakuwa umeisha hapo

NB:
Cheti unatakiwa kurenew baada ya mwaka kama mradi wako haujaisha
 
Looooooo utaratibu huu ungekuwepo na kufauatiliwa tusingekua na huu ujenzi wa ajabu, nenda pale kariakoo kuna flats ambazo kila mtu akisimama balcony mnaweza kubadilishana vikombe vya kahawa!sasa hivi vibali viliheshimiwa vipi hapo, maana hata hao zimamoto hawawezi kupafikia kama kuna emergency
 
Ujenzi holela unaratibiwa na Ofisi za Serikali za Mitaa
 
Fire and OSHA compliance ni takwa la sheria kwa miradi yote ya Ujenzi (Hapa huwa wanatarget miradi mikubwa mikubwa) . Hapo unapotakiwa nenda kasajili mradi Fire gharama ni tsh 200,000/=, OSHA kusajili mradi ni bure kabisa.

Unachotakiwa kufanya waite haohao fire wakague site yako, watakupa report ambayo inaelekeza mapungufu, Utayafanyia kazi baada ya hapo utawaita tena wajiridhishe then utapewa control number utalipia hiyo tsh 200,000. Utasubiria cheti chao mchezo unakuwa umeisha hapo

NB:
Cheti unatakiwa kurenew baada ya mwaka kama mradi wako haujaisha
Ahsante sana kwa Mwongozo mkuu, naomba kuuliza tena usinichoke, TAMISEMI wameelekeza ukaguzi wa michoro ufanywe katika eneo moja (One Stop Center) kabla ya kibali kutolewa kwanini tena nitoke kuwafuata Zimamoto peke yao???
 
Attachments

  • Screenshot_20221006-103319_Samsung Notes.jpg
    Screenshot_20221006-103319_Samsung Notes.jpg
    45.5 KB · Views: 38
Ahsante sana kwa Mwongozo mkuu, naomba kuuliza tena usinichoke, TAMISEMI wameelekeza ukaguzi wa michoro ufanywe katika eneo moja (One Stop Center) kabla ya kibali kutolewa kwanini tena nitoke kuwafuata Zimamoto peke yao???
Nadhani kuna jambo hujalifahamu. Kibali cha ujenzi kinatolewa na Halmashaur ya eneo husika mfano site yako iko Kinondoni basi kibali cha ujenzi utaombea hapo. Hapa huwa specific wanasimamia ujenzi holela,

Hawa watu wa fire na OSHA wao kazi yao ni kuhakikisha taratibu zote za usalama kwenye miradi zinafuatwa ikiwepo na majanga ya moto. Mwanzoni OSHA walikuwa wanasimamia mambo ya usalama pamoja na majanga ya moto yanayoweza kusababishwa na kazi zinazoendelea site husika, baadae Mambo yanayohusika na Fire yakarudishwa kwa watu Fire authority.

Kwa case yako ujenzi bado unaendelea, unachotakiwa kufanya sio kupeleka michoro bali ni kuwaita hao fire waje kuangalia site halafu watakupatia report ya mambo kadhaa yakuyafanyia kazi mfano site yako inatakiwa iwe na assembly point, mitungi ya kuzimia moto (fire extinguisher) kutokana na nature ya kazi zinazofanyika hapo site kama kuchomelea, kukata vyuma kwa gesi n.k

Kwa case ya kusubmit michoro ni kwa yale majengo ambayo yameshaisha na yanatumika mfano hospital, hii huwasaidia wao kujua idadi ya mitungi ya kuzimia moto, mpango wa uokoaji iwapo moto umetokea (Fire evacuation plan),
 
Shukran sana kwa mwongozo huu mkuu
 
Ahsante sana kwa Mwongozo mkuu, naomba kuuliza tena usinichoke, TAMISEMI wameelekeza ukaguzi wa michoro ufanywe katika eneo moja (One Stop Center) kabla ya kibali kutolewa kwanini tena nitoke kuwafuata Zimamoto peke yao???
Uko sahihi, ukishapeleka maombi ya kibali cha ujenzi, huku umeambatanisha na michoro, na kuikabizi kwa halmashauri husika; wao ndio hujiridhisha pamoja na taasisi zinginezo kwa kusaini nyuma ya michoro hiyo; baada ya kukamilika ndipo kibali kinatoka pamoja na kukabiziwa michoro iliyosainiwa na hao walengwa.

Baada ya mradi kukamilika, zimamoto huwa wanazungukia kwa kushauri namna ya kujihadhari pamoja na kushauri vifaa gani vya kujihami. Na huwa wanatoza ada kwa mwaka, ili waweze kukupatia cheti. Na ada hiyo inategemea na idadi ya watumiaji wa jengo husika.

Kama upo kwenye ujenzi na wanazunguka, jaribu kuwauliza tatizo ni nini, na ni kitu gani kiweze kutatuliwa ili ujenzi uendelee.​
 
Back
Top Bottom