Jeshi laidhibiti Myanmar baada ya kumshikilia Aung San Suu Kyi

Jeshi laidhibiti Myanmar baada ya kumshikilia Aung San Suu Kyi

Hivi kwanini Mynamar, Burma wasiihamishie Africa?
 
Huyu mama alipewa tuzo ya Nobel kwa kupinga utawala wa kijeshi kwa miaka mingi japo aliwekwa kizuizini muda mrefu.

Ila baadaye aliachiwa na chama chake kushika madaraka ila aliungana na wanajeshi pamoja na baadhi ya mabudha wenye msimamo mkali kwenye kampeni dhidi ya waislamu wa Rohingya ambapo maelfu waliuawa na wengine kuishia kwenye kambi za wakimbizi huko Bangladesh.

Sasa jeshi leo limemgeuka na kuangusha serikali yake, hii inaonyesha ushirika kati ya giza na nuru haudumu.

Kibaya zaidi ushirika wake na jeshi katika kuwaangamiza waRohingya umemuondolea sifa yake kuu aliyotunukiwa Nobel PP. Sasa hakuna anayetamka jina lake tena. Mataifa yanadai jeshi la Myanmar lirejeshe utawala wa kidemokrasia kama awali bila kusisitiza mama aachiwe huru.

Ukishahamia wrong side kisha ukatemwa, ni vigumu sana kuaminika tena na pande zote.
 
Sku jiwe nae atolewe hiv inakua n shangwe na, nderemo
 
Kwa kitendo cha kuwafukuza wale warohingya kwenye nchi yao bila ya yy kuchukua hatua yoyote ya kivitendo na kuwaacha wakihanya ughaibun kimeonyesha uhalisia wa huyu mama.
Hatachukua hatua gani wakati hana hata kauli yoyote ile kwenye jeshi
 
Mama wala hana kosa lolote kwenye mauwaji ya wa Rohingya.tatizo lipo kwenye jeshi, kiongozi wa jeshi ana nguvu kushinda Raisi na huyu bi mkubwa.

Ndo maana bi mkubwa hakuweza kutoa kauli yoyote ile wakati jeshi lilipoanzisha operation kwa jamii ya wa Rohingya.

Huyu bibi kama alikna hawezi ku control jeshi wakati yeye ni raisi maana yake hafai kua raisi na alitakiwa kujiuzuru mara moja. Hawezi kukwepa lawana za mateso kwa wa rohingya chini ya utawala wake.
 
Back
Top Bottom