Pre GE2025 Jeshi msipotambua umuhimu wenu, mtatumika vibaya kwa maslahi ya wanasiasa na wala siyo kwa maslahi ya Taifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hili halikubaliki
Halafu wanajisahau sana. Hao hawaelewi wala kukumbuka Iko siku yaja siku isiyo na jina wala tarehe wataondoka au wataondoshwa hapo kwenye viti wanavyokalia sasa na kuja kujiunga huku mitaani (kuishi na sisi) ambapo ndo wanabomoa na kuhaharibu sasa. Ulevi wa madaraka na matumizi mabovu ya madaraka ni mbaya sana.
 
Kwa kweli kila kiongozi anapaswa kufikiri kama unavyofikiri Mkuu.
Kila kiongozi atengeneze mazingira mazuri ili hata akitoka, Siku akihitaji huduma ya mtu mwingine, basi akutane na mazingira bora hata kama hakuna anayemfahamu hapo alipotoka!
So, wanajeshi kwa hili waungane na wananchi ili viongozi waachane na ANASA, wapunguze tozo, wazuie mfumko wa bei ya vitu, wapunguze nauli n.k.
Pia wahakikishe tunakuwa na katiba na sheria nzuri kwa kila raia na siyo kama hizi tulizo nazo sasa zinazowapendelea walioko madarakani na kuwakandamiza wadogo/wanyonge.
 
"......zinazowapendelea walioko madarakani." Na kuwakandamiza wadogo au kuwanyanyapaa wanyonge.
 
Ingia you tube angalia order of ranks za majeshi barani Africa uangalie jeshi letu ni la ngapi kwa ubora, ndo utaacha kulinganisha na majeshi Kama ya Kenya, Kongo, Ethiopia na kwingineko
 
Watanzania sio wajinga hawawezi andamana wakati wanajeshi wanafanya usafi ukizingatia watoto wa mbowe na lisu wapo ulaya na marekani na kwa namna yoyote maandamano hayawahusu
 
Amelidharau na kulishusha thamani sana jeshi letu pendwa. Aliombe radhi na asirudie tena huu upuuzi. Akatumie askari wa Jiji kufanya huo usafi na bajeti wanayo. Kwanza anatakiwa ajiuzulu!
 
Watanzania sio wajinga hawawezi andamana wakati wanajeshi wanafanya usafi ukizingatia watoto wa mbowe na lisu wapo ulaya na marekani na kwa namna yoyote maandamano hayawahusu
Jeshi lipo Kwa mujibu wa katiba na majukumu yake yapo wazi,pia maandamano yameruhusiwa na katiba ya nchi yetu,hivyo sio kosa kuandamana.
 
Jeshi lipo Kwa mujibu wa katiba na majukumu yake yapo wazi,pia maandamano yameruhusiwa na katiba ya nchi yetu,hivyo sio kosa kuandamana.
Kaandamane mimi ntasubiri nikimuona mke wa lisu,mbowe ,mnyika na watoto wao wapo front ntaandamana
 
Kaandamane mimi ntasubiri nikimuona mke wa lisu,mbowe ,mnyika na watoto wao wapo front ntaandamana
Kuandamana hakuna maana ya violence, tatizo ni mentality tu Kwamba maandamano lazima vurugu, maandamano ni njia moj a wapo kufikisha ujumbe,si zani yupo MTZ anayependa kuvuruga Amani, amani ni Kila kitu kuliko tofauti zetu za kisiasa.
 
Jeshi nalo limekubali kutumika vibaya wakati wanao ndugu zao uraiani wanasumbuka na hizi propaganda za kila siku ambazo serikali ya ccm imekuwa ikiziratibu.
 
Kuandamana hakuna maana ya violence, tatizo ni mentality tu Kwamba maandamano lazima vurugu, maandamano ni njia moj a wapo kufikisha ujumbe,si zani tupo MTZ anayependa kuvuruga Amani, amani ni Kila kitu kuliko tofauti zetu za kisiasa.
Kama kuandamana ni kufikisha ujumbe viongozi wote wa chadema wanapaswa kuwa front line sio kukimbia na kujificha kwa sababu wamepewa taarifa ya hatari,pia wahakikishe familia zao ziko mbele tuone wanamaanisha
 
Siku ya usafi Samiah na Chalamila watakuwa wanafanya usafi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…