Pre GE2025 Jeshi msipotambua umuhimu wenu, mtatumika vibaya kwa maslahi ya wanasiasa na wala siyo kwa maslahi ya Taifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hili halikubaliki
Halafu wanajisahau sana. Hao hawaelewi wala kukumbuka Iko siku yaja siku isiyo na jina wala tarehe wataondoka au wataondoshwa hapo kwenye viti wanavyokalia sasa na kuja kujiunga huku mitaani (kuishi na sisi) ambapo ndo wanabomoa na kuhaharibu sasa. Ulevi wa madaraka na matumizi mabovu ya madaraka ni mbaya sana.
 
Kwa kweli kila kiongozi anapaswa kufikiri kama unavyofikiri Mkuu.
Kila kiongozi atengeneze mazingira mazuri ili hata akitoka, Siku akihitaji huduma ya mtu mwingine, basi akutane na mazingira bora hata kama hakuna anayemfahamu hapo alipotoka!
So, wanajeshi kwa hili waungane na wananchi ili viongozi waachane na ANASA, wapunguze tozo, wazuie mfumko wa bei ya vitu, wapunguze nauli n.k.
Pia wahakikishe tunakuwa na katiba na sheria nzuri kwa kila raia na siyo kama hizi tulizo nazo sasa zinazowapendelea walioko madarakani na kuwakandamiza wadogo/wanyonge.
 
Kwa kweli kila kiongozi anapaswa kufikiri kama unavyofikiri Mkuu.
Kila kiongozi atengeneze mazingira mazuri ili hata akitoka, Siku akihitaji huduma ya mtu mwingine, basi akutane na mazingira bora hata kama hakuna anayemfahamu hapo alipotoka!
So, wanajeshi kwa hili waungane na wananchi ili viongozi waachane na ANASA, wapunguze tozo, wazuie mfumko wa bei ya vitu, wapunguze nauli n.k.
Pia wahakikishe tunakuwa na katiba na sheria nzuri kwa kila raia na siyo kama hizi tulizo nazo sasa zinazowapendelea walioko madarakani.
"......zinazowapendelea walioko madarakani." Na kuwakandamiza wadogo au kuwanyanyapaa wanyonge.
 
Hili suala la jeshi kuamriwa kufanya usafi kila vyama vya upinzani vinapotangaza maandamano halikubaliki.

Wote tunalia hali ngumu ya maisha ikiwemo wanajeshi pamoja na familia zao na viongozi wa serikali wako kimya, halafu wanapotakiwa kufanya kitu walau hata kwa shinikizo la maandamano, wanakimbilia Kuomba wanajeshi wetu wakafagie barabara na kuokota makopo! Kweli jamani?!! Hapana. Hii haikubliki kabisa.

Wanajeshi tumikieni maslahi ya nchi na wananchi wake na wala siyo viongozi wa hovyo wanaotusababishia hali ngumu kutokana na matumizi yao ya anasa huku raia tunaumia.

Jitambueni nyinyi ni watu wa muhimu sana kwa nchi na mnapaswa kuheshimiwa na siyo kutumika.
Ingia you tube angalia order of ranks za majeshi barani Africa uangalie jeshi letu ni la ngapi kwa ubora, ndo utaacha kulinganisha na majeshi Kama ya Kenya, Kongo, Ethiopia na kwingineko
 
Hoja yako imekaa kisiasa mno. Kwani Usafi hauwezi kufanyika siku nyingine isipokuwa siku hiyo ambayo hao jamaa walishapanga maandamano?
Tukumbuke na kuzingatia kwamba endapo yatatokea maafa (kama maandamano yatafanyika) mm na ww tutahusika kwa namna moja au nyingine e.g. Kuzika/rambirambi, kukosa amani siku hiyo - maduka/fremu na shughuli /huduma zitatatizika, huenda wakahusika Ndg au Jamaa zetu humo.
Mchuma janga hula na wakwao.
Watanzania sio wajinga hawawezi andamana wakati wanajeshi wanafanya usafi ukizingatia watoto wa mbowe na lisu wapo ulaya na marekani na kwa namna yoyote maandamano hayawahusu
 
Kweli kabisa mkuu.
Wanajeshi wana kazi siku zote -asikudanganye mtu. Kila kukicha salama tutambue uwepo wao. Kama hakuna vita au Vurugu; huo huwa ni wakati wa kazi za maandalizi e.g. mazoezi, mafunzo ya mbinu mpya na silaha mpya zinazoendana na wakati n.k. ie. Wanajeshi hawapumziki kama tunavyowadhania eti tunawaona wanaranda-randa mitaani. Ukiwaona mitaani ujue nayo hiyo ni mojawapo ya shughuli za ki-Upelezi.
Kwa kweli Mkuu wa Mkoa inafaa afanye mabadiliko atumie nguvu kazi nyingine sio Wanajeshi. Jeshi lipewe na liachiwe HESHIMA yake.
Amelidharau na kulishusha thamani sana jeshi letu pendwa. Aliombe radhi na asirudie tena huu upuuzi. Akatumie askari wa Jiji kufanya huo usafi na bajeti wanayo. Kwanza anatakiwa ajiuzulu!
 
Watanzania sio wajinga hawawezi andamana wakati wanajeshi wanafanya usafi ukizingatia watoto wa mbowe na lisu wapo ulaya na marekani na kwa namna yoyote maandamano hayawahusu
Jeshi lipo Kwa mujibu wa katiba na majukumu yake yapo wazi,pia maandamano yameruhusiwa na katiba ya nchi yetu,hivyo sio kosa kuandamana.
 
Kaandamane mimi ntasubiri nikimuona mke wa lisu,mbowe ,mnyika na watoto wao wapo front ntaandamana
 
Kuandamana hakuna maana ya violence, tatizo ni mentality tu Kwamba maandamano lazima vurugu, maandamano ni njia moj a wapo kufikisha ujumbe,si zani yupo MTZ anayependa kuvuruga Amani, amani ni Kila kitu kuliko tofauti zetu za kisiasa.
 
Hili suala la jeshi kuamriwa kufanya usafi kila vyama vya upinzani vinapotangaza maandamano halikubaliki.

Wote tunalia hali ngumu ya maisha ikiwemo wanajeshi pamoja na familia zao na viongozi wa serikali wako kimya, halafu wanapotakiwa kufanya kitu walau hata kwa shinikizo la maandamano, wanakimbilia Kuomba wanajeshi wetu wakafagie barabara na kuokota makopo! Kweli jamani?!! Hapana. Hii haikubliki kabisa.

Wanajeshi tumikieni maslahi ya nchi na wananchi wake na wala siyo viongozi wa hovyo wanaotusababishia hali ngumu kutokana na matumizi yao ya anasa huku raia tunaumia.

Jitambueni nyinyi ni watu wa muhimu sana kwa nchi na mnapaswa kuheshimiwa na siyo kutumika.
Jeshi nalo limekubali kutumika vibaya wakati wanao ndugu zao uraiani wanasumbuka na hizi propaganda za kila siku ambazo serikali ya ccm imekuwa ikiziratibu.
 
Kuandamana hakuna maana ya violence, tatizo ni mentality tu Kwamba maandamano lazima vurugu, maandamano ni njia moj a wapo kufikisha ujumbe,si zani tupo MTZ anayependa kuvuruga Amani, amani ni Kila kitu kuliko tofauti zetu za kisiasa.
Kama kuandamana ni kufikisha ujumbe viongozi wote wa chadema wanapaswa kuwa front line sio kukimbia na kujificha kwa sababu wamepewa taarifa ya hatari,pia wahakikishe familia zao ziko mbele tuone wanamaanisha
 
Siku ya usafi Samiah na Chalamila watakuwa wanafanya usafi?
 
Kaandamane mimi ntasubiri nikimuona mke wa lisu,mbowe ,mnyika na watoto wao wapo front ntaandamana
.
JamiiForums1389173211.jpg
 
Back
Top Bottom