Pre GE2025 Jeshi msipotambua umuhimu wenu, mtatumika vibaya kwa maslahi ya wanasiasa na wala siyo kwa maslahi ya Taifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Watu humu hawafahamu siasa za kikomunisti na kijamaa.

Let make it simple nchi yetu ni nchi ya kijamaa (ukomunisti uchwara ) kwa mujibu wa katiba pasipo kujali unafuatwa kivitendo kikamilifu au laah!

Ukijua haya huwezi shangaa yanayo endelea kati ya CCM na majeshi yote.
Ila hali ya Sasa hivi ni ukapitalisti mtupu usoshalisti upo kwenye makaratasi tu.
 
Hili suala la jeshi kuamriwa kufanya usafi kila vyama vya upinzani vinapotangaza maandamano halikubaliki.

Wote tunalia hali ngumu ya maisha ikiwemo wanajeshi pamoja na familia zao na viongozi wa serikali wako kimya, halafu wanapotakiwa kufanya kitu walau hata kwa shinikizo la maandamano, wanakimbilia Kuomba wanajeshi wetu wakafagie barabara na kuokota makopo! Kweli jamani?!! Hapana. Hii haikubliki kabisa.

Wanajeshi tumikieni maslahi ya nchi na wananchi wake na wala siyo viongozi wa hovyo wanaotusababishia hali ngumu kutokana na matumizi yao ya anasa huku raia tunaumia.

Jitambueni nyinyi ni watu wa muhimu sana kwa nchi na mnapaswa kuheshimiwa na siyo kutumika.
Nawatakia kila la kheri nyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa uimara, bidii na weledi katika kudhibiti uharibifu, uporaji na uhalifu mathalani wa mapanyarodi, nyumbu na maandamanaji haramu 🐒

Wanainchi wengi hususani mimi mwenyewe nawapongeza sana kwa ubunifu mlokuja nao. Suala la usafi wa mazingira jijini Dar es Salaam ni muhimu sana hususani kipindi hiki hatarishi kwa mlipuko wa kipindupindu....

Yeyote atakae jitokeze kuchafua mliposafisha huyo ni takataka tembeeni nae bila mbambamba mwendo wa ngiri, ili iwe fundisho kwa wakaidi na wachafua mazingira wengine....

Tunategemea Amani na utulivu wa kiwango cha lami January 23 na 24...🐒

Mungu Ibariki Tanzania..
 
Alafu Kuna mtu anasema waliozaliwa tisini 90s ndio wanasabanisha matatizo Kwa Taifa eti kisa wanamambo ya laana wakati inajulikana Taifa lipo kwenye mikono ya kizazi gani
 
Unaongelea jeshi ambalo linawapiga raia hovyo hovyo mitaani?
 
Kama USA wako very strict.
Wangekuwa kama hawa wetu, Trump angekuwa madarakani hadi kesho (japo binafsi pia huwa namkubali sana Trump).
Hawa wa kwetu wanaongozwa zaidi na akili za tumboni za kulinda ugali wao na familia zao na wala siyo kuangalia maslahi ya nchi.
Jeshi la kwanza kabisa baada ya ya la wakoloni kutimuliwa na nyerere lilijengwa na vijana was UVCCM!

Tusishangae Kwa haya!!

La kujiuliza he jwtz watakubali!!?
 
Hili suala la jeshi kuamriwa kufanya usafi kila vyama vya upinzani vinapotangaza maandamano halikubaliki.

Wote tunalia hali ngumu ya maisha ikiwemo wanajeshi pamoja na familia zao na viongozi wa serikali wako kimya, halafu wanapotakiwa kufanya kitu walau hata kwa shinikizo la maandamano, wanakimbilia Kuomba wanajeshi wetu wakafagie barabara na kuokota makopo! Kweli jamani?!! Hapana. Hii haikubliki kabisa.

Wanajeshi tumikieni maslahi ya nchi na wananchi wake na wala siyo viongozi wa hovyo wanaotusababishia hali ngumu kutokana na matumizi yao ya anasa huku raia tunaumia.

Jitambueni nyinyi ni watu wa muhimu sana kwa nchi na mnapaswa kuheshimiwa na siyo kutumika.
Wanajeshi wanapaswa kuheshimu mamlaka ndio maana wakuu wa mkoa na wilaya wanapigiwa salute na hao wanajeshi ,wakipewa agizo ni utii ,nawasifia sana ni watiifu
 
Alafu Kuna mtu anasema waliozaliwa tisini 90s ndio wanasabanisha matatizo Kwa Taifa eti kisa wanamambo ya laana wakati inajulikana Taifa lipo kwenye mikono ya kizazi gani
Nilishaandika kabisa uzi hapa JF kuhusiana na kizazi hiki kinachotuongoza Mkuu. Nadhani mambo yatakaa sawa tukifanya kama walivyofanya Burkina Fasso. Tuweke vijana wadogo lakini wazalendo kwa Taifa Lao.
 
Nawatakia kila la kheri nyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa uimara, bidii na weledi katika kudhibiti uharibifu, uporaji na uhalifu mathalani wa mapanyarodi, nyumbu na maandamanaji haramu 🐒

Wanainchi wengi hususani mimi mwenyewe nawapongeza sana kwa ubunifu mlokuja nao. Suala la usafi wa mazingira jijini Dar es Salaam ni muhimu sana hususani kipindi hiki hatarishi kwa mlipuko wa kipindupindu....

Yeyote atakae jitokeze kuchafua mliposafisha huyo ni takataka tembeeni nae bila mbambamba mwendo wa ngiri, ili iwe fundisho kwa wakaidi na wachafua mazingira wengine....

Tunategemea Amani na utulivu wa kiwango cha lami January 23 na 24...🐒

Mungu Ibariki Tanzania..
Hoja yako imekaa kisiasa mno. Kwani Usafi hauwezi kufanyika siku nyingine isipokuwa siku hiyo ambayo hao jamaa walishapanga maandamano?
Tukumbuke na kuzingatia kwamba endapo yatatokea maafa (kama maandamano yatafanyika) mm na ww tutahusika kwa namna moja au nyingine e.g. Kuzika/rambirambi, kukosa amani siku hiyo - maduka/fremu na shughuli /huduma zitatatizika, huenda wakahusika Ndg au Jamaa zetu humo.
Mchuma janga hula na wakwao.
 
Jeshi la kwanza kabisa baada ya ya la wakoloni kutimuliwa na nyerere lilijengwa na vijana was UVCCM!

Tusishangae Kwa haya!!

La kujiuliza he jwtz watakubali!!?
Kwa nini wasikubali Mkuu?!
Mi nafikiri kuna mambo huwa si ya kuomba bali ni kutekeleza tu kwa vitendo ikiwemo mabadiliko.
 
Ni wizi mtupu mkuu.
Wengi wanaumia, wanafaidi wachache
Yeah. Na hao wachache ndo wamelewa kiasi cha kutaka kuwaamuru hata Wanajeshi wetu watukufu eti wainame washike mfagio kufagia barabara ili VX 9 zilizonunuliwa kwa kodi zetu ambazo ndizo wanazotumia wao zipite vizuri. Ni AIBU. AIBU mno.
 
Hili halikubaliki
 
Kweli kabisa mkuu.
Wanajeshi wana kazi siku zote -asikudanganye mtu. Kila kukicha salama tutambue uwepo wao. Kama hakuna vita au Vurugu; huo huwa ni wakati wa kazi za maandalizi e.g. mazoezi, mafunzo ya mbinu mpya na silaha mpya zinazoendana na wakati n.k. ie. Wanajeshi hawapumziki kama tunavyowadhania eti tunawaona wanaranda-randa mitaani. Ukiwaona mitaani ujue nayo hiyo ni mojawapo ya shughuli za ki-Upelezi.
Kwa kweli Mkuu wa Mkoa inafaa afanye mabadiliko atumie nguvu kazi nyingine sio Wanajeshi. Jeshi lipewe na liachiwe HESHIMA yake.
Umenena vyema Mkuu.
Jasho jingi wakati wa amani, damu chache wakati wa vita.
 
Back
Top Bottom