Jeshi, Polisi na Usalama msijihusishe na siasa wananchi watawaona maadui

Jeshi, Polisi na Usalama msijihusishe na siasa wananchi watawaona maadui

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Jeshi, Polisi na Usalama msijihusishe na siasa na kuanza kupendelea vyama kwasababu inaelekea wananchi wengi sio washabiki wa vyama bali ni wapenda haki.

Vitendo vya watu kuona waziwazi wanaiba kura zao mnajenga uadui ambao utakuwa mbaya kuutoa.

Ushauri ni kwamba kuweni upande wa haki. Fanyeni usalama kwa kujali haki na sio kukandamiza watu.

Bila hivyo itafika sehemu hata hao wanao watuma hawatawaheshimu kama wananchi wengi hawako nyuma yenu.

Nyie mnatakiwa kuwa watu wa kupendwa si kuchukiwa.

Mkiwabana watu kupata haki kihalali watatafuta haki kinyemela kama Congo na sehemu za hivyo
 
Back
Top Bottom