Jesse John wa TBC Taifa tafadhali tafuta mtoto wa Kiume umuite Haruna Niyonzima

Jesse John wa TBC Taifa tafadhali tafuta mtoto wa Kiume umuite Haruna Niyonzima

Naona sasa ni wakati muafaka kwa huyu Mtangazaji wa michezo wa TBC Taifa aitwae Jesse John amuombe Mkewe akubali ' kumbebea ' Mimba ili amzalie Mtoto wa Kiume kisha amuite Haruna Niyonzima.

Nimesikiliza matangazo ya TBC Taifa yaliyokuwa ' mubashara ' na Mtangazaji wa leo akiwa ni Jesse John na alikuwa anaenda vizuri tu na sisi hadi Kipindi cha Kwanza kilipoisha ila hali ilikuja kubadilika pale kilipoanza Kipindi cha pili huku Yanga FC ikimuingiza Mchezaji Haruna Niyonzima.

Mtangazaji huyu ameshindwa kabisa kuficha ' mahaba ' yake ' niue ' kwa huyu Mchezaji kwani kwa takribani dakika zote 45 za Kipindi cha pili Mchezaji ambaye alikuwa akimtaja sana huku akimpamba hadi ' kutuboa ' sisi Wasikilizaji wake ni huyu Haruna Niyonzima.

Kilichonishangaza zaidi ni kwamba kuna wakati huyo Mchezaji alikuwa hata hana mpira na mpira uko sehemu nyingine lakini Mtangazaji Jesse John alianza sasa ' kusifia ' aina ya ' utembeaji ' wa Haruna Niyonzima hadi anavyoiweka mikono yake kitu ambacho kiukweli kilinishtua sasa Mimi Mwanaume wa ' Pwani ' hadi kudhani kama siyo kuhisi kuwa pengine huyu Mtangazaji angekuwa ni wa Kike basi TBC ingepata ' Shemeji ' kutoka nchini Rwanda.

Huku Pwani Kwetu Mtoto wa Kiume kuanza kumsifia ' Mwanaume ' mwenzio ni ' taboo ' kabisa na nimemshangaa sana huyu Mtangazaji wa TBC1 Jesse John kuwa hii nguvu na huu moyo wa ' kumsifia ' kiasi kile Mchezaji wa Yanga FC Haruna Niyonzima kautoa wapi na nadhani pengine hata Mkewe huwa hamsifii hivi kama ambavyo amemsifia leo huyu Mchezaji wa Kinyarwanda Haruna Fadhil Hakizimana Niyonzima a.k.a Niyo a.k.a Fabregas wa Mkoani Gisenyi nchini Rwanda.

Halafu sijui Watangazaji wa michezo wa TBC1 mna ' matatizo ' gani hakyanani. Hivi kwanini msiwe kama ' Poti ' wangu Chacha Maginga ambaye anatangaza ' Kiume ' na ' Kishujaa ' sana hadi Mtu unafurahia kumsikiliza na huwezi jua ama ana ' mahaba ' na Timu gani au Mchezaji gani. TBC wapigeni ' msasa ' hawa Watangazaji wenu wa hii ' mipira ' ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara ( VPL ) kwani kila ' Uchao ' wao ' wanakengeuka ' tu na itafikia muda tutawachoka na tutahamia ama Sibuka fm au Radio One Stereo ambako ' upuuzi ' wa hao Watangazaji wenu haupo.

" Siku zote dawa chungu na inayouma ( yenye maumivu ) ndiyo hutibu vizuri " Mwanamume nimemaliza kutoa langu la moyoni na ' nasepa ' zangu nikiamini kabisa kuwa ' Wagonjwa ' watapona.
NIYONZIMA NI MMOJA TU DUNIANI

Leo tumeona pasi za nyoka, pasi chonganishi, pasi mpenyezo, pasi lawama, pasi mashauzi, pasi ngwengwe, pasi mbinuko, pasi mbonyeo toka kwa mtoto wa Gisenyi Haruna Niyonzima na ile mikrosi upinde, mikrosi mmimino,mikrosi mshale toka Juma Abdul Jaffar Mnyamani.

Tanzania Prisons WATCH IT . . . . .Hata kama mnadhani mnaweza kucheza na Yanga . . . NOT TO THAT EXTENT . . . !!
 
duh! makavu live

Kama kawaida yangu Mkuu huwa ' simbakishi ' Mtu hasa nikiona anayagusa kwa namna moja au nyingine ' maslahi ' ya Simba Sports Club. Na ' nitawanyoosha ' sana tu Mkuu hadi wawe ' wanatangaza ' Kimaadili na siyo Kimabaha kwa ' kuipendelea ' na ' kuifagilia ' Yanga FC.
 
NIYONZIMA NI MMOJA TU DUNIANI

Leo tumeona pasi za nyoka, pasi chonganishi, pasi mpenyezo, pasi lawama, pasi mashauzi, pasi ngwengwe, pasi mbinuko, pasi mbonyeo toka kwa mtoto wa Gisenyi Haruna Niyonzima na ile mikrosi upinde, mikrosi mmimino,mikrosi mshale toka Juma Abdul Jaffar Mnyamani.

Tanzania Prisons WATCH IT . . . . .Hata kama mnadhani mnaweza kucheza na Yanga . . . NOT TO THAT EXTENT . . . !!

Na Mimi pia jana / leo nimetoa ' pasi chonganishi ' kwa Uongozi wa TBC juu ya huyu Mtangazaji Jesse John. Ngoma ' droo ' Mkuu.
 
Hapa bongo kwann watu hawataki waandishi na watangazaji wasionyeshe mahaba? Mbona nchi za wenzetu mtangazaji anatangaza mechi na goli likifungwa LA timu yake anainuka na kushangilia kabisa! Hata wachambuzi kina Henry, jammie carragher, Owen wote wakichambua wanaonyesha wazi mahaba yao yapo wapi lkn ni hapa peke Tz inakuwa ni kosa.
 
Vingekuwa ni vitu vya kawaida nisingevipazia sauti humu JF. Jifunze kutumia ' brain ' yako vizuri sometimes sawa?
Natumia mno brain kutathmini kila jambo. Yaani mtangazaji kumsifia mchezaji ndo maana kuwa ana mahaba na timu.!?

Mimi ni Mnyama. Lakini kwa hili mkuu hapana. Commentators in EPL na kwingineko tunawasikia namna anavyopaisha mchezaji je ana mahaba na timu.?

Tafakari bhana...!
 
Hivi kumbe hata ushindi wa ' kimagumashi / kununua ' nao huwa mnaushangilia kiasi hiki? Sisi Wana Simba SC tulijua fika kuwa iwe isiwe leo lazima tu Prisons hata ' wakibana ' vipi ila mngewafunga tu kwani tayari Bosi wao Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba ambaye ni ' mnazi wa kutupwa ' wa Yanga FC atakuwa aliwaambia kuwa ' wakiwabania ' tu Yanga FC leo basi Mishahara yao ya mwezi ujao wataisikia katika ' Bomba ' tu au labda wakiibania Yanga FC basi watafute ' ajira ' kwingineko hivyo Vijana wa Prisons FC ' wakatafakari ' wakaona isiwe taabu ngoja wawaachie akina Tambwe na Chirwa wawafunge ili maisha yaendelee.

Najua Yanga FC mtashinda mechi na Prisons FC, Kagera Sugar ( ambao wana hasira na Simba SC hivyo watawaachieni ili watukomoe sisi ) na ' Mitoto ' yenu ' mijinga ' Toto Africans ILA tuna uhakika kuwa Timu hizi mbili mtakazocheza nazo Mbeya City na Mbao FC ndiyo mtakapoliacha Kombe Kwao kwani hamna ' ubavu ' wa Kuwafunga hata mfanyeje na kwa aina ya ' Fitna ' ambayo Simba SC tunaenda kuicheza katika mechi yenu na Mbeya City na Mbao FC Yanga FC ' mkishinda ' hizo mechi ' nitajiteka ' menyewe hadi Ununio Mahaba Beach.

Mbeya City na Mbao FC ndiyo ' mbeleko ' ya Mnyama Mnyamani ( Simba Sports Club ) kuwa Mabingwa wapya wa Vodacom Premier League kwa msimu wa 2016 / 2017 na ' Umafia ' ambao Simba SC tunaenda kuwafanyia Yanga FC hakika mtajuta kutufahamu na haijawahi kutokea nchini Tanzania kwani mwaka huu iwe isie ikibidi hata kutoana ' Makafara ' au kutenda ' dhambi ' kubwa ili tu Simba SC iwe Bingwa tutafanya tu hivyo bila wasiwasi wowote kwani tumechoka sasa na matusi na kejeli za Yanga FC na tumechoka kwa miaka minne ( 4 ) kuwakodoloe tu macho kodo Yanga FC na Azam FC wakipanda zao ' Mbung'o / Ndege ' kwenda Kimataifa zaidi.

Kitaeleweka tu mwaka huu kudadadeki!!!!!!!
Nendeni FIFA mkaandamane mpewe point 3 huku watu wanatoa burudani uwanjani Na kuchukua Point 3 kwa mechi zote zilizobaki moja tayali zimebakia NNE .
 
Hapa bongo kwann watu hawataki waandishi na watangazaji wasionyeshe mahaba? Mbona nchi za wenzetu mtangazaji anatangaza mechi na goli likifungwa LA timu yake anainuka na kushangilia kabisa! Hata wachambuzi kina Henry, jammie carragher, Owen wote wakichambua wanaonyesha wazi mahaba yao yapo wapi lkn ni hapa peke Tz inakuwa ni kosa.

Tanzania siyo huko Ulaya. Kwahiyo ikitokea hao Watangazaji wa huko Ulaya wakianzisha ' mtindo ' wa Kutangaza huku wakiwa wamevalia ' chupi ' zao Vichwani kwa maana hiyo ungependa pia na hawa Watangazaji wetu wa Kibongo nao wawaige? Tumia vizuri ' brain ' yako katika kujenga ' hoja '.
 
Natumia mno brain kutathmini kila jambo. Yaani mtangazaji kumsifia mchezaji ndo maana kuwa ana mahaba na timu.!?

Mimi ni Mnyama. Lakini kwa hili mkuu hapana. Commentators in EPL na kwingineko tunawasikia namna anavyopaisha mchezaji je ana mahaba na timu.?

Tafakari bhana...!

Simba SC hatuna ' Shabiki ' hopeless wa mfano wako na usitake ' kunitibua ' Kichwa changu tafadhali ' nikakinukisha ' sasa hivi!
 
Simba SC hatuna ' Shabiki ' hopeless wa mfano wako na usitake ' kunitibua ' Kichwa changu tafadhali ' nikakinukisha ' sasa hivi!
Kinukishe tu. We nani katika Simba SC uwezae kumchagulia au kupima ushabiki wa klabu kwa binadamu

Ni mshabiki toka kitambo, chukua hiyo
 
Tanzania siyo huko Ulaya. Kwahiyo ikitokea hao Watangazaji wa huko Ulaya wakianzisha ' mtindo ' wa Kutangaza huku wakiwa wamevalia ' chupi ' zao Vichwani kwa maana hiyo ungependa pia na hawa Watangazaji wetu wa Kibongo nao wawaige? Tumia vizuri ' brain ' yako katika kujenga ' hoja '.
Nadhani wewe ndio utumie akili yako vizuri sababu unaleta chuki tu kushabikia timu si kitu cha ajabu wala kosa. Na usilazimishe unayoyataka wewe ndio mtu hafanye, wewe mwandishi fuata unayoona sahihi na wao waache wafanye wanavyoona sahihi.
 
Shida mleta mada siku zote anajiona yupo sahihi akishindwa ataanza mitusi kwenda mbele.
 
Na wewe mleta uzi mapenzi yako na bodyguard wa Majaliwa yaliishia wapi? Ushapigwa goli ngapi tunduni?
 
Back
Top Bottom