Jezi mpya za Simba SC 2019/2020

Nini maana ya Third Kit
 
Sisi kama wazee wa simba tumezikataa rangi za jeziiii ni kuizalilisha timu..

Haiwezekani tutumie jezi zinazotuahushia heshima kama club
 
Sema wewe Mkuu sababu ni Nguvu moja mwenzao.

Mana niliona sehemu wanasema kwa mbali zinafanana na za Barca nikabaki nashangaa tu.
 
Mkuu unafuatilia mpira kweli au ndy wale wanaojua kulaumu tu? bila ya kufanya uchunguzi kwanza. Umeambiwa CAF inazitaka team ziwe na jezi aina tatu tofauti, sasa simba tayari ina 2, kwahy kuna ubaya gani wakiongeza rangi nyingine? Kadri siku zinavyokwenda na mambo yanabadilika.

Kanuni na taratibu za mpira wa miguu zinabadilika ili kukidhi matakwa na mahitaji ya kipindi husika, kwahy hili suala la kuongeza rangi nyingine haliepukiki na me binafsi nimelielewa sana. Alafu rangi ikiwa ni zilezile zinachosha sana, sema sisi huu ujinga wa usimba na Yanga unatuharibu na kuzidi kudumaza akili zetu.

Duniani kote team kubwa kubwa kama unafatilia vzr, wana jezi aina tatu, na mara nyingi huwa zinabadilika badilika ktk rangi, hasa hizi za away, sasa simba ni nani wasifanye hvy, ikiwa ndy team pekee Tanzania inayoonesha ishara kuwa inataka kujipambanua kama ni team ya kisasa kwasababu ya aina ya utofauti ya mmb inayoyafanya hasa kipindi hiki cha miaka mitatu tangu mabadiliko ya uendeshaji wa club yafanyike.
 
Hiyo picha ya mwisho mkuu naomba waliopiga wamegeuka kwa nyuma kuna vitu nataka nijiridhishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…