Jezi za Nigeria zatajwa kuwa ni nzuri kuliko zote kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2018, nchini Russia

Jezi za Nigeria zatajwa kuwa ni nzuri kuliko zote kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2018, nchini Russia

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Jezi za Timu ya Taifa ya Nigeria za Kombe la dunia 2018 zimemalizika ndani ya dakika chache tangu kuingizwa sokoni leo hii Ijumaa, (SOLD OUT)

Foleni kubwa ya mashabiki ilionekana leo katika duka la Nike London mtaa wa Oxford, wakisubiri jezi hizo.

Jezi zimetajwa kuwa ni nzuri kuliko zote zitakazoonekana nchini Russia mwaka huu kwenye michuano ya kombe la dunia.

Nike walitaka kuzipeleka sokoni mapema wiki hii lakini wakasogeza mbele kutokana na idadi ya watu waliohitaji kuzidi kuwa kubwa.

Jezi zimeuzwa zote ndani ya dakika chache na hazipatikani pia tovuti ya Nike.

Kitu kingine cha kushangaza, jezi za kufanyia mazoezi nazo pia zimekuwa SOLD OUT.

Jezi ya juu pekee inauzwa na NIKE kwa pauni 64.95 ambayo ni sawa na Tsh 197,504.
IMG_20180602_001946_015.jpg
FB_IMG_1527887473485.jpg
FB_IMG_1527887454494.jpg
FB_IMG_1527887484225.jpg
IMG_20180602_002022_346.jpg
 
Yeah ni bonge ya jezi aiseee lkn pia na hizi kampuni ziache kuover price sport kits,huwezi muuzia mtu nguo ya juu pekee kwa bei hiyo,shout outs kwa starboi imemtoa balaa
 
Kwa hiyo nadhani hii itakuwa first time kwny WC timu inavaa shorts yenye maua,waende wacheze mpira sio kuishia makundi tu
Exactly..Siyo wawe vibonde tena kwa michuano hiyo
 
Jessy ziko poa zimetulia lakini cha ajabu hazichezi mpira wametoa Advertising kwa ajili ya kuvuta watazamaji wa mpira kutoka Africa
 
Wanatumia udhaifu ule ule wa kufikiri wa waAfrica kunyakua nyakua mapesa , wame overate price kwa sababu kuzidiana kuonesha ufahari kumbe wanatuumiza kwa kutumia psychology
 
Back
Top Bottom