Wana-JF wa Arusha,
Wababa :Enda-Subhai!
Wamama :Endakwenya!
Wote :Subhati Ngerai, habari-ya-Ngaji?..Engai Engoitoi!...poleni sana!
Wapendwa,
Nia yangu si ubaguzi wa Makabila au maeneo, lakini kama mjuavyo, Maasai ndio mila/kabila PEKEE linalojaribu kushindana na kasi ya mabadiliko yaliyoasisiwa na ujio wa wageni nchini!
Nia ya post hii ni kuwajulisha wana-JF wa Arusha na maeneo ya jirani kwamba kuelekea mwisho wa mwaka 2010 tuna Mpango Kabambe wa kuasisi mijumuiko ya kijamii, ambapo kwa kufanya hivyo tutakuwa tunatekeleza kwa vitendo upiganiaji haki wetu, ambao kwa bahati mbaya umekuwa kimabandiko-zaidi kuliko uhalisia..Charity begins home...na tuanze sisi wenyewe kuonyesha kwamba mambo haya yanaweza kubadilishwa na kutendewa kazi ya kuonekana kwa macho...lets go substantial!
Jana (9/12/2010-Uhuru wa Tanganyika) wana-JF kama 5 wa hapa Arusha, tukiwa na m-JF mgeni toka Dar tulikutana mahali kwaajili ya kufahamiana na kubadilishana mawazo, tukagundua kwamba ni jambo jema sana kukaa pamoja na kuongea, na hatimaye tukaona umuhimu wa kufanya kitu cha kirafiki.
Tuliazimia kuwa tu'organize safari ya kutembelea mbuga yoyote ya wanyama iliyoko pande za huku kama ambavyo tutakubaliana, kabla ya Krismas, yaani kati ya tarehe 15-23/12/2010...
Tumegundua kuwa Arusha kuna members wengi sana(huenda kuliko Dar:grouphug🙂...!
Kwa members wote mtakaokuwa interested, tafadhali aidha onyesheni kwenye bandiko hili, au nitumieni PM, ili pamoja na mengine tufanye kikao cha awali cha logistics.
NB:
Members wa nchi nzima mtakaokuwa Arusha/Moshi kwaajili ya X-MAS au LIKIZO au vyovyote mnakaribishwa sana ili tuungane pamoja!
Ngongo.. Rutashubanyuma, na wengineo, tunahitaji sana inputs zenu!
UPDATE 1:
Mkuu Maxence Melo atahudhuria kwenye hii safari, na ameomba kuwa na maongezi na members wa Arusha, na hata kujibu maswali mbalimbali kuhusu Jf na mengineyo.
Tarehe imebadilishwa(kwa convinience ya Melo na wanaJF wengine toka Dar, imekuwa 27/12/2010, badala ya 23/12.