Mwanakijiji,
Je inawezekana CCM wanajivunia kitu ambacho sisi tunakataa kuamini au kukikubali?
Katika kila kata, pamoja na malalamiko kuwa kuna shida, CCM bado wanajihakikishia ushindi wa Asilimia si chini ya 60 (60%). Je ina maan akuwa hawa 60% wameridhika na hali walizonazo pamoja na kulalamika na wako tayari kuendelea kuipa CCM hatamu?
Je ni kipi na wapi tunapokosea tunapopigana vita dhidi ya Umasikini, Ujinga na Maradhi na hata tukiongeza Ufisadi katika safari ya kujitegemea na kujiletea maisha bora, ikiwa 60% wanaridhika na uongozi ulioko ingawa bado wanalalamika kuwa hawapati mahitaji ya muhimu na lazima?
Ni kitu gani ambacho kinamfanya Mtanzania huyu (60%) ashindwe kubadilisha mawazo na hata kugoma kuendelea kupigia kura chama na Serikali ile ile ambayo inashindwa kuboresha maisha yake?
Jee ndivyo tulivyo?
Kwa nini basi nasi tuendelee kuburuzwa na hawa 60% walioridhika na Umasikini na Ufisadi?