JF Exclusive: Ka-Nzi kwenye kikao cha kampeni ya CCM, Busanda!

JF Exclusive: Ka-Nzi kwenye kikao cha kampeni ya CCM, Busanda!

Mwanakijiji,

Je inawezekana CCM wanajivunia kitu ambacho sisi tunakataa kuamini au kukikubali?

Katika kila kata, pamoja na malalamiko kuwa kuna shida, CCM bado wanajihakikishia ushindi wa Asilimia si chini ya 60 (60%). Je ina maan akuwa hawa 60% wameridhika na hali walizonazo pamoja na kulalamika na wako tayari kuendelea kuipa CCM hatamu?

Je ni kipi na wapi tunapokosea tunapopigana vita dhidi ya Umasikini, Ujinga na Maradhi na hata tukiongeza Ufisadi katika safari ya kujitegemea na kujiletea maisha bora, ikiwa 60% wanaridhika na uongozi ulioko ingawa bado wanalalamika kuwa hawapati mahitaji ya muhimu na lazima?

Ni kitu gani ambacho kinamfanya Mtanzania huyu (60%) ashindwe kubadilisha mawazo na hata kugoma kuendelea kupigia kura chama na Serikali ile ile ambayo inashindwa kuboresha maisha yake?

Jee ndivyo tulivyo?

Kwa nini basi nasi tuendelee kuburuzwa na hawa 60% walioridhika na Umasikini na Ufisadi?
Rev umeuliza swali la msingi kabisa(red) kwetu sisi 40%. Ni kweli tukubali yaishe tuu? Kwa vile hao walioridhika ndio wengi tunyamaze?
 
Ripoti ya kawaida tu na ni ni sawa na zile ambazo hutolewa na taasisi moja chuo kikuu cha dar es salaam.

Hivi ukijumlisha kura za CHADEMA,CUF na UDP hauwezi kuishinda CCM?wameamua kutengana na utengano ni dhaifu.

At the end CCM itashinda tu!
 
Ripoti ya kawaida tu na ni ni sawa na zile ambazo hutolewa na taasisi moja chuo kikuu cha dar es salaam.

Hivi ukijumlisha kura za CHADEMA,CUF na UDP hauwezi kuishinda CCM?wameamua kutengana na utengano ni dhaifu.

At the end CCM itashinda tu!
I biliv ktk unity ya kisera na si unity ya kivyama.
Nadhani dawa si kuitoa sisiemu kisha ndo mambo yetu yatakuwa sawa. bali ni kuchagua chama chenye sera bora zinazotekelezeka na si kuchagua muungano wa vyama. Hamjajifunza Kenya na sasa Zimbabwe wakuu???
Ni budi tuwe makini sana na hizi sera za kuungana kivyama maana isije ikawa ndo sera ya sisiemu ya kuwagonganisha vichwa wapinzani ili iendelee kutawala.... Bado sijaiamini CUF kama kweli ina nia ya kuwakomboa wananchi wake maana sasa wana wabunge na uwakilishi mkoa mzima wa pemba lakini bado wanapiga porojo badala ya kuchechemiza maendeleo ili kuonesha utofauti..... Nipo sooooo ceptical kwa hilo

Tuongelee sera na si vyama
 
Utaona wanaainisha matatezo kadha wa kadha lakini kila mmoja anafikia hitimisho kuwa watashinda kwa zaidi ya asilimia 60.. msingi wa hitimisho hilo ni nini?
kaazi kwerikweri,yaani unataja matatizooooooooo mwisho una rule out ushindi,hivi hawa wamesoma kweli kama ningekua mwalimu na nikatakiwa nisahihishe kwa kutoa maksi hizo minutes wangeambulia 2/100%.ama ningewapa supplimentary.
 
Hata Tarime kabla ya uchaguzi Tambwe Hiza alikuwa akijigamba kuwa watashinda kwa ushindi wa zaidi ya asilimia 60. Hii inahalalisha kuwepo kwao huko kwenye kampeni, vinginevyo nani atawapa posho? Ndani ya roho zao wana takwimu tofauti kabisa na hizi 60%!
 
one thing we must appreciate...ni kuwa atleast CCM wanaonyesha wana muelekeo fulani wa kuchambua matatizo na nini kifanyike.....hilo tu pekee ni hatua pekee ya kusolve tataizo na hatimaye wanaweza hata kutathmini na kujua %ges za ushindi

Hivi ni nani asiyejua matatizo ya watanzania?, matatizo yanajichambua yenyewe hasa kama mtu ambaye hunufaiki na ufisadi utakuwa unayajua tu. CCM hawana jipya hapa haya ni mambo yanayoishia kwenye vikao vya blah blah blah watu wanasaini karatasi ya mahudhurio na kunyoosha mkono wanachukua posho, kila mtu anakunguta makalio na kuondoka, mwisho wa shughuli. Huwezi kusolve matatizo kwenye vikao vya kampeni, matatizo yanakuwa solved na watu wenye utashi na moyo wa kizalendo sio wa kibinafsi kama walivyo majority ya wanaCCM.

Hizo %ge za ushindi ni nothing basi wishes, nakumbuka wakati nipo UDSM mtu ulikuwa unapiga hesabu za marks za kuclear kwamba test ijayo nikipata 60% tu nimeclear, ukitia timu unaondoka na 20% unasema bado test moja hiyo lazima nipate 40% mwisho wa siku unajikuta una supp. Njia pekee ya kuclear ni kusoma sana kabla ya mtihani na kwa CCM ni kutekeleza yale iliyoyaahidi kwenye chaguzi zilizopita sio kusubiri uchaguzi huu then unatoa ahadi mpya hapo ni lazima ukamatwe tu,

Watanzania si mabwege tene-Mwakyembe
 
Acha uvivu wewe kakitu ka kusoma dak 2 unapeleka kesho!
Nikimnukuu Dr. Mwakyembe hapa watanirushia mawe.
Lakini ndo bongo ilivyo hata kitu cha kuanguka sign cha robo ukurasa utapigwa kalenda mpaka ujuuute
 
Hapo wakuu naona hicho kikao kinatuambia jambo. Kwanini waseme wanayajua tayari matokeo wakati tukio lenyewe bado?

Pili ni utaratibu gani huu? Nadhani hapa Vyama vingine vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi huu wana haki ya kudoubt na kupinga ushiriki wa CCM katika uchaguzi huu kwa kuwa inaonesha tayari wanajua matokeo, kitu ambacho sidhani kama ni sahihi in any way?

Mkuu Mpandafarasi, ripoti hiyo ya ndani (CP) inatoa tathmini za hali halisi ya mwenendo wa kampeni (kama wao wanavyouona) katika Jimbo la Busanda hadi kufikia tarehe iliyotajwa.

Matarajio yanayobainishwa si matokeo halisi, bali ni matarajio tu. Matokeo hayo yataendelea kubadilika kadiri siku zinavyokwenda (kutegemea ufanisi wa mikakati yao). Reports kama hizi hutoa changamoto kwa team ya kampeni kuongeza juhudi ili kuhakikisha ushindi mkubwa zaidi.

Kwahiyo si kweli kuwa tathmini ya matokeo hayo yaliyobainishwa na ripoti ndio ukweli wa matokeo halisi ya uchaguzi.

Pili, ni kawaida kwa taasisi, chama, kampuni na hata mtu binafsi kuji-evaluate hasa unapokuwa na malengo ya kutimiza lengo fulani. Hakuna haja ya chama chochote ku-doubt takwimu hizi za CCM huko Busanda. Vyama vyote ni lazima viweze kupima matokeo ya jitihada zake na kuweka mikakati ya kufanikiwa zaidi katika ushindani ulio mbele yao.

Hivyo, report hii ni sahihi kwa mtazamo wao, na haivunji sheria zozote. Dunia nzima kuna tathmini za namna hii zinazotokana na research mbalimbali zinazofanywa na wahusika, au wadau wengine.


Mkuu, nimeshangazwa pia na hesabu hizi za kura, [kama kura zingepigwa tarehe 12/05/2009, CCM ingepata 61.5%] Hawa watu wako serious au? Huenda wanajua namna tofauti ya nguvu ya kura yenyewe.

Mkuu Migafilimbi, usiangaishwe sana na takwimu hizo za 12 May 2009. Ukipata report mpya ya leo, takwimu hizo ni dhahiri zitakuwa tofauti kwa kiasi kikubwa kutokana na maendeleo yanayoweza kuwa yamejitokeza baada ya kutimiza/kutokutimiza mikakati waliojiwekea.

Ni kweli kuwa nguvu ya kura ndio inayoelezewa na takwimu zote zilizopo kwenye hiyo report. Kumbuka, uchaguzi ni kura moja moja.

Kinachotakiwa ni kuelewa mantiki ya mikakati yenyewe.

Kwa maoni yangu, mapungufu ya report nzima ni kutokuwa inaelezea mikakati halisi waliyokubaliana kuifanya ili kuongeza kura wanazotegemea kupata. Inatakiwa waweke malengo ya nini wanachotarajia kukifikia ifikapo siku watakayokutana tena.
 
Na bado biharamulo pia same rhythms watakoma mwaka huu....2010 ndio moto mkubwa zaidi
 
OLd Villager- Siwezi kudownload is there a problem with attachment?? natamani sana kuisoma...
 
Mimi nafakamia mhindi wa kuchoma hapa na maji ya kuchemshwa huku mimacho nimekodolea kijikopmyuta changu cha mapajani hapa.

Hakuna kitu cha furaha pale ambapo mtaalam wa kuumbua wengine (sisiemu) anaumbuliwa peupeeee.

Nakumbushia muungano wa kisera na si kichama pekee
 
kudos msanii, this indicates decreasing CCM majority in Bunge after 2010.
 
Msanii;459727 kijikopmyuta changu cha mapajani hapa
Mpwa kuwa makini kuweka computer mapajani karibu karibu na sehemu zile husababisha uhanithi sababu ya joto litokalo kwenye laptop watch out ndugu!
 
Mpwa kuwa makini kuweka computer mapajani karibu karibu na sehemu zile husababisha uhanithi sababu ya joto litokalo kwenye laptop watch out ndugu!
hehehehehehe
kweli mzeee umenena maana nilikuwa nakosa jibu kwa nini since last wednesday nimekuwa nadunduliza moja moja kila siku badala ya mashuti mengi kuelekea golini. Ntaacha kuiweka mapajani nashukuru kwa ushauri mkuu
 
kudos msanii, this indicates decreasing CCM majority in Bunge after 2010.
Mkuu Jafar
Safari imeshaanza na sasa wanatafutana mchawi wakati wanalogana wenyewe.

Shime Vyama vya upinzani fanyeni homeworks zenu kwa usahihi mtuletee sera zinazotekelezeka ili tuwe na mchele mwingi badala ya pumba kama chaguzi zilizopita
 
Jamani, hata Senator McCain, team yake na chama chake mpaka dakika ya mwisho walikuwa wanatamba kuwa wanatarajia ushindi na hata "independent" polls zilikuwa zinakubaliana nao...
 
Rev. Kishoka,
Ikiwa hapa JF kuna asilimia 60 (hesabu ya kufikirika) hawaamini kuwa Rostam ni fisadi kwa sababu ati hakuna ushahidi.. Vipi wananchi wa Busanda wanaweza kufikiria kinyume!
Tukubali tu mkubwa yaishe.. NDIVYO TULIVYO!

Mkandara,

Nafikiri Zitto alikosea takwimu zake kwenye hotuba yake Busanda aliposema 25% wana utapiamlo na udhaifu unaowafanya washindwe kuwa na fikra bora na hivyo kuishia kufanya mambo kijingakijinga!

Hizo takwimu zinabidi zibadilike ikiwa leo CCM wanatuambia kuwa 60% ya Watanzania katika jimbo wameridhika na uongozi wa CCM na wanafurahia Lishe ya umasikini, ujinga na maradhi yanayoambatana na wao kuhujumiwa haki zao kunakofanywa na CCM!

Madela kasema kweli, fikiria kiroba cha mchanga wakati wa mvua, uzito huongezeka na pamoja na machungu ya kukibeba, mkubwa bado unakata mbuga badala ya kuktuama chini mvua ipite, au uachane nacho ambacho kinakuumiza!
 
Back
Top Bottom