Jf Hard Talk "Mwifwa"

Habari za wakati mkuu.

Nimepitia baadhi ya comments nimeona umejipambambanua kuwa wewe ni mdau wa sekta ya afya.

Naomba mtizamo wako kwa haya machache...

1. Hivi majuzi takwimu kutoka wizara ya afya kuhusu vifo zimeonesha ugonjwa wa homa ya mapafu kusababisha vifo vingi. Je, nini kifanyike kunusuru/kupunguza hili?
2. Mwamko kwenye suala la bima za afya bado ni mdogo kwa wengi wetu... Je, sera zibadilishwe hasa kwenye uchangiaji au serikali iongeze ruzuku na upatikanaji wa bima uwe nafuu?
3. Bado huduma kwa wazee na wajawazito linakuwa tatizo kwa jamii zetu.... Bima ya afya waliimplement huduma ya dirisha la wazee, sjui hii imeishia wapi. Tunakosea wapi?

Naomba niishie hapa kwa sasa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukikutana na Rais JPM utamwambia nini?
Uongozi ni hekima, busara na upendo kwa wote anaowaongoza.
Unajiskiaje wanafunzi wanaochaguliwa Muhas toka mwaka 2015 kukosa mikopo kwa wingi sana?

Najisikia vibaya sana.
Hili jambo serikali inatakiwa iliangalie kwa umakini sana.

Kusoma kozi za Afya hasa kwa MUHAS bila kuwa na mkopo/boom/au mfadhili mwingine(halafu ujigharamie mwenyewe hasa kwa mwananchi wa kawaida mwenye kipata kidogo na sio tajiri) ni hatari sana.

Mimi nilikuwa na mkopo asilimia zote lakini shule ilinipeleka puta sana(japo tunatofautiana kiakili) hadi nikasahau kula bata kama jinsi nilivyotegemea[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Japo hiyo ilikuwa ni mbinu yangu binafsi.

Mfumo wa elimu bado haujakaa sawa maana ndoto za watu zinakuwa haziko stable kuanzia mwanzo, zinakuwa zinabadilika badilika kwa kila stage tunayopita. Jambo ambalo sio zuri.

Mfumo wetu endapo ukiwa mzuri, mtu utaweza kupambana na ndoto yako toka mwanzo hadi mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…