Jf Hard Talk "Mwifwa"

Jf Hard Talk "Mwifwa"

Kuna story gani nyuma ya hiyo avatar? mwifwa wa jf ni yule yule wa *********?
Avatar nilitafutiwa na mdada mmoja wa humu JF(naomba nisimtaje)

Sijui maana yake, mimi naona tu ni picha ya kawaida ila jinsi anavyoonekana kuwa serious ndio na mimi huwa niko serious hivyo hivyo(kwa mtu ninayefahamiana ni full kuchangamka na kutabasamu isipokuwa kwa ambaye sijazoeana wala kufahamiana naye)
 
Uongozi ni hekima, busara na upendo kwa wote anaowaongoza.

Najisikia vibaya sana.
Hili jambo serikali inatakiwa iliangalie kwa umakini sana.

Kusoma kozi za Afya hasa kwa MUHAS bila kuwa na mkopo/boom/au mfadhili mwingine(halafu ujigharamie mwenyewe hasa kwa mwananchi wa kawaida mwenye kipata kidogo na sio tajiri) ni hatari sana.

Mimi nilikuwa na mkopo asilimia zote lakini shule ilinipeleka puta sana(japo tunatofautiana kiakili) hadi nikasahau kula bata kama jinsi nilivyotegemea[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Nmekubali mkuu_ but kuna waziri Wa mikopo muhas alipotea mwaka 2015 jee alipatikana na kwanini alipotea
 
1. Ukiwa kama mdau wa afya unalichukuliaje suala zima la Utoaji mimba kwa ujumla wake
Utoaji mimba sio mzuri kiafya, una madhara ikiwemo kuharibu kizazi.

Tujitahidi kuepuka sababu za kupelekea mimba zisizotarajiwa ili kuzuia mimba
2. Je, umewahi kushiriki kwa namna yoyote ile katika utoaji mimba.
Hapana
3. Unaishauri nini serikali katika kuruhusu utoaji mimba.

Iweke sheria za kusaidia kuzuia kupatikana kwa mimba kiholela.

Na kama mtu atapata mimba kwa kuteleza(japo hamnaga kuteleza kwe nye hili jambo) apatiwe elimu ya madhara ya kutoa mimba(serikali inatakiwa ielimishe jamii madhara ya utoaji mimba na jamii iiunge mkono serikali kuhusu hili jambo kwa kutekeleza maazimio yake)
 
Habari za wakati mkuu.

Nimepitia baadhi ya comments nimeona umejipambambanua kuwa wewe ni mdau wa sekta ya afya.

Naomba mtizamo wako kwa haya machache...

1. Hivi majuzi takwimu kutoka wizara ya afya kuhusu vifo zimeonesha ugonjwa wa homa ya mapafu kusababisha vifo vingi. Je, nini kifanyike kunusuru/kupunguza hili?
Tahadhari kabla ya hatari muhimu sana.

Jamii ielimishwe kuhusu ugonjwa huu. Jinsi unavyoambukizwa, dalili zake na namna ya kujikinga mwenyewe kabla ya kwenda hospital.

Huduma za afya ziboreshwe, ili huu ugonjwa uweze kutibiwa sehemu nyingi(kwenye vituo vingi vya afya)
2. Mwamko kwenye suala la bima za afya bado ni mdogo kwa wengi wetu... Je, sera zibadilishwe hasa kwenye uchangiaji au serikali iongeze ruzuku na upatikanaji wa bima uwe nafuu?
Sera ya uchangiaji ibadilishwe ili watu wengi waweza kuchangia/kujiunga hata wale wenye vipato vya chini.

Serikali ikiongeza ruzuku kwenye Bima ndio itafanya sera ya uchangiaji iweze kutekelezwa vizuri.
3. Bado huduma kwa wazee na wajawazito linakuwa tatizo kwa jamii zetu.... Bima ya afya waliimplement huduma ya dirisha la wazee, sjui hii imeishia wapi. Tunakosea wapi?
Kuna kupanga na kutekeleza.

Huenda utekelezaji umekuwa mbaya(umefeli).

Utekelezaji ukiwa mzuri kila jambo litafanikiwa kwa kiasi chake
Naomba niishie hapa kwa sasa...
Poa
 
Tahadhari kabla ya hatari muhimu sana.

Jamii ielimishwe kuhusu ugonjwa huu. Jinsi unavyoambukizwa, dalili zake na namna ya kujikinga mwenyewe kabla ya kwenda hospital.

Huduma za afya ziboreshwe, ili huu ugonjwa uweze kutibiwa sehemu nyingi(kwenye vituo vingi vya afya)Sera ya uchangiaji ibadilishwe ili watu wengi waweza kuchangia/kujiunga hata wale wenye vipato vya chini.

Serikali ikiongeza ruzuku kwenye Bima ndio itafanya sera ya uchangiaji iweze kutekelezwa vizuri.
3. Bado huduma kwa wazee na wajawazito linakuwa tatizo kwa jamii zetu.... Bima ya afya waliimplement huduma ya dirisha la wazee, sjui hii imeishia wapi. Tunakosea wapi? [/quote]Kuna kupanga na kutekeleza.

Huenda utekelezaji umekuwa mbaya(umefeli).

Utekelezaji ukiwa mzuri kila jambo litafanikiwa kwa kiasi chake
Poa[/QUOTE]Barikiwa sana mkuu.... At least I got something.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom