JF Hatd Talk "Malcom Lumumba

JF Hatd Talk "Malcom Lumumba

Malcolm you're, with no doubt a scholar.
I hope Tz inatendea haki huu ujuzi wako.

While on this..
Unaonaje Suala la Dual Citizenship, the way Tz inalichukulia na kama unashauri.
Najua kuna vijana wengi wa mfano wako, ambao ni brainiac, talented, charismatic and patriotic, lakini wanapata nafasi nzuri zaidi kimaendeleo nje ya nchi. Na wanapoamua kutumia hizo nafasi wanajifunga, na kupoteza Haki za Uraia wa Tanzania.
Personally, naona kama ni blocks mtu anawekewa ambazo zinamzuia kutumia their full potential, especially kwa underdeveloped country ambayo kwa namna moja ama nyingine ingeweza kutumia ujuzi na maarifa yao, bila vipingamizi.
 
Mkuu Malcom Lumumba heshima kwako.
Mimi Nina maswali kadhaa yanayohusu personal development.
Q1. Unaweza kutupa kwa ufupi ratiba yako ya siku nzima.

Q2. Nipo kwenye taaluma inayonihitaji kuwa vizuri kwenye kuandika, hasa kwa lugha ya kigeni.
Safari yako ya kuwa mwandishi mzuri wa kitaaluma ilianzaje? Na unajirate vipi kwenye score ya 1-10 kwenye writing skills.

Q3. Naamini wewe ni diaspora( naweza kuwa wring), je mtu akikufuata na kukuomba ushauri wa ni vitu gani akazanie kama anataka kuexpand fishing net yake nje ya mipaka yetu, ni vitu gani utashauri.

Asante, nilichelewa kuona hii intavyuu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu Malcom Lumumba swali langu iko hivi;Sekta ya madini hapa Nyumbani Tanzania imeonekana kwa na Changamoto nyingi sana ambapo ilipelekea wizara husika pamoja na Mh Rais kufanya mkutano na wadau pamoja na wafanyabiashara mbalimbali wa madini,je unadhani ni kwa kiwango gani hiki kikao kilichofanyika kinaweza kutatua hizo changamoto zinazosemwa kila siku?,pili Mh Rais alitoa agiza la kuanzishwa kwa vituo vya kuuzia madini je unadhani kwamba hi itasaidiaje serikali?

Sent from Gamboshi air line
 
Mkuu tutoke kidogo mpaka Africa mashariki ad beyond.

Iangalie Rwada. Leo inaonekana kuwa ni ya kupigiwa mfano Africa nzima ilihali vyanzo vyake vya mapato ni questionable. Je imefika wakati na sisi wa Tz kunufaika na migogoro ya majirani zetu kwa kufanya looting kama Kagame ili kupata maedeleo kwa kiasi fulani ?

Hili la Paul Kagame na Rwanda sitaliongelea sana, ila ninachoweza kusema ni kwamba Tanzania hatuhitaji kwenda nje ya mipaka yetu kupora mali za watu: Nisema tu kwamba haijawahi kuwa ni utamaduni wa kitanzania na sera yetu ya mambo ya nje kwenda kupora mali za watu nje ya mipaka wakati sisi tuna kila aina ya utajiri. Tuna kila aina ya utajiri ndani ya nchi hii, kuanzia rasilimali watu, madini, mafuta, gesi, bandari, maziwa, mito, bahari, mbuga za wanyama, uoto wa asili na ardhi kubwa yenye rutuba. Tutaendaje nchi za watu wakati utajiri wetu hata kuutumia vizuri hatujaweza ???

Ndugu zetu wa Malawi hadi leo huwa wanajiuliza sana kwanini tung'ang'anie ziwa Nyasa/Malawi wakati sisi tuna maziwa mengi makubwa hapa nchini. Hivyo mimi nasema haina haja ya Tanzania kutolea macho mali za watu wakati sisi tunazo nyingi sana na hata hazijaanza kutumika

Lakini kubwa zaidi ni kwamba sera ya mambo ya nje ya Tanzania ya kutofungamana na upande wowote, kutetea haki za wanyonge na kuheshimu sheria za kimataifa ndiyo imetufanya tuwe ni nchi yenye amani kwenye ukanda wa maziwa makuu ambao umejaa machafuko: Tanzania

Umesema wewe ni mwanasheria kwa taaluma. Unamchukuliaje Fatuma Bensounda na ofisi yake hasa kwa kuzingatia yale ya Ivory Coast na Garbo ambaye ameachiwa sasa, Kenyatta na Ruto pia wako huru sasa to mention te few. Je huwa anatenda haki ktk uandaaji wa mashtaka au hutumika kama mbwa tu anayewatisha waafrika wenzake huku akiwaacha wengi weyemakosa kama haya wasio waafrika?

Nadhani Fatou Bensouda siyo sehemu ya tatizo, maana hata Louis Moreno Ocampo alishutumiwa hivihivi. Tatizo linaanzia wapi sasa: Kuingia kwenye Mkataba wa Roma (The Rome Treaty) ulioanzisha Mahakama ya uhalifu wa kivita (ICC) yalikuwa ni maamuzi ya nchi zenyewe za Afrika bila kushinikizwa. Mahakama ilipoanza kufanya kazi viongozi wengi wa Afrika waliifurahia sana. Kinachoshangaza sana ni kwamba katika kesi nyingi zilizopelekwa kule ICC waliozipeleka ni waafrika wenyewe na siyo muendesha mashitaka: Katika kesi nane hadi kufika mwaka 2014, kesi tani zilikuwa zimepelekwa na waafrika wenyewe na mbili ofisi ya muendesha mashitaka, huku moja ikipelekwa na Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Mataifa.

Kesi ya Uhuru Kenyatta na Rutto hazikupelekwa na Ocampo wala Bensouda, bali Wakenya wenyewe. Hati ya kukamatwa ya Joseph Konyi ilitengenezwa baada ya serikali ya Raisi Museveni kuandika barua kwa ofisi ya muendesha mashitaka wa wakati huo bwana Louis Moreno Ocampo, Kesi ya Generel Thomas Lubanga Dyilo ilipelekwa ICC na Serikali ya Congo DRC. Sasa hapa utasemaje wanaonewa wakati wenyewe ndiyo waliyataka ????

Upande wa pili, Ofisi ya mwendesha mashitaka huwa haijiamulii tu kupeleka kesi dhidi ya mtu: Mahakama ya ICC hufanya kazi pale tu ambapo mahakama za ndani ya nchi wanachama zimeonyesha kushindwa kuendesha kesi za jinai kwasababu mbalimbali. Hii kisheria tunaita The Complementarity Principle: Hivyo wenye dhamana ya kusikiliza kesi zote za jinai ni mahakama za nchi husika na kama zitashindwa basi kesi hupelekwa kule ICC. Hili limesemwa kwenye Ibara ya 1 ya Mkataba wa Roma.

Lakini upande mwingine ICC nao hawapokei kila aina ya kesi tu lazima waangalie kama kesi ina uzito au lah. Hii tunaita Admissibility of the case, hapa majaji huangalia kama kweli kesi iliyoletwa ina uzito na pia kama inakidhi vigezo vya kusikilizwa na hiyo mahakama. Hivyo ukiona kesi imepokelewa na ICC ujue ni lazima imekidhi vigezo vilivyotolewa kwenye Ibara ya 5 hado 21 ya mkataba wa Roma.

Shida inakuja hapa: Waafrika wanahisi kuonewa kwasababu wanaofanya makosa na uhalifu wa kivita ni wengi sana hapa duniani lakini kwanini wakamatwe wao tu ??? Mtu kama Rodrigo Duterte wa Ufilipino aliwahi kukiri kabisa hadharani kwamba ameua maelfu ya watu na ataendelea kuwaua tu lakini kwanini hakamatwi mpaka leo ??? Au ule uhalifu ambao unatokea nchi Afghanistani kwanini haufanyiwi uchunguzi wakati Afghanistani ni nchi mwanachama wa mkataba wa Roma ??? Kwanini Marekani izuie wanajeshi wake kuchunguzwa ilhali anapenda kuona waafrika wakichunguzwa ???

Haya ndiyo malalamiko ya Waafrika kwamba sheria ikate kotekote, lakini hili la kusema wanaonewa mimi nalikataa kwasababu wote waliowahi kupelekwa ICC kwa namna moja au nyingine walikuwa ni sehemu ya machafuko nchini kwao.

Somaliland akipata uanachama Afrika mashariki tutegemee nini?
Kama tukiwaruhusu waingie kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki basi kaa ukijua kwamba tutarithi mafanikio yao na matatizo yao pia. Sasa kama matatizo yao ni mengi kuliko mafanikio lazima tutakwama tu sehemu na sehemu: Hili liliwakuta Umoja wa Ulaya baada ya kuwaruhusu Uingereza , Ireland na Dernmark mwaka 1973: Matatizo yote ya Uingereza, Ireland na Dernmark yalibebeshwa kwenye jumuiya. Umoja wa Ulaya hadi leo umejikuta unatatua matatizo ya nchi ambazo zimekumbwa na majanga kama vile Uhispania na Ugiriki. Hivyo kama na sisi tutawaruhusu, basi tujiandae tu.

Pia naomba busara yako kuhusu Economic Freedom Fighting ( EFF) ya Julius Malema: Jana wamefanya manifesto Launch huku wakipigaia Sera ya kuteka ardhi bila malipo kwa Boers. Je atafanikiwa? Atachukua nchi? Watamwacha salama? Kuna la kuigwa na upinzani wa kwetu hapa?

Sera ya kuchukua ardhi siyo ya EFF tu bali hata ANC nao wanakubaliana nayo: Kuhusu EFF kusika nchi nadhani nisema tu bado ni chama kidogo ambacho kinahitaji kukomaa sana na kuwa na mizizi mikubwa kabla ya kushika nchi yenye uchumi mkubwa na siasa ngumu kama Afrika kusini.
 
While on this..
Unaonaje Suala la Dual Citizenship, the way Tz inalichukulia na kama unashauri.

Mimi naunga mkono Dual Citizenship: Mtu akienda kutafuta maisha nje ya mipaka ya nchi yake haimundolei haki ya kuitwa mtanzania. Upande wa pili ni ule wa kwenye rasimu ya Mzee Warioba kwamba hata kama nchi haitambui Uraia pacha basi, wale wazawa waliouchukua uraia wa nchi nyingine ni lazima wapewe heshima ya tofauti (Special Treatment) wanaporudi Tanzania: Waruhusiwe kumilika ardhi, Kuingia nchini bila vikwazo na hata kuwekeza kama watanzania.

Jiulize kama siku za mbeleni Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa na pasi moja ya kusafiria na mipaka ikafunguliwa, unadhani kutakuwa na haja tena ya kuzuia swala la Uraia pacha ??? Kama wakenya na waganda ambao siyo raia waliozaliwa Tanzania watakuwa wanaruhusiwa kuingia Tanzania na kuishi bila vikwazo: siyo vyema zaidi kama tukiruhusu wazawa wenye asili ya kitanzania nao kuingia nchini kwao kwa shughuli za kiuchumi bila vikwazo vyovyote vile ???

Nadhani ifike mahali tubadilike tu: Maana siku zijazo hii dhana ya Uraia haitakuwa na nguvu sana kwasababu mipaka itafunguliwa na wanajumuiya wa Afrika Mashariki wataruhusiwa kufanya shughuli za kiuchumi ndani ya nchi wanachama. Sasa hapa unadhani kuzuia uraia pacha kutakuwa na umaana wowote ule ??? HAPANA SIDHANI.
 
Mkuu Malcom Lumumba heshima kwako.
Mimi Nina maswali kadhaa yanayohusu personal development.
Q1. Unaweza kutupa kwa ufupi ratiba yako ya siku nzima

Sent from my iPhone using JamiiForums
Ratiba yangu inabana sana mkuu, naamka asubuhi saa kumi na moja na kulala saa sita, saba au nane. Lakini nikiamka lazima niangalie simu yangu au kompyuta kama kuna ujumbe wowote muhimu wa kujibu au kuufanyia kazi. Kabla ya kazi kuanza huwa natumia saa moja na nusu au mawili kupitia majarida mbalimbali ya habari, ukiwemo mtandao wa JF.

Kazi zikianza basi zimeanza mzee, kazi nyingi nazofanya zinahusiana na kuandika (Paper Work) na tafiti (Research). Hivyo asilimia kubwa ya ninayoyafahamu huwa nayakuta kwenye kazi nazofanya. Sasa kama nimewahi kutoka kazini basi lazima nikimbie kilomita zangu kadhaa halafu nikirudi nafanya mazungumzo na familia. Wanapoenda kulala mimi napitia JF kidogo halafu, narudi zangu mezani kufanya kazi hadi saa saba au sita.

Nipo kwenye taaluma inayonihitaji kuwa vizuri kwenye kuandika, hasa kwa lugha ya kigeni.
Safari yako ya kuwa mwandishi mzuri wa kitaaluma ilianzaje? Na unajirate vipi kwenye score ya 1-10 kwenye writing skills.
Kujijenga katika kuandika huwa haiji ndani ya usiku mmoja tu, huwa inachukua muda mrefu sana wa kujifunza na kujiongeza. Binafsi kuna kipindi nilikuwa naandika sana kwa lugha za kigeni, lakini nilichojifunza ni kwamba ili uweze kuandika ni lazima uwe msomaji na mfuatiliaji mzuri wa vitu. Fuatilia vitu vya taaluma yako lakini pia fuatilia na mengineyo ya muhimu. Ukiwa msomaji mzuri basi huwezi kukosa kitu cha kuandika hata siku moja.

Mkuu wangu, kuhusu kujirate katika uandishi basi nadhani niwaachie waandishi wengine walifanye.........
 
Hivi ni kwa namna gani elimu hii tunayo isoma mashuleni mpaka vyuoni inaweza kumfanya kijana au mwanafunzi husika kuwa na tabia njema au maadili ?
Shule na Chuo humpa mtu maadili ya kiraia (Civic Discipline), Maadilia ya Kisheria (Legal Discipline) na Maadili ya kifedha na kiuchumi (Financial Discipline) na Maadili ya tamaduni za nchi (General Cultural Discipline). Haya maadili ni muhimu sana lakini hayawezi kumjengea mtu tabia njema moja kwa moja: Sehemu kubwa ya tabia njema hasahasa ile inayokufundisha kuhusu maadili ya kuishi na jamii inayokuzunguka ambayoo tunaita Elimu Dunia mtu hujifunza nyumbani au kwenye dini yake husika. Hivyo Shule na Chuo inabidi viende sambamba na Elimu Dunai ambayo inaipatia nyumbani au kwenye dini. Lazima kuwepo na uwiano mzuri baina ya hivi vitu ndiyo mtu huwa mwadilifu mwenye tabia njema.
 
Hili la Paul Kagame na Rwanda sitaliongelea sana, ila ninachoweza kusema ni kwamba Tanzania hatuhitaji kwenda nje ya mipaka yetu kupora mali za watu: Nisema tu kwamba haijawahi kuwa ni utamaduni wa kitanzania na sera yetu ya mambo ya nje kwenda kupora mali za watu nje ya mipaka wakati sisi tuna kila aina ya utajiri. Tuna kila aina ya utajiri ndani ya nchi hii, kuanzia rasilimali watu, madini, mafuta, gesi, bandari, maziwa, mito, bahari, mbuga za wanyama, uoto wa asili na ardhi kubwa yenye rutuba. Tutaendaje nchi za watu wakati utajiri wetu hata kuutumia vizuri hatujaweza ???

Ndugu zetu wa Malawi hadi leo huwa wanajiuliza sana kwanini tung'ang'anie ziwa Nyasa/Malawi wakati sisi tuna maziwa mengi makubwa hapa nchini. Hivyo mimi nasema haina haja ya Tanzania kutolea macho mali za watu wakati sisi tunazo nyingi sana na hata hazijaanza kutumika

Lakini kubwa zaidi ni kwamba sera ya mambo ya nje ya Tanzania ya kutofungamana na upande wowote, kutetea haki za wanyonge na kuheshimu sheria za kimataifa ndiyo imetufanya tuwe ni nchi yenye amani kwenye ukanda wa maziwa makuu ambao umejaa machafuko: Tanzania

Nadhani Fatou Bensouda siyo sehemu ya tatizo, maana hata Louis Moreno Ocampo alishutumiwa hivihivi. Tatizo linaanzia wapi sasa: Kuingia kwenye Mkataba wa Roma (The Rome Treaty) ulioanzisha Mahakama ya uhalifu wa kivita (ICC) yalikuwa ni maamuzi ya nchi zenyewe za Afrika bila kushinikizwa. Mahakama ilipoanza kufanya kazi viongozi wengi wa Afrika waliifurahia sana. Kinachoshangaza sana ni kwamba katika kesi nyingi zilizopelekwa kule ICC waliozipeleka ni waafrika wenyewe na siyo muendesha mashitaka: Katika kesi nane hadi kufika mwaka 2014, kesi tani zilikuwa zimepelekwa na waafrika wenyewe na mbili ofisi ya muendesha mashitaka, huku moja ikipelekwa na Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Mataifa.

Kesi ya Uhuru Kenyatta na Rutto hazikupelekwa na Ocampo wala Bensouda, bali Wakenya wenyewe. Hati ya kukamatwa ya Joseph Konyi ilitengenezwa baada ya serikali ya Raisi Museveni kuandika barua kwa ofisi ya muendesha mashitaka wa wakati huo bwana Louis Moreno Ocampo, Kesi ya Generel Thomas Lubanga Dyilo ilipelekwa ICC na Serikali ya Congo DRC. Sasa hapa utasemaje wanaonewa wakati wenyewe ndiyo waliyataka ????

Upande wa pili, Ofisi ya mwendesha mashitaka huwa haijiamulii tu kupeleka kesi dhidi ya mtu: Mahakama ya ICC hufanya kazi pale tu ambapo mahakama za ndani ya nchi wanachama zimeonyesha kushindwa kuendesha kesi za jinai kwasababu mbalimbali. Hii kisheria tunaita The Complementarity Principle: Hivyo wenye dhamana ya kusikiliza kesi zote za jinai ni mahakama za nchi husika na kama zitashindwa basi kesi hupelekwa kule ICC. Hili limesemwa kwenye Ibara ya 1 ya Mkataba wa Roma.

Lakini upande mwingine ICC nao hawapokei kila aina ya kesi tu lazima waangalie kama kesi ina uzito au lah. Hii tunaita Admissibility of the case, hapa majaji huangalia kama kweli kesi iliyoletwa ina uzito na pia kama inakidhi vigezo vya kusikilizwa na hiyo mahakama. Hivyo ukiona kesi imepokelewa na ICC ujue ni lazima imekidhi vigezo vilivyotolewa kwenye Ibara ya 5 hado 21 ya mkataba wa Roma.

Shida inakuja hapa: Waafrika wanahisi kuonewa kwasababu wanaofanya makosa na uhalifu wa kivita ni wengi sana hapa duniani lakini kwanini wakamatwe wao tu ??? Mtu kama Rodrigo Duterte wa Ufilipino aliwahi kukiri kabisa hadharani kwamba ameua maelfu ya watu na ataendelea kuwaua tu lakini kwanini hakamatwi mpaka leo ??? Au ule uhalifu ambao unatokea nchi Afghanistani kwanini haufanyiwi uchunguzi wakati Afghanistani ni nchi mwanachama wa mkataba wa Roma ??? Kwanini Marekani izuie wanajeshi wake kuchunguzwa ilhali anapenda kuona waafrika wakichunguzwa ???

Haya ndiyo malalamiko ya Waafrika kwamba sheria ikate kotekote, lakini hili la kusema wanaonewa mimi nalikataa kwasababu wote waliowahi kupelekwa ICC kwa namna moja au nyingine walikuwa ni sehemu ya machafuko nchini kwao.

Kama tukiwaruhusu waingie kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki basi kaa ukijua kwamba tutarithi mafanikio yao na matatizo yao pia. Sasa kama matatizo yao ni mengi kuliko mafanikio lazima tutakwama tu sehemu na sehemu: Hili liliwakuta Umoja wa Ulaya baada ya kuwaruhusu Uingereza , Ireland na Dernmark mwaka 1973: Matatizo yote ya Uingereza, Ireland na Dernmark yalibebeshwa kwenye jumuiya. Umoja wa Ulaya hadi leo umejikuta unatatua matatizo ya nchi ambazo zimekumbwa na majanga kama vile Uhispania na Ugiriki. Hivyo kama na sisi tutawaruhusu, basi tujiandae tu.

Sera ya kuchukua ardhi siyo ya EFF tu bali hata ANC nao wanakubaliana nayo: Kuhusu EFF kusika nchi nadhani nisema tu bado ni chama kidogo ambacho kinahitaji kukomaa sana na kuwa na mizizi mikubwa kabla ya kushika nchi yenye uchumi mkubwa na siasa ngumu kama Afrika kusini.
Shukrani kwa majibu.

Tukibaki hapo SA. Kuna hoja kuwa Mandela was a sell out as Malema calls him kwasababu hakuapa watu kile ambacho weusi wanataka: kumiliki ardhi. Kwa wengi true patriot ni Chriss Hani. Je unaamini dhana ya Rainbow nation ya Nelson Mandela ime/ita fanikiwa?

Kukekuwa na existence of military bases na camps nyingi za mataifa yalioendelea kiviwanda ktk nchi za kiafrika. Unaliongeleaje hili mkuu. Why should or shouldn't allow that here in Tz?

Kuna mtu aliniambia espionage is the key to industrialization. Akaniambia pia China inaendelea kwa sababu wanawatu wanaiba ujuzi, siri, teknolojia etc na kupeleka kwao. Kama unaliafiki kuendelea kwa viwanda kunategemea espionage je Sera yetu ya viwanda imebebwa na espionage? Je tutatoboa?

What have you personally done for Tanzania? Have served in the any of public offices in Tz? Or work for her in overseas? Army? Or anything relating to it?

Nb
The last one ikikupendeza sawa usipojibu pia ni sawa

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Kwa Mkuu Lumumba dini za magharibi na mashariki ya kati zimeleta machafuko,chuki,na kudumaza maendeleo na kupuuza mila na desturi zetu sisi wa Afrika Mtazamo wako ni hupi kuhusu hizi za dini kuja?
Naamini suala la dini ni suala la mtu binafsi na hata sheria za nchi zinatambua hilo. Amini dini yako binafsi lakini usisababishe kero kwa mwingine. Upande wangu binafsi huwa sitenganishi dini asilia na zile za nje au za kuja, kwangu dini ni dini tu na ikitumika vibaya huweza kusababisha matatizo makubwa.
 
1. Who is favourite author for academics and for non academics ?

2. For Literature

3. Army general?

4. Republican or Democrats

5. Pinda Mizengo or Kassim Majaliwa?

6. Makonda or Aggrey Mwanri? (Reasons if any

Colors red or blue?

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Mimi naunga mkono Dual Citizenship: Mtu akienda kutafuta maisha nje ya mipaka ya nchi yake haimundolei haki ya kuitwa mtanzania. Upande wa pili ni ule wa kwenye rasimu ya Mzee Warioba kwamba hata kama nchi haitambui Uraia pacha basi, wale wazawa waliouchukua uraia wa nchi nyingine ni lazima wapewe heshima ya tofauti (Special Treatment) wanaporudi Tanzania: Waruhusiwe kumilika ardhi, Kuingia nchini bila vikwazo na hata kuwekeza kama watanzania.

Jiulize kama siku za mbeleni Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa na pasi moja ya kusafiria na mipaka ikafunguliwa, unadhani kutakuwa na haja tena ya kuzuia swala la Uraia pacha ??? Kama wakenya na waganda ambao siyo raia waliozaliwa Tanzania watakuwa wanaruhusiwa kuingia Tanzania na kuishi bila vikwazo: siyo vyema zaidi kama tukiruhusu wazawa wenye asili ya kitanzania nao kuingia nchini kwao kwa shughuli za kiuchumi bila vikwazo vyovyote vile ???

Nadhani ifike mahali tubadilike tu: Maana siku zijazo hii dhana ya Uraia haitakuwa na nguvu sana kwasababu mipaka itafunguliwa na wanajumuiya wa Afrika Mashariki wataruhusiwa kufanya shughuli za kiuchumi ndani ya nchi wanachama. Sasa hapa unadhani kuzuia uraia pacha kutakuwa na umaana wowote ule ??? HAPANA SIDHANI.

💯 I wish most of us (especially lawmakers) can see this far, and think out of the box this way..
 
Ndani ya mwaka naweza kusoma vitabu visivyopungua kumi ambavyo viko nje ya taaluma yangu.
Lakini ndani ya mwaka mzima huwa nasoma sana Machapisho yanayohusika na taaluma yangu, na hili nalifanya kila siku.
Nafanya hivi ili niweze kuandika sana, kazi yangu inanitaka kuandika na kufanya tafiti sana.
Vitabu ninavyosoma sana ni vile vya Historia, Uchumi, Siasa, Saikolojia na Sayansi ya Jumla.....
Aliyesoma kitabu cha Nadine's goldmayer July's people anieleze
 
Back
Top Bottom