Mkuu tutoke kidogo mpaka Africa mashariki ad beyond.
Iangalie Rwada. Leo inaonekana kuwa ni ya kupigiwa mfano Africa nzima ilihali vyanzo vyake vya mapato ni questionable. Je imefika wakati na sisi wa Tz kunufaika na migogoro ya majirani zetu kwa kufanya looting kama Kagame ili kupata maedeleo kwa kiasi fulani ?
Hili la Paul Kagame na Rwanda sitaliongelea sana, ila ninachoweza kusema ni kwamba Tanzania hatuhitaji kwenda nje ya mipaka yetu kupora mali za watu: Nisema tu kwamba haijawahi kuwa ni utamaduni wa kitanzania na sera yetu ya mambo ya nje kwenda kupora mali za watu nje ya mipaka wakati sisi tuna kila aina ya utajiri. Tuna kila aina ya utajiri ndani ya nchi hii, kuanzia rasilimali watu, madini, mafuta, gesi, bandari, maziwa, mito, bahari, mbuga za wanyama, uoto wa asili na ardhi kubwa yenye rutuba. Tutaendaje nchi za watu wakati utajiri wetu hata kuutumia vizuri hatujaweza ???
Ndugu zetu wa Malawi hadi leo huwa wanajiuliza sana kwanini tung'ang'anie ziwa Nyasa/Malawi wakati sisi tuna maziwa mengi makubwa hapa nchini. Hivyo mimi nasema haina haja ya Tanzania kutolea macho mali za watu wakati sisi tunazo nyingi sana na hata hazijaanza kutumika
Lakini kubwa zaidi ni kwamba sera ya mambo ya nje ya Tanzania ya kutofungamana na upande wowote, kutetea haki za wanyonge na kuheshimu sheria za kimataifa ndiyo imetufanya tuwe ni nchi yenye amani kwenye ukanda wa maziwa makuu ambao umejaa machafuko: Tanzania
Umesema wewe ni mwanasheria kwa taaluma. Unamchukuliaje Fatuma Bensounda na ofisi yake hasa kwa kuzingatia yale ya Ivory Coast na Garbo ambaye ameachiwa sasa, Kenyatta na Ruto pia wako huru sasa to mention te few. Je huwa anatenda haki ktk uandaaji wa mashtaka au hutumika kama mbwa tu anayewatisha waafrika wenzake huku akiwaacha wengi weyemakosa kama haya wasio waafrika?
Nadhani Fatou Bensouda siyo sehemu ya tatizo, maana hata Louis Moreno Ocampo alishutumiwa hivihivi. Tatizo linaanzia wapi sasa: Kuingia kwenye Mkataba wa Roma (The Rome Treaty) ulioanzisha Mahakama ya uhalifu wa kivita (ICC) yalikuwa ni maamuzi ya nchi zenyewe za Afrika bila kushinikizwa. Mahakama ilipoanza kufanya kazi viongozi wengi wa Afrika waliifurahia sana. Kinachoshangaza sana ni kwamba katika kesi nyingi zilizopelekwa kule ICC waliozipeleka ni waafrika wenyewe na siyo muendesha mashitaka: Katika kesi nane hadi kufika mwaka 2014, kesi tani zilikuwa zimepelekwa na waafrika wenyewe na mbili ofisi ya muendesha mashitaka, huku moja ikipelekwa na Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Mataifa.
Kesi ya Uhuru Kenyatta na Rutto hazikupelekwa na Ocampo wala Bensouda, bali Wakenya wenyewe. Hati ya kukamatwa ya Joseph Konyi ilitengenezwa baada ya serikali ya Raisi Museveni kuandika barua kwa ofisi ya muendesha mashitaka wa wakati huo bwana Louis Moreno Ocampo, Kesi ya Generel Thomas Lubanga Dyilo ilipelekwa ICC na Serikali ya Congo DRC. Sasa hapa utasemaje wanaonewa wakati wenyewe ndiyo waliyataka ????
Upande wa pili, Ofisi ya mwendesha mashitaka huwa haijiamulii tu kupeleka kesi dhidi ya mtu: Mahakama ya ICC hufanya kazi pale tu ambapo mahakama za ndani ya nchi wanachama zimeonyesha kushindwa kuendesha kesi za jinai kwasababu mbalimbali. Hii kisheria tunaita
The Complementarity Principle: Hivyo wenye dhamana ya kusikiliza kesi zote za jinai ni mahakama za nchi husika na kama zitashindwa basi kesi hupelekwa kule ICC. Hili limesemwa kwenye
Ibara ya 1 ya Mkataba wa Roma.
Lakini upande mwingine ICC nao hawapokei kila aina ya kesi tu lazima waangalie kama kesi ina uzito au lah. Hii tunaita
Admissibility of the case, hapa majaji huangalia kama kweli kesi iliyoletwa ina uzito na pia kama inakidhi vigezo vya kusikilizwa na hiyo mahakama. Hivyo ukiona kesi imepokelewa na ICC ujue ni lazima imekidhi vigezo vilivyotolewa kwenye I
bara ya 5 hado 21 ya mkataba wa Roma.
Shida inakuja hapa: Waafrika wanahisi kuonewa kwasababu wanaofanya makosa na uhalifu wa kivita ni wengi sana hapa duniani lakini kwanini wakamatwe wao tu ??? Mtu kama Rodrigo Duterte wa Ufilipino aliwahi kukiri kabisa hadharani kwamba ameua maelfu ya watu na ataendelea kuwaua tu lakini kwanini hakamatwi mpaka leo ??? Au ule uhalifu ambao unatokea nchi Afghanistani kwanini haufanyiwi uchunguzi wakati Afghanistani ni nchi mwanachama wa mkataba wa Roma ??? Kwanini Marekani izuie wanajeshi wake kuchunguzwa ilhali anapenda kuona waafrika wakichunguzwa ???
Haya ndiyo malalamiko ya Waafrika kwamba sheria ikate kotekote, lakini hili la kusema wanaonewa mimi nalikataa kwasababu wote waliowahi kupelekwa ICC kwa namna moja au nyingine walikuwa ni sehemu ya machafuko nchini kwao.
Somaliland akipata uanachama Afrika mashariki tutegemee nini?
Kama tukiwaruhusu waingie kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki basi kaa ukijua kwamba tutarithi mafanikio yao na matatizo yao pia. Sasa kama matatizo yao ni mengi kuliko mafanikio lazima tutakwama tu sehemu na sehemu: Hili liliwakuta Umoja wa Ulaya baada ya kuwaruhusu Uingereza , Ireland na Dernmark mwaka 1973: Matatizo yote ya Uingereza, Ireland na Dernmark yalibebeshwa kwenye jumuiya. Umoja wa Ulaya hadi leo umejikuta unatatua matatizo ya nchi ambazo zimekumbwa na majanga kama vile Uhispania na Ugiriki. Hivyo kama na sisi tutawaruhusu, basi tujiandae tu.
Pia naomba busara yako kuhusu Economic Freedom Fighting ( EFF) ya Julius Malema: Jana wamefanya manifesto Launch huku wakipigaia Sera ya kuteka ardhi bila malipo kwa Boers. Je atafanikiwa? Atachukua nchi? Watamwacha salama? Kuna la kuigwa na upinzani wa kwetu hapa?
Sera ya kuchukua ardhi siyo ya EFF tu bali hata ANC nao wanakubaliana nayo: Kuhusu EFF kusika nchi nadhani nisema tu bado ni chama kidogo ambacho kinahitaji kukomaa sana na kuwa na mizizi mikubwa kabla ya kushika nchi yenye uchumi mkubwa na siasa ngumu kama Afrika kusini.