JF Housing scheme

JF Housing scheme

serio

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2011
Posts
7,340
Reaction score
4,734
Habari wakuu,

Mimi ni member kwenye group moja huko Facebook. Members wanajadili sana mambo ya ujenzi mpaka wamefikia level za kuonana na kufanya vikao kujadili mambo mbalimbali. Hao wadau walifanya jambo moja ambalo mpaka kesho litanifurahisha. Waliji organise, wakanunua eneo/shamba la acres kama 200, huko Bagamoyo. Kila mdau alipewa acres zake kulingana na pesa aliyota. Walitafuta ma surveyor, wakapimiwa mpaka sasa watu wameshapewa documents zao zote zinazo husu umiliki wa lile eneo.

Hapo ndipo likanijia wazo la housing scheme. Humu ndani kuna wadau wengi wanauza viwanja, kwa mfano ndugu Gezaulole, Bizney, na wengine wengi. Viwanja vingine unakuta viko potential kabisa kwa bei nzuri tu. Sasa, kweli inashindijkanaje, kwa mfano,

  1. Wana JF 8 wakanunua kiwanja kimoja..mfano chenye ukubwa wa 40x60m[SUP]2 [/SUP]
  2. Wakatafuta architect aka design majengo mawili, kila jengo likiwa na floors mbili, kila floor ikawa na units mbili, na kila unit ikawa na vyumba vitatu au viwili, sitting room, kitchen, public toilet na store. (jumla ni units nane)
  3. Hao wana jf wakatafuta Qs akawapa gharama za ujenzi wa hayo majengo yao.
  4. Wakachanga pesa, wakamtafuta contractor akawafanyia ujenzi.
  5. Ujenzi ukakamilika, kila mtu akapewa hati yake (unit title) ya unit anayo imiliki.
  6. Mwana JF akahamia kwenye unit yake, akauza, au akakodisha.

Na kama hayo yote yanawezekana, definately wana JF tunaweza kuji organise, tukanunua viwanja vikumba na tukajenga nyumba za gharama nafuu, tukaishi, tukauza na tukakodisha. Na huu mradi tunaweza kuita JF HOUSING SCHEME or anyother appropriate name. In the event, inaweza kuwa biashara kubwa sana hapo baadae.

Wadau, nyie mna mawazo gani juu ya hili?

Nawasilisha.

cc Zamazamani frozen msani Realtor Kingdom_man Mchambuzi Candid Scope ZeMarcopolo na wengine woote wenye interest na REAL ESTATE.
 
Last edited by a moderator:
It's good idea for real, even hata kama sio nyumba inawezekana kuanzisha hata mradi mwingine tofauti wenye faida, watu wakaandika proposal na hata kupata mkopo kutoka taasisi za kifedha, sababu taasisi nyingi za kifedha zinapenda group of people
 
Daah, umewaza nini kiongozi... This is a very good idea. Ngoja wapembizi waje wamwage nondo zao.
 
It's good idea for real, even hata kama sio nyumba inawezekana kuanzisha hata mradi mwingine tofauti wenye faida, watu wakaandika proposal na hata kupata mkopo kutoka taasisi za kifedha, sababu taasisi nyingi za kifedha zinapenda group of people

Sure.. Hapa nimejaribu kuangalia housing needs za nchi yetu, especially Dar es salaam. Rates za kupanga nyumba nzuri ni kubwa, na ukisimama peke yako unatumia gharama kubwa kwa ajili ya ujenzi... Mimi naona kuunganiasha nguvu za kifedha au mitaji ni suluhu tosha..
 
Ni wazo zuri, lakini utekelezaji ili ufanikiwe hautakiwi kuhusisha watu wote.

Kunatakiwa kuwe na watu wawili au watatu ambao wanasimamia zoezi na kampuni ambayo itajenga. Ujenzi wa wengi haufai kufanywa kwa kutumia mafundi "wa kuokoteza" kwa sababu kutakuwa na too many irregularities na changes zinazoweza kuwa sababu ya migogoro.

Members wengine watoe equity kulingana na hesabu za gharama na wawe na fursa ya kutembelea site kuona maendeleo.

Changamoto ni kupata watu hao wawili au watatu ambao wanaaminika kumanage mamilioni ya watu...
 
wazo zuri tatizo wanajjf kwenye kukutana na kupanga ndio kila mtu atajifaanya yupo busy utafikiri anaumba roho za watu. watu walioshiriki kwenye mchakato wa JE saccoss wanaelewa namaanisha nn.
Aisee hapo kwenye saccoss sijui kilitokea nini. Nilikua mfatiliaji mzuri tu, lakini siku moja niliamka na kukuta uzi una password, then ukapotea na sikuuona tena.
 
Ni wazo zuri, lakini utekelezaji ili ufanikiwe hautakiwi kuhusisha watu wote.

Kunatakiwa kuwe na watu wawili au watatu ambao wanasimamia zoezi na kampuni ambayo itajenga. Ujenzi wa wengi haufai kufanywa kwa kutumia mafundi "wa kuokoteza" kwa sababu kutakuwa na too many irregularities na changes zinazoweza kuwa sababu ya migogoro.

Members wengine watoe equity kulingana na hesabu za gharama na wawe na fursa ya kutembelea site kuona maendeleo.

Changamoto ni kupata watu hao wawili au watatu ambao wanaaminika kumanage mamilioni ya watu...

Kweli sana kiongozi, inabidi kuwe na level kubwa ya organisation and trust. Lakini makundi mengine mbona yanaweza?
Nadhani tatizo ni kwamba, kila mtu anajiona anajua zaidi ya mwenzake, na hataki kuwaamini wenzake. Over criticism nayo inasababisha mambo yasiende vizuri kwani watu wengine wanakata tamaa mapema..
 
Cha muhimu ni good selection of participants. Sio kila mtu anafaa. Then kuwe na high level of transparency.

Lakini vyote hivyo msingi wake ni good intention. Kusiwe na mtu anayetaka kuwafanya wenzake deal.

In this idea specifically, wewe kama author of the idea unaweza kutengeneza plan kamili then kuspot and recruit watu unaoona wanafaa. Mkachagua wasimamizi/viongozi na kuanza utekelezaji.

Lakini kuna maswali ya msingi ya kujijibu kabla ya kuanza:
1. Je, lengo la ushirikiano ni nini? lengo haliwezi kuwa kupunguza gharama za ujenzi kwa sababu unit price ya nyumba mtakazojenga kwa kikundi itakuwa kubwa kuliko mtu akijenga mwenyewe. Sababu ni kwamba ujenzi wa vikundi ni lazima uheshimu taratibu zote za kisheria ambazo huongeza gharama. Taratibu zisipofuatwa ni mwanya wa migogoro.
2. Taratibu gani zitatumika kwenye maintenance of shared areas. Msijenge nyumba halafu kila mtu atake kuchimba shimo lake la takataka.
3. Repairs policy. Nyumba isije kupata ubovu halafu mwengine aone ubovu huo haustahili kurekebishwa.
4. Policy ya matumizi. Isije kutokea mmoja wenu akageuza sebule yake kuwa kilabu cha pombe.

Hizi policies ni vizuri zikiwa registered kisheria kwa sababu nyumba ni long-term property.

Advantage ya kujenga pamoja ni kuweza kuboresha miundombinu kwa umoja. Lakini in my view inafaa zaidi kushirikiana kuown eneo kubwa ambalo kila mtu atajenga kiwanja chake, kuliko kujenga ghorofa ambalo mtagawana apartments.
 
wazo zuri tatizo wanajjf kwenye kukutana na kupanga ndio kila mtu atajifaanya yupo busy utafikiri anaumba roho za watu. watu walioshiriki kwenye mchakato wa JE saccoss wanaelewa namaanisha nn.
Yaan nimecheka hadi basi, unajua tatizo watu hamuielewi hii forum, kwanza kuona tu mtu amechagua ID fake ujue kuna mengi yanafichwa na anaweza fanya chochote, pili anakuwa hata hajulikani alipo kuliko angetaja jina kamili ingekuwa aibu maana wanaomjua wangemshangaa. Hapa tunajadiliana na kuitikia au kupanga kuwekeza mahali fulani ila ungekuwa una uwezo wa kutuona wapi tunakoishi au fanyia shughuli zetu wakati huo nafikiri ungeghairi na kusema basi sijapata watu. ni wachache walio wazi kwamba kitu fulani nitakuja au sitakuja au nitashirika etc wengine wanaitikia ila wapo mbali na pia hawana nia kiivyo.
Face book na kwingine watu wameingia na majina yao na kazi zao wazi wakiwa na nia ya kuanzisha biashara au kuuza bidhaa zao zile ni biashara, kampuni wengine CV zao wanauza skills sasa jiulize lengo la watu wengi wenye IDs fake ni wachache wanaaminika walio wengi ndio waamninifu ila labda wanahofia mengine waliofanya au fanyiwa walio disclose ID zao. huu ni uzoefu mdogo ingawa mie siko FB na naweza sema hapa nimepata wshirika wakutosha, nimeuza vingi na kununua vingi so ni suala la nini unafanya na approach unayotumia.
 
hapo ndo tatizo sugu na wengine huenda wakakimbia na mahela ya watu ikawa tatizo juu ya tatizo
Ni wazo zuri, lakini utekelezaji ili ufanikiwe hautakiwi kuhusisha watu wote.

Kunatakiwa kuwe na watu wawili au watatu ambao wanasimamia zoezi na kampuni ambayo itajenga. Ujenzi wa wengi haufai kufanywa kwa kutumia mafundi "wa kuokoteza" kwa sababu kutakuwa na too many irregularities na changes zinazoweza kuwa sababu ya migogoro.

Members wengine watoe equity kulingana na hesabu za gharama na wawe na fursa ya kutembelea site kuona maendeleo.

Changamoto ni kupata watu hao wawili au watatu ambao wanaaminika kumanage mamilioni ya watu...
 
hapa mkuu umeongea vyema aiseee
ni kama umenifungua macho kweli kwa suala hili ni bora likanunuliwa eneo kubwa kila mtu akawa na eneo lake na kujenga anachotaka hapo hii ndo kitu nzuri sana

Cha muhimu ni good selection of participants. Sio kila mtu anafaa. Then kuwe na high level of transparency.

Lakini vyote hivyo msingi wake ni good intention. Kusiwe na mtu anayetaka kuwafanya wenzake deal.

In this idea specifically, wewe kama author of the idea unaweza kutengeneza plan kamili then kuspot and recruit watu unaoona wanafaa. Mkachagua wasimamizi/viongozi na kuanza utekelezaji.

Lakini kuna maswali ya msingi ya kujijibu kabla ya kuanza:
1. Je, lengo la ushirikiano ni nini? lengo haliwezi kuwa kupunguza gharama za ujenzi kwa sababu unit price ya nyumba mtakazojenga kwa kikundi itakuwa kubwa kuliko mtu akijenga mwenyewe. Sababu ni kwamba ujenzi wa vikundi ni lazima uheshimu taratibu zote za kisheria ambazo huongeza gharama. Taratibu zisipofuatwa ni mwanya wa migogoro.
2. Taratibu gani zitatumika kwenye maintenance of shared areas. Msijenge nyumba halafu kila mtu atake kuchimba shimo lake la takataka.
3. Repairs policy. Nyumba isije kupata ubovu halafu mwengine aone ubovu huo haustahili kurekebishwa.
4. Policy ya matumizi. Isije kutokea mmoja wenu akageuza sebule yake kuwa kilabu cha pombe.

Hizi policies ni vizuri zikiwa registered kisheria kwa sababu nyumba ni long-term property.

Advantage ya kujenga pamoja ni kuweza kuboresha miundombinu kwa umoja. Lakini in my view inafaa zaidi kushirikiana kuown eneo kubwa ambalo kila mtu atajenga kiwanja chake, kuliko kujenga ghorofa ambalo mtagawana apartments.
 
wazo zuri tatizo wanajjf kwenye kukutana na kupanga ndio kila mtu atajifaanya yupo busy utafikiri anaumba roho za watu. watu walioshiriki kwenye mchakato wa JE saccoss wanaelewa namaanisha nn.
Its human nature kutokuamini kama kitu fulani kinaweza fanikiwa sasa wachache wenye kuamini waendelee na idea baadae members watakuja wakiona kimetokea!
 
Issue ni watu ni rahisi kujitokeza kuuza kununua maana ni vitu vya muda papo hapo lakini ukija suala la commitment tuwe wa kweli ni ngumu mtu kuchukua mamilioni na kuwekeza na mtu hujamjua vizuri, na kujuana inachukua muda hapa tayari kuna watu tumewaamini na unaweza kuona waweza fanya nao kitu fulani. Pili wengi wetu tayari wameishajiingiza kwenye ujenzi na wanaendelea taratibu....funds. sasa kuwatoa huko waanze kingine inakua kazi. Afu kuna hizo athari za kushare apartment nafikiri tuliokaa maghorofani muda mrefu wanalijua hili: maintainance, kelele, wageni+wanyama mf paka, mbwa, parking nk vinahitaji strict policy otherwise ni majuto. Lakini wapo ambao ni vijana au hawajaanza ujenzi au wana extra capital watapatikana na ni kitu kizuuri sana. Just a matter of time
 
Cha muhimu ni good selection of participants. Sio kila mtu anafaa. Then kuwe na high level of transparency.

Lakini vyote hivyo msingi wake ni good intention. Kusiwe na mtu anayetaka kuwafanya wenzake deal.

In this idea specifically, wewe kama author of the idea unaweza kutengeneza plan kamili then kuspot and recruit watu unaoona wanafaa. Mkachagua wasimamizi/viongozi na kuanza utekelezaji.

Lakini kuna maswali ya msingi ya kujijibu kabla ya kuanza:
1. Je, lengo la ushirikiano ni nini? lengo haliwezi kuwa kupunguza gharama za ujenzi kwa sababu unit price ya nyumba mtakazojenga kwa kikundi itakuwa kubwa kuliko mtu akijenga mwenyewe. Sababu ni kwamba ujenzi wa vikundi ni lazima uheshimu taratibu zote za kisheria ambazo huongeza gharama. Taratibu zisipofuatwa ni mwanya wa migogoro.
2. Taratibu gani zitatumika kwenye maintenance of shared areas. Msijenge nyumba halafu kila mtu atake kuchimba shimo lake la takataka.
3. Repairs policy. Nyumba isije kupata ubovu halafu mwengine aone ubovu huo haustahili kurekebishwa.
4. Policy ya matumizi. Isije kutokea mmoja wenu akageuza sebule yake kuwa kilabu cha pombe.

Hizi policies ni vizuri zikiwa registered kisheria kwa sababu nyumba ni long-term property.

Advantage ya kujenga pamoja ni kuweza kuboresha miundombinu kwa umoja. Lakini in my view inafaa zaidi kushirikiana kuown eneo kubwa ambalo kila mtu atajenga kiwanja chake, kuliko kujenga ghorofa ambalo mtagawana apartments.

Asante sana bwana ZeMarcopolo , umenipa vitu ambavyo nilikua hata sijavifikilia.. Ni mambo ya muhimu sana kuyajua kabla ya kufanya makubaliano na partners...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom