JF ilivyoua huba langu

JF ilivyoua huba langu

Samaleko,

Basi bwana, miaka kadhaa nyuma nilikuwa na Id yangu xxxx, haikuwa Maarufu hata kidogo, nilikuwa napenda kumchangia kidogo kwenye Jukwaa la siasa, intelligence na international news na History.Sasa Maulid moja akaja ex shemeji yenu kunitembelea,Kwa kawaida nikiwa nyumbani napenda sana kumsikiliza Country music,basi nikawa nimewasha laptop zile miziki zinaimba,halafu tab nyingine nilifungua JF,Sasa yule bwana alivyofika Mimi napikapika akasema bwana mi natoa Hawa wababu wako,Nia abadilishe aweke miziki anayopenda yeye,Mimi Niko zangu napikapika,basi Ile anaendelea kushikashika laptop nikasikia naulizwa,
Baby una account Jamii forum?
Mi kiroho safi nikamjibu eeh mbona siku nyingi😁😁
Eeeeeh bwana nilisimangwaaa,nilisomewa risala,niliambiwa sifai kabisa,Mimi sio wife material,maana mke wa mtu hawezi kuwa member wa JF.
Basi kila mkitofautiana utakisia wewe umeshaharibika sababu ya JF🙄,ikawa JF,JF,JF sipumui,mpaka safari ikaishia njiani...

Sasa nikawa nashangaa Ina maana wadada tulio JF tuna tabia mbaya kiasi hiki🤣??eti kina kaka mkigundua wapenzi zenu ni member wa JF mtakasirika?

NB:nilihisi lazima na yeye ni member humu ila sijui ID yake,nikabadili zangu ID chaaaa..

Happy Maulid to all
Mimi huwa nikitaka kuanzisha ugomvi navizia litokee lolote.Nikiona halitokei naanza hata kuwa mkali kwa nini unaniangalia!🤔
 
Huyo haijui JF zaidi ya kusimuliwa. Angekuwa kweli anaijua basi asingekusakama ww kuitumia.

Anaisikia tu aijui vizuri na kalishwa uongo.

Huezi amini wengine wanajuaga JF ni mtandao wa siasa tu na kutafuta wapenzi.
Mmh mbona alikasirika sana😁😁😁😁?
 
Samaleko,

Basi bwana, miaka kadhaa nyuma nilikuwa na Id yangu xxxx, haikuwa Maarufu hata kidogo, nilikuwa napenda kumchangia kidogo kwenye Jukwaa la siasa, intelligence na international news na History.Sasa Maulid moja akaja ex shemeji yenu kunitembelea,Kwa kawaida nikiwa nyumbani napenda sana kumsikiliza Country music,basi nikawa nimewasha laptop zile miziki zinaimba,halafu tab nyingine nilifungua JF,Sasa yule bwana alivyofika Mimi napikapika akasema bwana mi natoa Hawa wababu wako,Nia abadilishe aweke miziki anayopenda yeye,Mimi Niko zangu napikapika,basi Ile anaendelea kushikashika laptop nikasikia naulizwa,
Baby una account Jamii forum?
Mi kiroho safi nikamjibu eeh mbona siku nyingi😁😁
Eeeeeh bwana nilisimangwaaa,nilisomewa risala,niliambiwa sifai kabisa,Mimi sio wife material,maana mke wa mtu hawezi kuwa member wa JF.
Basi kila mkitofautiana utakisia wewe umeshaharibika sababu ya JF🙄,ikawa JF,JF,JF sipumui,mpaka safari ikaishia njiani...

Sasa nikawa nashangaa Ina maana wadada tulio JF tuna tabia mbaya kiasi hiki🤣??eti kina kaka mkigundua wapenzi zenu ni member wa JF mtakasirika?

NB:nilihisi lazima na yeye ni member humu ila sijui ID yake,nikabadili zangu ID chaaaa..

Happy Maulid to all
Mtazamo wake tu labdah hataki mpate wote nondo za humu
 
Back
Top Bottom