JF ilivyoua huba langu

JF ilivyoua huba langu

Hilo halikuwa huba bali “bua”.
Basi alikuwa anawafanyia vibaya jinsia ke..so akajua yalealiyokuwa akiyatenda..basi nawe utakuwa ni wale wale woi.

Nimejaribu kuwaza kivingine au alikuwa anataka kukupiga chini muda sema hakupata sababu😁😁

Mwanadamu bhana hajawahi kuwa na utulivu jamani😆

Kuna mwamba Niko naye sasa huyu bwana ni anajielewa 95% aise na tangu nimekuwa nae nimekuwa na Amani mno siwezi lalamika 🥰

Sasa yapata wiki moja ninaanza kupata kisirani juu yake yani ninakila chokochoko za kuchimbua ugomvi🥹🥹

Nimelogwa hakika niombewe 😆😆ninajijua sipendagi mikwaruzano kwenye mahusiano kabisa
Shenzy zake kabisa!Sasa si angesema tu anazungukazunguka Nini😁😁😁
Sasa na wewe umeanza kulitafuta uachike useme umerogwa hebu jitulize,ukipendwa pendeka mamaa
 
Samaleko,

Basi bwana, miaka kadhaa nyuma nilikuwa na Id yangu xxxx, haikuwa Maarufu hata kidogo, nilikuwa napenda kumchangia kidogo kwenye Jukwaa la siasa, intelligence na international news na History.Sasa Maulid moja akaja ex shemeji yenu kunitembelea,Kwa kawaida nikiwa nyumbani napenda sana kumsikiliza Country music,basi nikawa nimewasha laptop zile miziki zinaimba,halafu tab nyingine nilifungua JF,Sasa yule bwana alivyofika Mimi napikapika akasema bwana mi natoa Hawa wababu wako,Nia abadilishe aweke miziki anayopenda yeye,Mimi Niko zangu napikapika,basi Ile anaendelea kushikashika laptop nikasikia naulizwa,
Baby una account Jamii forum?
Mi kiroho safi nikamjibu eeh mbona siku nyingi😁😁
Eeeeeh bwana nilisimangwaaa,nilisomewa risala,niliambiwa sifai kabisa,Mimi sio wife material,maana mke wa mtu hawezi kuwa member wa JF.
Basi kila mkitofautiana utakisia wewe umeshaharibika sababu ya JF🙄,ikawa JF,JF,JF sipumui,mpaka safari ikaishia njiani...

Sasa nikawa nashangaa Ina maana wadada tulio JF tuna tabia mbaya kiasi hiki🤣??eti kina kaka mkigundua wapenzi zenu ni member wa JF mtakasirika?

NB:nilihisi lazima na yeye ni member humu ila sijui ID yake,nikabadili zangu ID chaaaa..

Happy Maulid to all
Pole sana!
Kimsingi haya mambo ya social media yanataka mtu mwenye uelewa wa mambo ya kidunia;
Kuna watu wazuri sana huko kwa social media hata huku JF pamoja na kuwa lipo kundi pia la watu malimbukeni wanafikiri kutokuonekana wazi wazi ndio nafasi ya kuposti kila uchafu wanaowazia....
Nachelea kusema huyo wa kwako hakuwa na exposure ya mambo ya mitandao; Pole!!!
 
Kwahyo jamaa kaogopa pisi yake italiwa kimasihara😂😂😂😂
 
Pole sana!
Kimsingi haya mambo ya social media yanataka mtu mwenye exposure kuyaelewa
Kuna watu wazuri sana huko kwa social media kama JF pamoja na kuwa lipo kundi pia la watu malimbukeni wanafikiri kutokuonekana wazi wazi ndio nafasi ya kuposti uchafu wote....
Nachelea kusema huyo wa kwako hakuwa na exposure ya mambo ya mitandao; Pole!!!
Kwani boyfriend sio shemeji yenu😁😁😁😁? anyways atakuwa alikuwa na lake jambo ,na kukosa exposure
 
Back
Top Bottom