JF imekusaidia nini tangu uijue?

Madam vivian original

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2018
Posts
503
Reaction score
997
Wakuu habar za masiku. Mko poa, nimewamiss sna.

Twende kwenye point Je famii forom imekusaidia nn tangu uijue, ni ukweli usiopingika hakuna social network ambayo inapendwa na inayotizamwa na watu wengi kama JF.

Mm binafs kilichofanya nijiunge humu ni michango ya watu, kuna watu walikua wanaiinsipire sna, yaan hakuna kitu utagoogle ambacho JF hawajakijadili na kuna nondo za Hataree

Nikashawishika kujiunga na mpaka leo nafurahia kuwa member wa JF, ila kwasasa mambo yamebadilika sna, zaman ukitoa hoja itajibiwa vzr na kwa fact, lakin sasa hv kumekua sehemu sio salama sna maana naweza ukapewa jibu mpaka ukalia.

Nakumbuka kuna siku moja kuna member alawah kunijibu vibaya na kunitukana kwenye comment mpaka nililia, nikawa naiogopa JF nikawa naingia kwa kubip na nikiingia naogopa kuchangia mada maana wengine vifua vyetu vyepes hatujazoea tabu na maneno ya kashfa.

Kiukwel JF ilinipatia rafiki mmoja ninae mkumbuka mpaka Leo, niliwah kutoa post kuhusu KCMC na mambo ya bima ya afya, basi doctor mmoja alikoment na akanisaidia akaniconect na doctor mwenzake yupo KCMC kwa kweli nilifurah sna.

Baada ya hapo yule doctor akawa rafik angu na tukatumiana PC, akafurah kunijua namm pia nilifurah sna. Ni rafiki angu sna ila kwa sasa tumepotezana popote ulipo Dr nyak nakusalimia sna rafiki angu.

Je wewe tokea ujiunge na jf umenufaika nayo vp, uliwah kukwazika humu? au kupata furaha humu ndan mpaka ukisikia jf inafungiwa unaumia.

Karibu
 
Kwangu jf ni kisima cha maarifa sitaorodhesha maarifa hayo lkn jueni maarifa tu tena makubwa!..

Jf kwangu ni Kama Kijiji nikiamka nakutana na majirani tunasalimiana,tunapiga story,kuchekeshana,kuzinguana,kupigana mikwala.. yeah like that jamiiforum naipenda na hainikinai ndo maana nimekuwa active member kwelikweli..😅

Ila kikubwa imenisaidia kupata maarifa humu unatakiwa ujue chakubeba na chakuacha.. nawakubali member wote..😜
 
Kweli inategemea na jinsi mtu atakavyoitumia kwa upande ukitaka kupata madini unapata
 
Umenikumbusha kuna mrembo nilikua nachat nae pisi kali haswaa daah kumbe alikua mjamzito, natumaini sasa hivi mtoto ameshakua nanii popote ulipo nitafute mrembo tuyajenge,
[emoji847][emoji5]
 
Yote 9, 10 ni kuwa niliwahi comment jambo humu nikiwa natania, nilishushiwa mvua za comments za masimango zinazokarahaisha mpaka nikatamani kulia machozi..!

Cha kushangaza miongoni mwao walionisimanga nawakumbuka kama wawili ambao lazima nipatane na nondo zao kwenye baadhi ya thread, points zao zimesimama mpaka najikuta naishia ku admire na ku like tu..!

Life ain't fair walaqhi'...!😀
 
JF ni Jamii Forum. Ni Jukwaa la Jamii.

Mada za siasa, uchumi, kijamii na kisayansi zimenijenga kifikra.

Jamii Forum ni kisima Cha fikra. Imenijenga kifikra na kimawazo.

Nimeifahamu Jamii Forum mwaka 2010 wakati ninakaribia kujiunga chuo, na ni wakati ule siasa zimepamba moto JK anatafuta muhula wa pili.

Kimsingi, purukushani za kisiasa za akina Makamba Yusuf, Nappe na wengineo walinifanya kutafuta maarifa zaidi na niliyapata Jamii Forum maana katika mijadala ile, hao wanasiasa waliihusisha Jamii Forum kwamba Kuna watu wanatoa Siri za chama JamiiForum, kwa hiyo pia nikawa na kiu kujua Jamii Forum Ni kitu gani.

Humu nilikutana na watu wenye weledi kifikra Kama vile Kiranga, king kong, miss chaga, @lara1, The bold, Nifah, Everlyn salt, Kongosho, Ben Saanane (RIP), @nappe nnauye, Mshana Jr ASHA dii na wengineo ambao walichambua mambo kwa kina na kuifanya Jamii Forum iheshimike hapa Tanzania na hata nje ya mipaka.

Pongezi kwenu @jamiiforum, Mhariri, na haswa Mello, M kwa kazi nzuri ya kukutanisha Watanzania katika jukwaa moja la mijadala huru.

Kazi kubwa iliyopo Sasa ni kuilinda heshima ya Jamii Forum japo irudi ilipokuwa mwaka 2013 maana humu wachangiaji wenye ueledi na staha wanapungua sana.
 
Jf imenisaidia sana kifikra kwenye mambo mengi sana yanayoendelea kwenye jamii zetu. Kupitia mikasa na njia za busara za kutatua changamoto za kimaisha imenisaidia sana na nazidi kujifunza kila nikiingia humu.

Nikiwa stressed huwa napita na koment za memba wa humu nafurahi mno ni moja ya social network nayoikubali sana.
 
Umenikumbusha kuna mrembo nilikua nachat nae pisi kali haswaa daah kumbe alikua mjamzito, natumaini sasa hivi mtoto ameshakua nanii popote ulipo nitafute mrembo tuyajenge,
[emoji847][emoji5]

Khaaaa kumbe mkuu ni ME,siku zote najuaga KE vile unavyotupia mapishi mbalimbali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…