Sanctus,
Nimeipitia website yenu, kuna vitu nimeridhika navyo na kuna baadhi ambavyo bado nina matatizo navyo. Nitazungumzia mambo ambayo bado nina wasiwasi au dukuduku nayo.
1. Mnaposema financial empowerement, kwangu iko too general, ni lengo ambalo kinadharia linawezekana ila tukija katika practice inabidi mjaribu kuweka road map au concept map ya kitu gani hasa mnanuia kufanya.
2.Wealth creation for profesionals pia inakuwa too general, ni kwamba mnaangalia maslahi ya professionals too au focus yenu ni katika kuleta mabadiliko Tanzania ambayo yanaweza kuigwa na hatimaye kuwasaidia either wanachama wenu katika maisha ya kila siku au community ambayo naona mnakuwa mnaitaja mara kwa mara ambayo inakuwa na both wanachama na wasio wanachama?. Mnamaanisha nini hasa katika jambo hili?
3.Website yenu haijakaa ki-professional nyie kama professional manaweza kutafuta idea kutoka kwa professionals namna ya kufanya website yenu iweze kuonekana professional zaidi hii ni pamoja na kuwa na information za muhimu katika page ya kwanza ambazo zinaweza kuelezea ninyi ni akina nani na malengo yenu ni yapi. Information zingine zimefichika, kawaida mtu anafanya uamuzi wa kujiunga na chama au professional body in less than 3 minutes, kama huwezi kupata information za muhimu katika mda huo then mtakuwa mnapoteza wengi ambao wangeweza kuwa wanachama.
4.Mwaka 2050 ni mbali sana, kama mnazungumzia malengo ni vizuri kuwa na short terms na long terms strategies, strategy mliyoweka haimotivate watu kwa sababu inaashiria kwamba mnayo time ya kutosha kufanya au kufikia malengo mnayoyataka.
5.Ada ya uanachama hii ni pamoja na registration na annual fees haijawekwa wazi kuwa ni kiasi gani na inalipwa yote mara moja au installments.
6.Katiba yenu imeweka focus kubwa sana kwa graduates, pia inaruhusu members wengine ambao wanashare vision yenu, hamuoni kuwa mnavyotumia titles za elimu na nchi au vyou wanachama waliposoma mnaweza kuwa-switch off ambao wanaweza kuwa na vision kama zenu ila wakajisikia kuwa wako katika wrong network kwa sababu hawana title after their names? au kujenga matabaka kati ya wale waliosoma nje na wale waliosoma Tanzania?
Finally ningependa kukuhakikishia kuwa nitajiunga na nyie mda si mrefu, nimesave site yenu kwenye my favorites, nitanguliza shukrani zangu kwa majibu yako.
Mzalendo GM (General Manager??? LOL), nashukuru sana kwa kutenga muda wako na kuandika kwa makini sana mchango wako wa mawazo ndani ya TPN. Nimefarijika sana na napenda nikuahidi kuwa mawazo yako mazuri yatafanyiwa kazi.
Ni kweli kuna mambo yanaweza yakawa hayoko clear sana na kwa maoni ya wengi ni vema kuweka nafasi ya mabadiliko ya kikatiba.
Mfano katika Suala Zima na Financial Empowernment and Wealth Creation, tulikuwa tunaangalia ni jinsi gani ya kulifanikisha hili. Kuna matatizo ya namna tatu yaligunduliwa ambayo yanawakabili Wanataaluma kufanikiwa kipesa au kibiashara:
1. Ujasiliamali - Baadhi ya wanataaluma wengi hawana Elimu ya Ujasiliamali wa Kimaadili. Kwa hili tumeanzisha Seminar Mbalimbali na Workshops ili kuwaelimisha wanataaluma wanaopenda, wote, walio na wasio wanachama na wadau wengineo. Kuna DVD na hat PPT ambazo zinapatikana kwa wale watakaozihitaji.
2. Mitaji - Suala zima la kupata mitaji ya kibiashara lilionekana ni kikwazo hata kwa wale ambao tayari ni wajasiliamali na wana elimu ya ujasiliamali. Kwa hili tuliongea na baadhi ya Mabenki amboyo walitupa offer ya unsecured loan hadi Million 30. Pia wanataaluma wanaweza kuungana na kuchanga mitaji. Tayari kuna baadhi ya vikundi wameunda makampuni na kuchanga mitaji. Latest group wameungana kama 15 na kuchanga Millioni 30 kama mtaji wao kwa ajili ya biaashara yao. Wapo ambao wameungana na kuandika proposals nzuri na wanashughulikia kupata mikopo kupitia security ya pamoja.
3. Masoko - Katika hili kuna ambao hata kama wamefanikiwa katika 1 na 2 hapo juu lakini masoko ya huduma au bidhaa zao ni tatizo. Kwa hili TPN inakuwa kama Market Place kwa ajili ya kuwaunga mkono. Kwa hili tunaweza pia kujifunza sana kutoka kwa ndugu zetu Waasia ambao wao katika jumuiya zao km Jamatini, nk huwa wanasaidiana sana kipesa na kimasoko.
Tumeshuhudia katika Network ya TPN watu wakifahamiana na kufanya biashara. Tunao uwezo na Network kubwa kama tukii-extend katika familia zetu kwa wanaotutegemea. Si hili tu, tunaao watanzania wengi wanaoishi nje ya nchi ambao tunaweza kufanya nao biashara na kutupatia masoko ya uhakika.
Mtazamo wa kwanza wa TPN ni kuwa wanataluma wako katika nafasi nzuri ya kuanzisha maakampuni ambayo yatatoa ajira na kuchangia katika uchumi. Katika kufanya hivyo wote wanataaluma na watanzania kwa ujumla wote watafaidika.
Lakini pia katika sura ya pili TPN pia ni kwa ajili ya watanzania wote wenye mtazamo wa kupenda maendeleo ambao nao wanafit katika maelezo yangu hapo juu. Katika hili TPN inaangalia maaendeleo ya nchi kwa ujumla.
Kuna sheria ya asili ambayo binafsi naamini "Every Human Being is Capitalist at Heart" ni vema kuwawezesha walio katika level ya kufanikiwa kirahisi ili na wao wawasaidie wengine. The whole issue here is a question of Networking.
Kuhusu website yetu, hilo nakubaliana na wewe kuwa ina mapungufu sana na tunaomba msaada na mwongozo kwa wale wenye taarifa ili tuweze kulifanikisha. Tungependa tovuti iwe nzuri na kubeba pia mambo makuu na ya msingi. Please assist on this if u know someone.
Kuhusu vision ya kujenga taifa lenye maarifa ifikapo mwaka 2050. Nakumbuka kulikuwa na mvutano sana katika hoja hii. Wengi walidhani kuwa tuwe na vision ambayo ni realist kuwa achieved na 2050 ikakubalika. Hata hivyo tuko katika process ya kutengeneza Strategic Plan na Road Map kama ulivyoshauri pia. Kama kuna mawazo bora tafadhali tusaidiane.
Kuhusu ada ya uanachama: kabla ya kufikia muafaka wa ada, tulijaribu kufikiria sana na kukubaliana kuwa ni vizuri tuepukane na misaada kila inapowezekana ambayo baadhi huwa na masharti mbalimbali. Kwa kuzingatia hilo tulitaka TPN iwe na uwezo wa kujiendesha na wakati huo huo wanachama walio wengi waweze kuimudu ada zake. Kilichokubaliwa kwa sasa ni kuwa Ada ya Usajili ni TZS 100,000/= na unaweza kuilipa kwa awamu. Lakini pia kuna subscrption Fees ya kila mwezi ya TZS 20,000 ambayo unaweza kuilipa kwa mwezi au kwa mkupuo. Ada hizi hutumika katika kuendesha chama ikiwepo kulipa mishahara, uandaaji wa Workshops nk. Mpaka sasa kwa karibu mwaka mzima TPN imekuwa inajitegemea bila kutegemea msaada katika shughuli zake za kila siku. Katika uandaaji wa Semina wakati mwingine tumekuwa tukipataa sponsors.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadau na wanachama wa TPN wenye makampuni yao ambao wakati mwingine wamekuwa wakitoa sponsorship katika Networking Events.
Kuhusu focus ya TPN katika katiba: tuliopewa kazi ya kuandikisha TPN tulianza kuliona mapema hili. Huenda tulikuwa na malengo mengi sana ambayo hayakuwa yana-focus kwenye kitu kimoja. Katika AGM inayofuata, tutawashauri wanachama wafanye maabadiliko na kuboresha zaidi. Wenye maoni bora pia mnakaribishwa.
Kuhusu membership, kwa uhakika membership iko open kwa Wanataaluma wote waliopo ndani na nje ya nchi. Na hata sasa tunao wanachama ambao wako nje ya nchi. Nadhani itabidi tuliangalie hili kimaandishi tuliboreshe vipi bila kuleta mkanganyiko.
Mwisho na mimi nakushukuru sana ndugu yaangu GM kwa mchango wako. Napenda kuwahakikishia wote michango yote inayotolewa itafaanyiwa kazi.