JF Karibuni Tanzania Professionals Network

JF Karibuni Tanzania Professionals Network

Jamani hivi JF ni anti ccm tu? hili niswali ambalo naona niulize humu ndani. maana sielewi ccm imeingiaje hapa ktk tpn?
ina maana akifanya mbowe ufisadi haandikwi huku? mi naona humu tunachukia mabmbo maovu from what ever source ccm and the like. mnatutisha sisi tulio neutral na tunakaataa maovu yote sio nusu nusu je hatustahili?
msifanye huu ukawa mtandao wa upinzani naamini hata nia ya waanzishaji haikua hivyo. MODERATORS PLEASE HELP KAMA NIMEKOSEA HAPA.
Afterall kujiunga ni hiyari ameomba utembelee website uwasome ukikubaliana sawa au la basi . na hakika ww hata ujatake time kwenda huko ila basi tuu tunatumia uhuru wetu vibaya.

Mzalendo Kamonga, asante pia kwa mchango wako na pia msimamo wako wa kutoegemea upande wowote.

Binafsi naamini sana katika uhuru wa kutoa mawazo na kushindana kwa hoja. Hofstede alitumia uhuru wake ingawa inawezekani maoni yake hukuyapenda.

Napenda kuamini kuwa JF haijali itikadi za vyama kwa wanachama wake kama ilivyo TPN, lakini wanachame wake wanaweza kuwa na itikadi mbalimbali. Hivyo tofauti ya mawazo na jinsi ya kuyawakilisha itakuwepo.

Tafadhali tuvumiliane waungwana. Asante ndugu yangu kwa concerns zako. Nadhani ujumbe utakuwa umewafikia walengwa.
 
Sanctus Mtsimbe,

You are the man. Baada ya kusoma post yako na majibu yako kwa hoja mbalimbali nashawishika kuamini kwamba upo makini katika kutekeleza malengo na ndoto za TPN. Hongera sana, mimi nakuunga mkono 100%. Kila hatua ya kutusogeza mbele na kulitoa taifa letu katika aibu tuliyo nayo inapaswa kuungwa mkono sana.

Mzalendo Kitila Mkumbo, asante sana kwa kunitia moyo ingawa natambua pia kama binadamu ninaweza kuwa na mapungufu fulani fulani.

Hata hivyo michango yetu wote hasa ile ambayo itakuwa ya uchambuzi na kuboresha kwa hakika inaweza kutusaidia sana tukiwa kama watu binafsi, jamii na kisha kama taifa katika kujiletea maendeleo. Asante sana Mzalendo
 
. . . . . JF sio mtandao wa Upinzani bali ni mtandao wa kupinga yale yote ambayo yanafanywa kuwaumiza Watanzania wa Kawaida kama mimi na wewe. Mtandao wa Watanzania wenye uchungu na Tanzania.

JF: WHERE WE DARE TO TALK OPENLY!!!

Asante Mzozo, hakika uliyosema yana ukweli. Na ni pale tu kutakapokuwa na Mtandao mkubwa wa Watanzania wenye uchungu na Tanzania au Wazalendo, ndipo maendeleo ya kweli yanaweza kupatikana.

Ni ndoto ya TPN kuwa na Mtandao nchi nzima ambao hatimaye utasaidia kuleta maendeleo katika nchi.
 
Sure, but we should not go that route blindly bila kuhoji. Nimefuatilia huu mjadala nikitegemea ningepata kuelewa what TPN is all about. Huenda nikaanza kuamini kuwa hawa TPN ni wasanii.

Mzee Mkumbo nilitegemea ungesema mawili matatu kuhusu mjadala huu?
.

Lazydog nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%. Kitu usichokijua ni sawa na usiku wa kiza. Ni vema kufanya uchambuzi wa kina kabla hujaamua kujiunga na TPN. Please take your time. Afterall kujiunga na TPN si sheria ni suala la hiari ya mtu.

Hata hivyo napenda kukuhakikishia kuwa TPN si chama cha wasanii. Mafanikio machache katika mwaka mmoja yaliyopatikana yanadhihirisha hivyo. Naamini katika mwaka mmoja ujao mtazamo wako huenda ukabadilika. Jipe muda tu . . . LOL.

Mzee Mkumbo, kwa nini usiseme mawili matatu ili Mzalendo Lazydog naye afurahi? . . . LOL. Asante ndugu yangu Mzalendo Lazydog kwa mchango wako. Hata tahadhari kama hizo zinaifanya TPN iwe makini zaidi.
 



Kuna watu natambua uwepo wao kwenye online community. Ila mnapokuwa wakimya, napata picha kwamba you guys know something we don't; but why the secrecy? Sanctus Mtsimbe is being so diplomatic on his responses. Nikisema TNP wasanii nitakuwa nimekosea? I'm outta here! 😡

"wakimya" - nikiwa na maana when someone say something but avoid to speak about what you expected her to say on the matter.

.

Lazydog . . . unanifurahisha sana. Kama watu watakuwa wanaogopa kusema kwa kuwa natumia jina langu halisi, basi itakuwa ni kitu cha ajaabu sana. Binafsi siwafahamu wote mnaochangia zaidi ya baadhi ambao wameniandikia katika email na kujitambulisha ni akina nani au ambao wameomba kujiunga na TPN.

Naomba msiogope kutoa maoni yenu. Kuweni huru na naamini kuwa mnatoa maoni yenu kwa uhuru. Asante kwa angalizo hilo Mzalendo Lazydog.
 
Sanctus,

naona TPN mnatumia sana neno Mzalendo mnamaanisha nini?
 
Kitila Na Mwana Msimbe!!

Nilichojifunza Humu Jamvini Ni Kwamba, Usipokua Makini... Unawez Kukosa Usingizi!!

Tpn Ni Nzuri Na Kama Haukidhi Kuwa Member Ni Bora Kuacha Walengwa Wa Tangazo, Nina Wasiwasi Na Baadhi Ya Walio-negative... Hawakubali Kwamba They Dont Fit In Every Network

Keep It Up BWANA Msimbe, Na Wapinzani Wa Tpn Kalaga Baho!!!!!!!!

MTM - Mtanzania wa Kiume . . . LOL Asante sana kwa mchango wako. Wakati mwingine si lazima wote wakubaliane na mawazo ya TPN. Kitu kimoja ambacho nami nimejifunza ni kuwa kadiri ya wachangiaji wanavyo crticise ndivyo mnapata nafasi ya kujua wapi penye upungufu, wapi parekebishwe na nini kifanyike.

Asante sana kwa maneno mazuri juu ya TPN.
 


Ndo maana hatupendelei watu kutumia majina yao halisi humu jamvini. Ukiwa rafiki na mtu na unajua anatumia jina gani JF mara nyingi kabla ya kuhoji chochote asemacho utasita kufanya hivyo, wakati ambavyo kutojua mtoa hoja ni nani pengine ungeshiriki kikamilifu.

.

Asante tena Lazydog, ni bahati mbaya sana kama mtu atashindwa kutoa maoni yake eti kwa sababu tu nimetumia jina langu. Nimepata kusoma humu kuna wengine wanatumia majina yao kama Mh. Dr. Slaa, Mh. Zitto nk. Nilidhani hili ni suala la uamuzi binafsi tu ambalo haliwezi kumuathiri mchangiaji.
 
Sanctus,

Kwanza naomba msamaha kama maswali nitakayouliza yameshaulizwa au kuzungumziwa kwenye kurasa zilizopita. Duh maana kurasa ni nyingi sana kuanza kuzisoma....

Anyway, mimi maswali yangu ni :-

1. Hii TPN imejizatiti kiasi gani katika the all corporate politics nchini mwetu? Labda nifafanue swali katika njia nyepesi zaidi, je memba wa TPN wanaweza ku-mention "proudly" uwanachama wao wa TPN kwenye interview as a way ya ku-show how professional they are? In other words, je TPN inaweza kuongeza nguvu ya kuvutia recruiters ikiwa listed kwenye CV?

2. Je TPN ina provide some sort of recommendations kwa wanachama wake ambao wako kwenye job hunting, seek profession advancement, et al..?

3. Je TPN ina provide career mentoring kwa wanachama ambao pengine wana seek mabadiliko katika professions zao?

Ni hayo tu kwa sasa hivi....
 
Lazydog nakubaliana na wewe kwa asilimia 100%. Kitu usichokijua ni sawa na usiku wa kiza. Ni vema kufanya uchambuzi wa kina kabla hujaamua kujiunga na TPN. Please take your time. Afterall kujiunga na TPN si sheria ni suala la hiari ya mtu.

Hata hivyo napenda kukuhakikishia kuwa TPN si chama cha wasanii. Mafanikio machache katika mwaka mmoja yaliyopatikana yanadhihirisha hivyo. Naamini katika mwaka mmoja ujao mtazamo wako huenda ukabadilika. Jipe muda tu . . . LOL.

Mzee Mkumbo, kwa nini usiseme mawili matatu ili Mzalendo Lazydog naye afurahi? . . . LOL. Asante ndugu yangu Mzalendo Lazydog kwa mchango wako. Hata tahadhari kama hizo zinaifanya TPN iwe makini zaidi.



Katika kushawishi na kujibu hoja nimekukubali mzee. Ni mategemeo yangu kwamba sifa hii inafanana na utendaji kazi wako ulivyo.
Upatapo muda siku nyingine utueleze kwa mifano hayo *mafanikio ya mwaka mmoja unayoyazungumzia. Itasaidia sana kushawishi vichwa ngumu kama mimi.
Asante.



NB: *Mafanikio kwa members

.
 
Asante sana Mzozo . . . . Sina uhakika nililala saa ngapi, lakini nadhani ni baada ya saa nane na nusu usiku . . . LOL wakulu bado hawajanitoa kwenye Tanuru la moto . . . LOL

Najitahidi kuzingatia na kuelewa yote yaliyo muhimu. Nashukuru tena kwa mchango wako pia.




Katika kushawishi na kujibu hoja nimekukubali mzee. Ni mategemeo yangu kwamba sifa hii inafanana na utendaji kazi wako ulivyo.
Upatapo muda siku nyingine utueleze kwa mifano hayo *mafanikio ya mwaka mmoja unayoyazungumzia. Itasaidia sana kushawishi vichwa ngumu kama mimi.
Asante.



NB: *Mafanikio kwa members

.

Asante kwa majibu yako.

Kuhusu kuachiliwa JF, usijali ukitoka hapa utatoka na digrii ya juu ya utetezi wa hoja kutoka chuo kikuu cha JF!

Kila la kheri kwenye mabadiliko ya katiba-ni muhimu sana.
 
The confirmation process continues, Senator Kuhani exhaustively expounges extreme extrapolations, as expected. Details aside, president Mtsimbe exhibits a rare flare of tenacious "toe-to toeing" and tenets of tough-cookieness without as Mwanakijiji put it "snapping" or getting condescending and cocky.

Whether this hue of humility will hang to heights or go to the hang heights remains to be seen.

With reservation, I will cut him and his organization some slack, short of joining at least during the vetting period due to privacy concerns.

Just as there is no trade of between having a phone with a sizable screen and having a small phone (challenge to engineers) there is also no trade off between joining an effective real world organization and anonimity.

Mzalendo Pundit, one of the things which I noted about your contributions, is your ability to use above the normal level vocabulary. I have never seen before and I must admit you must be good in an advanced english . . . LOL. I am not that much good.

I also admit Mzalendo Kuhani have been very good in cross-examinations! This has made me sometimes to go back to the books and fetch some more facts before I could respond. At the same time I had to compromise with his style of questioning and language while also trying to understand him to benefit from his contributions. I sincere thank you if your observations in this has made any impact.

As mentioned in one of my responses, joining or not joining TPN is voluntary and not mandatory. Although I have invited JF members to TPN, it is also advisable to weigh out the facts and see for yourselves if it makes any sense to join. No hurry, take your time. My strong belief is that within another one coming year TPN will be able to demonstrate more on how its members can benefit effectively. This is in addition to what has been achieved so far.

Asante sana Pundit. I will take into consideration your cautions.
 
The good president himself invited critical analysis in the hope that it will help check and even iron out a few things. If some senators are asking one too many questions, it is not because they love TPN and it's ideals less, it is because they love efficiency, transparency and accountability more and hope to have these to the maximum at TPN.


Pundit . . . very well spoken. Let people talk what they feel freely and without fear. What I promise is: I see both criticizing and supporting arguments to be useful in moulding TPN to be a better organization. I also agree that questioning creates a sense of Efficiency, Transparency and Accountability.
 
It is unfortunate that some of us are reduced to labelling the few detail oriented (or pedantic, depending on your viewpoint) souls in here as "walio negative" and "wapinzani wa TPN"

The good president himself invited critical analysis in the hope that it will help check and even iron out a few things. If some senators are asking one too many questions, it is not because they love TPN and it's ideals less, it is because they love efficiency, transparency and accountability more and hope to have these to the maximum at TPN.

Agreed Pundit;

It is even more dissapointing when a few can conclude ones intention [and reduce them to size] without asking themselves why one is thinking that way? the point we have to note always is how one asks questions... I read the thread and i know who I was targeting; from questions you can learn walio skeptics, positives, ignorants, radicals as well as people like you!!
 
Last edited:
Mzee Mkumbo, kwa nini usiseme mawili matatu ili Mzalendo Lazydog naye afurahi? . . . LOL. Asante ndugu yangu Mzalendo Lazydog kwa mchango wako. Hata tahadhari kama hizo zinaifanya TPN iwe makini zaidi.

Nimetingwa sana. Nikipata nafasi nitachangia mawazo yangu kikamilifu. Lakini nimeona nia ni nzuri sana maana ni katika harakati za kuzidi kutufungua watanzania na kutusogeza hatua moja mbele. Mimi kitu chochote hukiangalia positively kwanza kabla sijakitafutia kasoro. I always give the benefit of doubt to any noble cause, such as this one!
 
Sanctus,

naona TPN mnatumia sana neno Mzalendo mnamaanisha nini?

Asante GM, neno MZALENDO limekuwa likitumika zaidi kama title ya mwanzo ya mwanachama au shabiki yeyote wa TPN kama vile vyama vingine vinavyopenda kutumia title ya MHESHIMIWA.

Maana halisi ya neno MZALENDO ni mtu anayejali utaifa, mwenye uchungu na nchi. Actually kwa kiingereza lina maana ya PATRIOTIC au NATIONALIST.

Imekuwa ni vema zaidi kutumia title hii kuliko ile ya MZAWA ambayo kisiasa imekuwa ikileta hisia a kibaguzi. MZALENDO halibagui mtu.

Kwa kutumia title ya MZALENDO mnaonyesha umoja wenu katika kujali maslahi ya nchi.

Hakuna kiongozi yeyote wa TPN anayekuwa addressed kwa kuitwa MHESHIMIWA haijalishi kama ni Rais, Katibu Mkuu, Treasurer au Kiongozi yeyote wa Executive Committee. Wote hawa wanatumia title MZALENDO.

Kuna baadhi ya Waheshimiwa halisi kwa maana ya Mawaziri na Wabunge na Viongozi wa Vyama vya kiraia na kisiasa ambao huwa wanahudhuria mikutano ya TPN. Kuleta zana sawia ya kujali taaluma zote, huwa nao tunawa-address kwa kutumia title ya MZALENDO badala ya ile ya MHESHIMIWA. Tunadhani kuwa katika Wanataaluma neno Mheshimiwa linaleta matabaka ya wenye vyeo na wasio na vyeo vitu ambavyo si vigezo katika TPN. Na ukizingatia hali halisi ya mwenendo wa mambo Tanzania, MZALENDO could just be the best title.
 
Agreed Pundit;

It is even more dissapointing when a few can conclude ones intention [and reduce them to size] without asking themselves why one is thinking that way? the point we have to note always is how one asks questions... I read the thread and i know who I was targeting; from questions you can learn walio skeptics, positives, ignorants, radicals as well as people like you!!

I guess maswali yangu yana fall hapo kwenye bold. Maana naona yamechuniwa... lol
 
Mgoyanyi, usiogope yakhe . . . Hili si tego ndugu yangu. Huwezi kunaswa na wala usihofu . . . LOL

Ungekuwa mtego ungesema "ogopa yahke...Hili ni tego ndugu yangu. Unaweza kunaswa na hofia." Halafu ungecheka?

Linaweza kuwa tego vile vile, for all I can smell.

Watu wamekuwa wowed kwamba wewe ni kiongozi mzuri kwa sababu huwaki waki, unatumia diplomatic poise. Hata Kikwete nae hawaki waki. Mzee ana hulka ya kucheka cheka yule. Anamshinda hata Nyerere na Mkapa kwa temperament ya kutofoka foka na kutukana tukana. Lakini hiyo ni kama wajibu wa Kiongozi. Unategemewa uwe hivyo. Hupati shada la maua kwa kuwa even-tempered, hususan Riasi wa chama. Lakini, kwa hilo, umewateka watu hapa.

Chama chako kinaweza kuwa tego kwa sababu "Chama cha Wasomi na Mashirika" hakiwezi kuwa na Katiba imeandikwa kana kwamba ni ya kikundi cha Sindimba cha watoto. Inajipinga kila mahala. Na Raisi wake anashindwa kuielezea. Unakubali Katiba imepinda halafu unaitetea. Hai make sense. Huwezi kuwa na Katiba ina clause moja inafuta clause mbili za juu yake, tena kuhusu kitu rahisi kama nani anaweza kuwa Mwanachama.

Hicho chama ni cha Watalaam kweli? Kuna mainjiani, na waalimu, na madaktari, na wajenzi, na wachumi, na wanamuziki, na wahasibu, na manesi, na wafanyabiashara, na polisi humo kweli?

Au ni usanii?
 
Back
Top Bottom