JF Madaktari msaada wenu juu ya hii alama inaongezeka kila kukicha

Vitiligo.

Ni ugonjwa wa ngoji ambapo kinga yako mwenyewe ya mwili inaharibu melanin (kimakosa), pigment muhimu unayoleta rangi ya mwili.

Huanza hivyo hivyo taratibu na kuenea.
Maeneo yanayopendelea zaidi kutokea ni sehemu zinazopigwa sana na jua, hivyo uso na sehemu za kichwa ni namba 1, mikono na sehemu za shingo, ikifuatiwa na viungo vyengine vya mwili.

Matibabu ya vitiligo hakuna, ila kuna dawa huwa zinasaidia kupunguza athari na muda mwengine hata kutibu kabisa.. tatizo ni upatikanaji mgumu na gharama kubwa!
 
Hapa umemaliza kila kitu mkuu, njia mbadala nyigine ni skin lightening unabadili rangi ya ngozi yako ili ifanane na yale mabaka ya vitiligo ziko product maalum (sio mkorogo). Lakini sio njia salama sana kwa wakazi wa kusini mwa jangwa la sahara na jua la utosi
 
Hizo dawa zipo kawahi tu hospitali.
Kama ni vitligo anza mapema, Bibi yangu aliumwa hiyo kitu mpaka amefariki mi nilikua simwelewi tu.
Nikimwambia ukatibiwe hospitali hataki.
Ilikua usoni pote
 
jamani hii ALAMA haiwashi wala haiumi ila inaongezeka kila Siku naona mabadiriko​

View attachment 3524567
Kipindii BALOZI POLE POLE AKIWA CUBA ALIFANIKISHA ALIWALETA WATAALAMU NAKUMBUKA WALIFANYA JOINT NA HOSPITALI ZA TANZANIA..

WA CUBA WANA DAWA ZA KUUTIBU HUU UGONJWA wa vitiligo unatibika ila ukizembea utageuka kuwa kama PUNDAMILIA.

Ngoja nikutafutie mawasiliano ya KUWEZA kupata huo msaada wa wa CUBA nadhani still wanatoa msaada wa matibabu ya vitiligo hapa bongo...

Au unaweza kwenda UBALOZI WA CUBA ukapata MAELEKEZO zaidii au kama Kuna wenye access watakusaidia hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…