JF member leo share weakness yako hapa

Kila mtu ana weakness yake sasa ebu tuseme leo tuone kama hivi vitu huwa vinafananaga kwa wengi..
Mimi bhana weakness yangu ni churaaa yani churaaa nikipishana na mkia haswaa lazima nigeuke nyuma niutathmini.
Nahonga sana siku hizi
 
Utakufa kwa umaskini kama wewe ni pangu pa kavu,
Lasivyo badili lifestyle mkuu.
 
Mkuu stori yako imenigusa aise.
Huyo mtoto kanikunbusha kichaa mmoja.

Siku moja nilikuwa niko saloon kwa rafiki wa rafiki yangu(ni mmama)mwaka jana kipindi cha corona kilivyokuwa kimeshika hatam.kazini tulifunga so nikawa niko nyumbani kwa kipindi kirefu kidogo,pesa sikuwa nayo kwa kipindi kile.

So nilikuwa na 2000 tu hapo sijala mchana wala kunywa maji..nikaenda kununua ugali 1500 ikabaki 500 nikasema hii nitainunulia maji ya kunywa kurudi nyumbani nitaprint tu(kutembea).basi nikajipigia nguna yangu fresh nikachukua maji 1.5 (500) nikanywa kidogo sana.

Baada kama ya dakika 30 akaja mkaka(kichaa)amechafuka na ananuka akasema anakiu cha maji...nikiikumbuka hii siku machozi hunitoka hata hapa ninapoandika.pale saloon kulikuwa na maji yangu pamoja na ya mama mwenye saloon.

Yule mama alipomuona yule mkaka na jinsi anavyonuka alimfukuza kama mbwa.sijui unaielewa ile tone ya kumfukuza mbwa ee..eee hiyo hiyo sasa.haki nilijisikia vibaya mno🥺🥺nilimkata yule mama jicho(alijua)
Yule kaka(kichaa)akawa anatabasamu tu.

Kumbuka ninamaji ambayo yakiisha hayo sina mengine na pesa sina hata ya nauli ya kunirudisha nyumbani.yule mama alipogundua sijapenda alichokifanya akajibaragusa kutaka kumpa maji nikamwambia usimpe yako nitampa yangu.
Yeye kanyanyuka kumpa na mimi nikanyanyuka kumpa maji,lakini cha ajabu ni kwamba yule kaka(kichaa)aliyachukua maji yangu akanywa,yote kwa wakati mmoja.kisha akatabasamu akaondoka huku kaishikilia suruali yake(nilibakiwa na kifuniko mkononi)

Baadae nikapata nauli ya kunirudisha nyumban na pesa pia ya kutumia niliipata.tangu hapo yule mama nilimchukulia tofauti kabisa.

Nalitafakari sana.tunakutana na Baraka zetu lakini tunazifukuzia mbali kwa sababu zimekuja kwa zile njia ambazo hatutaki zije nazo,njia zenye muonekano wa kudhalilisha na kufedhehesha machoni pa wanadamu.
 
Sure mkuu. Inaumiza kuona unaweza kusaidia ila hujasaidia, binafs hiyo ck ntakesha najisonya tu kwa kushindwa kufanya kitu. Wengi huamn baraka za moja kwa moja na hizo ni nadra sana kuzipata.
Mm rafk yng alivyokuta n mwepesi wa kusaidia sana "ogopa sana kumsaidia mtu vitu kama hela nk anavyobaki navyo uliyemsaidia" nikamwuliza kwann? Alinambia wengine huwa si binadamu but hilo halijawahi kamwe nizuia kusaidia nikiwa na uwezo huo😇

Hongera pia kwa huo moyo wa kusaidia
 
Ni kweli asemacho rafiki yako..sasa hivi binadamu wamekuwa si waaminifu kabisa...unaweza kumsaidia mtu msaada wako ukaja kukutesa.

Lakini hiyo haituzuii tusisaidie watu.
Kabla hujasaidia kabidhi kwanza msaada wako mikononi mwa Mungu..na Mungu atashughulika nao kwa namna tusiyoijua.sadaka inalinda,inaponya,inaadhibu watesi wako,sadaka ni kila kitu.

Kwa pamoja tuendelee kutoa misaada kwa chochote tunachojaaliwa....namuomba aendelee kukuza kipato changu.kuna mambo ambayo yanahitaji pesa kuyatatua.

Ningepata mdhamini ningeshukuru sana.☹️☹️.
Ndoto yangu ni kusaidia watu.mimi ninauhitaji lakini kuna watu wauhitaji zaidi yangu.


Ni kawaida yangu nipatapo kazi sehemu..basi mshahara wangu wote(si mshahara mwingi lakini huo huo) kununua mahitaji na kwenda kuwapatia watoto yatima.na kila mwisho wa mwezi natoa asilimia kadhaa.

Siku hiyo nilienda kituo fulani kigamboni ni mda kidogo...nilikutana na vijana,wasichwna kwa wavulana..nikakutana na watoto wa kiume (miaka kama saba au nane)mmoja alikuwa amekaaa kwa huzuni mno🥺🥺😥😥😥😥 niliwaza mbali mno niliumia mno na ninaumia mpaka sasa(siwezi kuendelea kusema)maana nilitaman nimchukue aonje mapenzi ya mama kupitia mimi lakini Mungu wangu sikuwa na uwezo huo jamani🥺🥺🥺🥺.

Na iman humu ndani kuna watu wanandoto,mawazo na uwezo wa kusaidia watu wenye uhitaji..ikikupendeza tushikamane kuweza kuwasaidia kwa kadri Mungu atakavyosema nasi.

Kuna watu wanahitaji japo kuonyeshwa upendo kwa dakika kadhaa kuweza kubadilisha maisha yao.

Nimesaidiwa mno mpka kufika hapa nilipo.walionisaidia wanaishi moyoni mwangu na wataendelea kuishi mpka mbinguni.

Nataman kuishi mioyoni mwa watu kwa mazuri,natamani kuwa ngazi ya kuwapandisha wenzangu waliokwama.nafanyaje mimi Chakorii??🥺🥺🥺🥺 nifanyaje wana Jf???🥺🥺🥺
 
Hakika wapo wengi tu ila wengi wanaishia kuwaza anasa, jambo kama hili la mhimu wachache sana wanaweza kujitokeza na huenda wakapita bila ata kukomenti kitu utadhani hawajaona haja ya kufanya hivo.

Umewaza mbali zaidi na hata mm natamani kufanya kitu ila ndo hivo tena hiyo pawa naikosa. Ila najua wadau wenye roho za kusaidia watakuwa wameona, nawaombea tu Mungu awaguse waone umuhimu. Kuliko kipato chako ukakitumia kunywea bia bora bia moja ikamsaidia mtu mwenye uhitaji.
Daaa, Ila Mungu ni mwema atafanya jambo Chakorii
 
Amen.Mungu ni mwaminifu mno mkuu..huwa naamini hivyo..Mungu kufanya njia pasipokuwa na njia.kwa wakati wake atafanya mlango wa kutokea.

Tuwe na Imani na kumuomba Mungu atusimamie
 
Amina kibwa mkuu
Amen.Mungu ni mwaminifu mno mkuu..huwa naamini hivyo..Mungu kufanya njia pasipokuwa na njia.kwa wakati wake atafanya mlango wa kutokea.

Tuwe na Imani na kumuomba Mungu atusimamie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…