Katika mitandao yote kwa hapa Tanzania ni JamiiForums tu ndio utakuta nyuzi na majadiliano magumu yenye kufikirisha bongo na hata kuumiza akili.
Mitandao mingine yote ukiondoa wanaharakati wachache na wafanyabiashara wanaofanya matangazo ni utumbo na uchafu mtupu. Maudhui yaliyopo ni ya akili ndogo sana, umbea wa uswahilini, pamoja na content za GenZ za ki-teenagers au zenye utoto mwingi.