Hii noti inanikumbusha Mzee mmoja alikuwaga mfanyakazi katika mgodi wa Mwadui, enzi hizo wavuta tumbaku walikuwaga wanatumia maganda ya mahindi kusokota sigara. Sasa huyu Mzee alikuwaga analima mahindi kwa wingi Sana akivuna anayatundika nje kwenye 'NSHIGITE' msiojua kisukuma mnisamehe Bure. Ukipita kwake ukamkuta yeye halafu ukaomba ganda la mahindi anaingia ndani anakuja na hiyo noti anakuambia ganda hili hapa.
Kijijini kwetu tuliibatiza tukawa tunaiita jina la huyo Mzee.